Police Jamii na Sungusungu wanatumia vibaya kituo kidogo cha Police Lift-Valley, Kimara Stop Over

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Wakuu salamu.

Kuna kituo kidogo cha polisi kipo maeneo ya Kimara Stop over, mitaa ya Rift valley. Kituo hiki kimekuwa kama shamba la bibi kwa police jamii na sungusungu wa eneo lile. Kimekuwa kama ndio kijiwe chao cha kahawa.

Muda wote ukienda hapo utakuja wamejazana huko ndani, wanapanga njia za kwenda kusumbua raia kwa kudai hela za ulinzi shirikishi ambao hata hawalindi. Kituo kimekosa hadhi na heshima ya kuwa kituo cha police, watu wanachukuliwa na police jamii na kwenda kuwekwa cello.

Kwa mfano Jumapili iliyopita (21/01/2024l) wamweka ndani mama mmoja pamoja na mwanae mdogo eti kisa hajalipa hela ya ulinzi. Not fair. Huwezi kumfunga mama na katoto kake.

Tunaliomba jeshi la police la kanda husika lichukue hatua haraka sana, kituo kirejeshwe mikononi mwa jeshi la police na viongozi wa mtaa waonywe mara moja hii tabia ya kusumbua raia kuhusu hela za ulinzi wakati hakuna anayelinda na kila siku bado watu wanaibiwa.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom