IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Sep 4, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,561
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Mkuu IGP, Kamanda Saidi Mwema,

  Hebu Shuhudia!.

  [​IMG]

  Hii ndio picha ya mwisho ya mwanahabari, mpiganaji Daudi Mwangosi aliyefia kwenye uwanja wa mapambano!,

  1. Ukiangalia kwa makini, utashuhudia hapa, Daudi Mwangosi alikuwa amepigwa mpaka kuangushwa chini, askari hao 6 wenye uniform na mmoja plain clothes mwenye T-shirt ya blue na kofia nyeusi ameshika bastola kwa mkono wake wa kulia, walikuwa wanaendelea kumpigia nini ili hali hana silaha yoyote, haja resist arrest yoyote, why all this police brutality?.

  2. Ukimwangalia Mwangosi, amejishika kiunoni kwa huyo OCD mwenye kifimbo, licha ya kipigo alichokipata, kamwe hakuacha zana zake za kazi, mkuno wake wa kulia bado umeshika kamera yake na baada ya kifo, begi lake la laptop ndogo lilikuwa pembeni yake!. Hivi hawa polisi wote sita, wanamshambulia mtu mmoja tena mwenye camera inaonekana wazi, huku kamanda wao akijitahidi kuwazuia kwa kumkinga, lakini bado wakaona haitoshi ndipo unamuona askari huyo akimuelekezea kabisa mtutu wa bomu la machozi!, whay all this police brutality, why?!.

  3. Najua Mkuu Kamanda Mwema, inawezekana wewe hupati muda kupita humu JF kwa vile mtandao huu 'hauna jema la kuisifia serikali yako', na vile vile 'uko bize sana' na shughuli za ulinzi wa raia na mali zao (japo wengine kwa kuwaua kwa makusudi mazima), lakini naamini vijana wako wanapita humu na watakuletea hizi salamu zetu, tunakuomba sana sana sana, stop this police brutality, utakuja kumponza bure shemeji!.

  4. Tanzania tuna uchache sana wa wanasheria, na waliopo wengi hufanya kazi kwa wenye nazo, hivyo tangu huu mlolongo wa mauaji ya polisi, hakuna mwanasheria, shirika, wanaharakati, au chama chochote cha siasa kimelifikisha jeshi la polisi mahakamani, simply because wanaokufa wote ni watu hohehahe, familia zao hazina uwezo wa hata tuu wa kujua haki zao za kudai fidia rasmi serikalini, bali uwezo wa kuajiri mwanasheria kuwatetea mbele ya haki kwa kulishitaki jeshi la polisi!.

  5. System ilipoamua kumshuhulikia Imram Kombe kwa kutumia polisi wazembe, angalau familia ile ilikuwa na uwezo wa kuajiri wakili jeshi la polisi likashitakiwa na serikali ikalipa fidia ya kifuta machozi cha mamilioni, japo mlizuga kuwa askari wale walihukumiwa vifungo japo hawakuvitumia lakini familia ile angalau chochote kitu ilipata, milioni 300 kwa miaka hiyo, japo hailingani na uhai wa binadamu, lakini angalau ilikuwa sii haba!, hawa wengine wote, hawakuwa na wa kuwapigania lakini kwa Mwangosi, its a wrong button!.

  6. This time, tunataka kuwaona vijana wako behind bars, the soonest posible wakati uchunguzi ukiendelea, hata kama utawashitaki wewe kwa negligence, sisi bado tutakushitaki wewe kwa kesi ya madai, ili familia ya Mwangosi angalau ipate pa kushikilia!.

  7. Yote vijana wako waliyoyafanya, watu wamevumilia l;akini kwa hili la Daudi Mwangosi, uvumilivu umetufika mwisho maana ni kifo cha unyama wa ajabu kab isa kupata kushuhudiwa na binadamu alietendewa na binadamu mwingine kwa kisingizio cha line of duty!.

  8. Nimekupa angalizo, kama usipochukua hatua madhubuti zenye genuinity kama sura yako inavyoonyesha, unaweza kushindwa kuamini kuwa hata 2015 inaweza kuwa mbali, angalia sana usije kujikuta unamponza shemeji, wewe na yeye na wenzenu, mnaweza kujishtukia mko njia moja kuelekea the Hague bila kuamini!.

  9. Watanzania ni watu wapole, wavumilivu na wastahimilivu wa hali ya juu, lakini angalia usiwafikishe mahali, wakaishiwa upole, uvumilivu na usahilivu na kufikia kuamua liwalo na liwe, Hata Ghadafi alijua kuwa anapendwa hivi hivi anavyopendwa shemeji, hata Hosni Mubarak alijua anapendwa hivi hivi anavyopendwa shemeji, hata Wamisri nao walikuwa wapole, wastahimilivu na wavumilivu kama Watanzania, hata Walibya nao walikuwa vivyo hivyo, uvumilivu ulipofika mwisho, matokea sote tunayajua, yakitokea ya kutokea, usije kusema hatukukuonya kabla!.

  10. Mwisho kiukweli, to be honest, Kamanda Mwema kama lilivyo jina lalo, unaonekana wewe ni mwema genuinely kwa maneno na matendo, na naamini alishataka kuwachukulia hatua vijana wako siku nyingi, ila ulizuiwa na aliyekuzuia tunamjua na sababu tunazijua!, nakushauri this time, usikubali!, mkatalie na uchukue hatua zile dhamira yako inazokutuma, vinginevyo 2015, na wewe utajikuta unatafuta nchi ya kuhamia!.

