IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II!

Du! Juzi tulipokutana pale msibani kumsindikiza mpiganaji Freddy Mtoi, nilitaka kukwambia kitu kimoja muhimu na kikubwa sana. Hatukupata nafasi bahati mbaya. Andiko lako hili la leo du! Siongezi sana.

Lakini kinachoendelea kunishangaza katika suala hili, specificallybla Mwangosi, hivi ni kwa nini mpaka leo wanahabari tumeshindwa ku pressurize vifaa vya kazi vipatikane. Alikufa akiwa na notebook, computer na CAMERA mikononi mwake. Hata kama kamera haikuwa ikichukua picha vizuri kutokana na purukushani, bado ilikuwa inachukua sauti. Nimeshajaribu kuzungumza sana hili lakini naona, nji...sijui ni sauti ya nyikani.
 
Maneno mengi hayavunji mfupa kaka Pasco, Mwaga strategies za kufuatwa Tuanzie wapi, wengine sisi ni Librarians Hatujui hata sheria moja.
Mkuu pasco uko sahihi ukitaka jamii ibadilike anzia kuwaelimisha wajue haki na wajibu then strategies zitafuata
 
Mimi ninahakika sasa serikali ya chama cha mapinduzi inatapatapa maana inaona kifo chake kile pale 2015. ndio maana utawasikia na kauli za kukata-tamaa kama "lolote na liwe" sasa wanaendeleza utekelezaji wa kauli zao
hata mwenyekiti wao kawaambia kwamba wasitegemee tena kusaidiwa na usalama wa taifa kwenye uchakachuaji wa kura kama ilivyoakua 2010, wajipange upya.
 
Mara nyingi nimekuwa nikiangalia na kujiuliza jinsi unavyo shughulikia machafuko..Definately you don't act professionally..Na mtu akiangalia kwa makini atagundua namna unavyo tenda kazi zako ni kwa maelekezo ya wanasiasa. Sina shaka kuona ukiwasikiliza wao sababu ndio walio kuweka hapo lakini mwisho wa siku amini ulicho kichumia juani hata siku moja hutokilia kivulini..bali kuleee THE HAGUE.

Msione akina Charles Taylor, Milosevic na wengine walitenda tofauti saaana na ninyi. Nina imani kabisa kwa mtindo huu wa utendaji wako na jeshi lako ukiongozwa na chama tawala kama mkiendelea hivi mpaka uchaguzi wa 2015 na baada ya hapo hamtobaki salama. Nguvu zote mlizo tumia kutuibia rasirimali zetu mtazipoteza bure kwani mtaishia The Hague na mali mlizo pora kurudishwa kwa wananchi.

------ yeye anachojua katika kuthibidi hali tete ni kutumia mabomu, risasi, maji ya kuwasha, na usalama wa taifa kutesa na kuua. Hana mbinu nyingine wala uwezo wa kufikiri zaidi ya huo. Mara zote kila jambo analifanya kwa ubabe, badala ya kutumia akili anatumia nguvu nyingi. Mnapo kuwa na kiongozi wa nchi wa aina hii basi mna hasara. Pamoja na matukio mengi tuliyo shuhudia haya ya sasa Mtwara yana dhihirisha udhaifu mkubwa tena sana wa huyu jamaa. Haoni mbali..anacho ona ni pesa waliyo pokea kwa kutoa kandarasi ya kujenga bomba la gesi hadi Dar. Hiki ndicho kinacho wahangaisha sababu mtu ukisha pokea kitu lazima utimize mlicho kubaliana na aliye kupatia.

Kitendo cha TPDC kutokuwa na copy ya mkataba baada ya kamati ya Bunge ya mashirika ya umma kutaka kuuona na wao kupiga danadana eti uko Wizarani kunaleta shaka kubwa tena saaana. Katika mantiki ya kawaida ukimuuliza ------ sababu za msingi za kutaka kwa nini bomba lijengwe badala ya umeme kuzalishiwa Mtwara hana. Kumbukeni mkataba ulisainiwa chini ya FISADI NGELEJA. Yalee!! ya Karamagi kusainia mkataba hotelini. Kwa hiyo hapa hakuna kitu zaidi ya watu kuwa tayari wamesha kula pesa za wachina hivyo lazima watekeleze au warudishe fedha. Simnajua tena mambo ya 10%?