  RIP KAMANDA MPIGANAJI DAUDI MWANGOSI, DAMU YAKO HAIKUMWAGIKA BURE!, SOMEONE MUST PAY VERY DEARLY HAPA HAPA DUNIANI! KAMA NI NOMA NA IWE NOMA!, LIWALO NA LIWE!.

  Paskali.

  NB: Pasco wa JF ni mwanahabari wa kujitegemea aliyesomea fani ya sheria lakini anaendelea kuitumikia fani ya habari kutokana na mapenzi makubwa ya fani hii!. Kufuatia kifo cha Mwangosi kumgusa sana, sasa ameamua kumbe msaada mkubwa kwa Watanzania sio fani ya habari tena, anaanza taratibu za ku wind up, kuachana na ku fani ya habari, na kuelekeza majeshi kuitumikia rasmi fani ya sheria, to stand for the voiceless ambao can't affort to pay for an advocate!.
   
 2. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  tupo pamoja somo
   
 3. L

  LIBRARY JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Maneno mengi hayavunji mfupa kaka Pasco, Mwaga strategies za kufuatwa Tuanzie wapi, wengine sisi ni Librarians Hatujui hata sheria moja.
   
 4. MERCIFUL

  MERCIFUL JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,471
  Likes Received: 746
  Trophy Points: 280
  Pasco - Well said my brother and Bravo for taking the lead....you have proven the saying "it begins with You"!! Asante kwa kutufafanulia hio picha kwa undani. Mimi binafsi nilijawa na uwoga na hasira zilizopelekea nishindwe kuona hata camera.. Hakika Mkono wa Mungu hautaiacha familia ya mpiganaji huyu itaabike!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu pasco,asante kwa kuonesha kujali kwa vitendo! Ninaamini likisimamiwa vizuri hili lililotokea, walau tutatengeneza mwanzo mzuri wa Tanzania tunayoitamani! Na damu ya mtanzania mwenzetu,kijana na mwanahabari haitapotea bure. Kila la kheri!
   
 6. T

  THEJEWDA Member

  #6
  Sep 4, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Bro. Pasco, huyo shemeji yake anapendwa na warembo wenzake.
   
 7. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Duu.... Ucambuzi umetulia... hivi kumbe mabomu ya machozi yapigwa kwa mtutu..?
   
 8. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #8
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana
   
 9. LENGIO

  LENGIO JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 1,032
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Kwa hali ilivyo kwa nchi hii kwa sasa inaitajika waziri wa mambo ya ndani mwenye akili timamu sio kama huyo bisho shoga.kutokana na umahiri wa wabunge wa cdm kwa kutetea wananchi hakuna anaeweza kutembea kwa miguu kokote watu wasiwafuate na inakuwa kama maandamo sasa wasitembe?
   
 10. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60

  Mkuu, upo sahihi. sio waziri tu, ni wote, Kikwete, Nchimbi, Mwema, Chagonja, Manumba na li ccm lote bovu. tuliondoeni madarakani li mfumo lote la utawala wa ccm.
  Tuendeleeni kuwaelimisha wananchi, waelimike ili waling'oe madarakan hili li serikali la ccm MAONGO/MAJAMBAZI/MAFISADI/WAUAJI.
   
 11. s

  sad JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wakiendelea kufanya hivyo tunawaondoa na wao
   
 12. s

  sad JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona tukiwaita kwenye matukio ya ujambazi munaogopa? hata mukija munakuja kwa kuchelewa.
   
 13. AMBANYONGE

  AMBANYONGE Member

  #13
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwakeli matukio yanayo endelea nchini yanatia uchungu sana ni wakati wa kuchukua hatua kwa vitendo na tuache kutoa matamko ya kulaani, kwani kesho au kesho kutwa kama sita uwawa mimi itakuwa zamu yako wewe!
   
 14. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mkuu Sad, watakujaje mapema wakati ndo issue zao. Yale wanayoyafanya nyuma ya pazia yameonekana sasa. Mungu hamfichi mnafiki.
   
 15. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Hivi watanzania mkisema mnauawa na wale wanaokaa Syria waseme nini. Watu wengine bwana.
   
 16. m

  maswitule JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,385
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Unaangalia idadi ndio unasema watu wanauwawa eti, siku atakapouwawa ndugu yako ndio utalijua hilo lisemwalo
   
 17. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mpaka mabomu na risasi ziishe....
   
 18. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Police Brutality haijaanza leo. Itafika wakati raia na polisi wataishi kama paka na panya na uswahilini wasikae. nakumbuka miaka ya 90 raia wa Afrika Kusini ilibidi waelimishwe maana ya kuwa na polisi ukizingatia wao walitoka ktk utawala wa kibaguzi.
   
 19. AMBANYONGE

  AMBANYONGE Member

  #19
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatuwezi kukulaumu kwani inavyo onekana umeasilika na matatizo ya kutofikiri kwa makini! kwani wewe unataka wafe wangapi ndo uone ni mauaji?
   
 20. o

  one army Member

  #20
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali hii imemwaga damu Arusha,Mwanza,Mara,Mbeya, Morogoro na Iringa sasa polisi mbwa wa serikali ya ccm watwambie WATANZANIA malengo ya haya mauaji na wanaisaidia ccm kwa malengo yepi ili tuweze kuwa na imani na hili jeshi kabla hatuja chukua sheria mikononi kama yaliyo tokea egpty, tunisia na libya
   
Loading...