Kwa hiyo wako radhi wana Mtwara wafe lakini wachina, wao na familia zao wanufaike. wanamtwara na kwingineko katika nchi hii, kumbukeni maneno ya kuungwa mkono na Mh.Mkono kwamba wao Buhemba wanalia kwa kuachiwa mashimo kwa sababu waliiamini sana serikali na ndiyo yaliyo wakuta. Serikali hii ilipotufikisha inabidi kila mpango wanaokuja nao lazima tuuchunguze kwanza kabla ya kukubaliana nao sababu nchi hii mtu hafanyi kitu kama hana faida nacho. Na ikiwa kweli hato faidika nacho(hao viongozi) atakipinga. Na hii ni tahadhari kubwa sana kwa wana Kigamboni na mpango wenu wa mji wa kisasa.

Wanajamvi nimetoka nje kidogo ya mada ya onyo kwa IGP nikijaribu kuweka bayana aone maelekezo anayopewa na wanasiasa yalivyo na hila na upotoshaji wa hali ya juu ilimradi wanafanya hivyo kutimiza azma yao ya kupora rasilimali za nchi hii japo najua haya yote anayajua lakini kaamua ku act un professionally. Tuna hitaji jeshi lililo karibu zaidi na wananchi sababu hata hao viongozi anao watii waliwekwa na wananchi. Ilibidi awe mshauri mzuri pale anapo ona haki za wananchi zina porwa au kandamizwa na kwenda mbali zaidi kwa kujiuzuru kuliko kushiriki genge la mafisadi.

Hakika kati ya list ya majina itakayo takiwa na The Hague IGP hatokosa iwayo yote.
 
bwana pasco vipi kuhusu hili la kibanda-lwakatare?
Mkuu Jingalao, kama la Ulimboka hadi majina waltajiwa, na hawakufanya lolote, unategemea kwa kibanda, watafanya nini?!. Ila kwa vile jeshi letu la polisi, huficha udhaifu wao kwa kutumia "scapegoat", msijekushangaa hiyo kesho, mtu asiyetarajiwa akafikishwa mahakamani kwa kesi ya Kibanda, kwa kisingizia cha "aliyekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama", "kwa vile "jamaa" walipanga kumshughulikia mwandishi fulani, na kwa vile Kibanda pia ni mwandishi, then itajengwa hoja, walianza na Kibanda na kufuatia kelele nyingi, ile video ilikuwa ni ya maelekezo ya kubadili strategies!.
Pasco.
 
Ukishakula nyama ya mtu ni ngumu sana kuiacha, hii ni laana kubwa sana kwa wauaji hawa damu ya waliouawa haitawaacha kamwe salama wauaji. Sasa kama watawala hawachukui hatua ina maana wanaunga mkono wauaji.
 
Mkuu Pasco, jiandae kutembelea Mtwara maana huku nako hakuna wanasheria wakutusaidia kwani inavyoonekana serikali inajiandaa kuichukuwa gesi asilia kwa nguvu ila balaa kubwa litokea ambalo halijawahi kushuhudia katika nchi hii, na kwa hili njia ni nyeupe kwa shemeji kuelekea the Hague maana ameepa kuwa ni lazima bagamoyo iwe kama dubai kwa kutumia gesi asilia ya Mtwara ili mapato ya bagamoyo yakaribiane na ya dar es salaam nasi Mtwara tunasema Kusini ni lazima iwe kama honkong'o china kwa kutumia gesi asia na mafuta yetu. hivyo ni lazima kitanuka siku si nyingi shemeji atalianzisha hii ni kwa mujibu wa entellingesia.
 
mimi nadhani ungempa ushauri kuwa kila askari apewe kinanda.watu wakifanya vurugu polisi wampigie kinanda.majambazi wakipora wawatafute kwa kupiga kinanda.
 
Maovu ya Polisi yalianza zamani tokea fujo za Pemba, Mauaji ya mwembe chai , Vifo vya mahabusu waliorundikwa Mbeya, Mtikila na wafuasi wake n.k .

wengi wenu wakati huo mliona Polisi wapo sahihi tu hadi sasa ndio mnakuja kulialia.

Wote mliokaa kimya wakati ule hamja haja ya kuongea wakati huu acheni double standard!!!
 
Mkuu IGP, Kamanda Saidi Mwema,

Hebu Shuhudia!.

attachment.php


Hii ndio picha ya mwisho ya mwanahabari, mpiganaji Daudi Mwangosi aliyefia kwenye uwanja wa mapambano!,

1. Ukiangalia kwa makini, utashuhudia hapa, Daudi Mwangosi alikuwa amepigwa mpaka kuangushwa chini, askari hao 6 wenye uniform na mmoja plain clothes mwenye T-shirt ya blue na kofia nyeusi ameshika bastola kwa mkono wake wa kulia, walikuwa wanaendelea kumpigia nini ili hali hana silaha yoyote, haja resist arrest yoyote, why all this police brutality?.

2. Ukimwangalia Mwangosi, amejishika kiunoni kwa huyo OCD mwenye kifimbo, licha ya kipigo alichokipata, kamwe hakuacha zana zake za kazi, mkuno wake wa kulia bado umeshika kamera yake na baada ya kifo, begi lake la laptop ndogo lilikuwa pembeni yake!. Hivi hawa polisi wote sita, wanamshambulia mtu mmoja tena mwenye camera inaonekana wazi, huku kamanda wao akijitahidi kuwazuia kwa kumkinga, lakini bado wakaona haitoshi ndipo unamuona askari huyo akimuelekezea kabisa mtutu wa bomu la machozi!, whay all this police brutality, why?!.

3. Najua Mkuu Kamanda Mwema, inawezekana wewe hupati muda kupita humu JF kwa vile mtandao huu 'hauna jema la kuisifia serikali yako', na vile vile 'uko bize sana' na shughuli za ulinzi wa raia na mali zao (japo wengine kwa kuwaua kwa makusudi mazima), lakini naamini vijana wako wanapita humu na watakuletea hizi salamu zetu, tunakuomba sana sana sana, stop this police brutality, utakuja kumponza bure shemeji!.

4. Tanzania tuna uchache sana wa wanasheria, na waliopo wengi hufanya kazi kwa wenye nazo, hivyo tangu huu mlolongo wa mauaji ya polisi, hakuna mwanasheria, shirika, wanaharakati, au chama chochote cha siasa kimelifikisha jeshi la polisi mahakamani, simply because wanaokufa wote ni watu hohehahe, familia zao hazina uwezo wa hata tuu wa kujua haki zao za kudai fidia rasmi serikalini, bali uwezo wa kuajiri mwanasheria kuwatetea mbele ya haki kwa kulishitaki jeshi la polisi!.

5. System ilipoamua kumshuhulikia Imram Kombe kwa kutumia polisi wazembe, angalau familia ile ilikuwa na uwezo wa kuajiri wakili jeshi la polisi likashitakiwa na serikali ikalipa fidia ya kifuta machozi cha mamilioni, japo mlizuga kuwa askari wale walihukumiwa vifungo japo hawakuvitumia lakini familia ile angalau chochote kitu ilipata, milioni 300 kwa miaka hiyo, japo hailingani na uhai wa binadamu, lakini angalau ilikuwa sii haba!, hawa wengine wote, hawakuwa na wa kuwapigania lakini kwa Mwangosi, its a wrong button!.

6. This time, tunataka kuwaona vijana wako behind bars, the soonest posible wakati uchunguzi ukiendelea, hata kama utawashitaki wewe kwa negligence, sisi bado tutakushitaki wewe kwa kesi ya madai, ili familia ya Mwangosi angalau ipate pa kushikilia!.

7. Yote vijana wako waliyoyafanya, watu wamevumilia l;akini kwa hili la Daudi Mwangosi, uvumilivu umetufika mwisho maana ni kifo cha unyama wa ajabu kab isa kupata kushuhudiwa na binadamu alietendewa na binadamu mwingine kwa kisingizio cha line of duty!.

8. Nimekupa angalizo, kama usipochukua hatua madhubuti zenye genuinity kama sura yako inavyoonyesha, unaweza kushindwa kuamini kuwa hata 2015 inaweza kuwa mbali, angalia sana usije kujikuta unamponza shemeji, wewe na yeye na wenzenu, mnaweza kujishtukia mko njia moja kuelekea the Hague bila kuamini!.

9. Watanzania ni watu wapole, wavumilivu na wastahimilivu wa hali ya juu, lakini angalia usiwafikishe mahali, wakaishiwa upole, uvumilivu na usahilivu na kufikia kuamua liwalo na liwe, Hata Ghadafi alijua kuwa anapendwa hivi hivi anavyopendwa shemeji, hata Hosni Mubarak alijua anapendwa hivi hivi anavyopendwa shemeji, hata Wamisri nao walikuwa wapole, wastahimilivu na wavumilivu kama Watanzania, hata Walibya nao walikuwa vivyo hivyo, uvumilivu ulipofika mwisho, matokea sote tunayajua, yakitokea ya kutokea, usije kusema hatukukuonya kabla!.

10. Mwisho kiukweli, to be honest, Kamanda Mwema kama lilivyo jina lalo, unaonekana wewe ni mwema genuinely kwa maneno na matendo, na naamini alishataka kuwachukulia hatua vijana wako siku nyingi, ila ulizuiwa na aliyekuzuia tunamjua na sababu tunazijua!, nakushauri this time, usikubali!, mkatalie na uchukue hatua zile dhamira yako inazokutuma, vinginevyo 2015, na wewe utajikuta unatafuta nchi ya kuhamia!.

RIP KAMANDA MPIGANAJI DAUDI MWANGOSI, DAMU YAKO HAIKUMWAGIKA BURE!, SOMEONE MUST PAY VERY DEARLY HAPA HAPA DUNIANI! KAMA NI NOMA NA IWE NOMA!, LIWALO NA LIWE!.

PASCO.

NB: Pasco wa JF ni mwanahabari wa kujitegemea aliyesomea fani ya sheria lakini anaendelea kuitumikia fani ya habari kutokana na mapenzi makubwa ya fani hii!. Kufuatia kifo cha Mwangosi kumgusa sana, sasa ameamua kumbe msaada mkubwa kwa Watanzania sio fani ya habari tena, anaanza taratibu za ku wind up, kuachana na ku fani ya habari, na kuelekeza majeshi kuitumikia rasmi fani ya sheria, to stand for the voiceless ambao can't affort to pay for an advocate!.

Wengine hili tuliliona kitambo tukalizungumzia, baada ya wabunge kulizungumza ndipo JK akalisikia!.
Pasco
 
Hivi hili nalo liliishiaga wapi? Au ndio hicho kiini macho cha kupeleka mtuhumiwa kwa mbwembwe mahakamani na waandishi nyie kuanzisha tuzo ya mwangosi baasi!? Manake kila mtu kahamia kwa zitto kabwe mbangubangu issue ya fidia kwa familia hii imefikia wapi?!
 
Please, Please,
Please, Stop This Police Brutality!.
Utampeleka JK The Hague-Part II!
baada ya kuona madhara waiyopata waandishi nimeonelea kupandisha uzi huu.
 
Wanabodi, tusiwalaumu sana vijana wa kamanda Sirro, as if tukio la kifo cha Akwilina ndio mwanzo!. Hawa hizi ndio zao!.

Polisi hawakuanza leo matukio kama haya, hivyo hapa ni katika kukumbushana tuu, mambo kama haya yaliishatokea huko nyuma, yametokea sasa, na yatatokea tena!. Tutakumbushana!.
P
 
Back
Top Bottom