IGP Mwema must go now!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema must go now!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 28, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  How long shall we wait for this guy to go? NI kweli wabunge wanaogopa kutaka aondolewe? watu wangapi wameteswa mikononi mwa polisi na kufa; ni mara ngapi tumelalamikia nguvu zinazotumiwa na polisi dhidi ya wanaharakati? Kwanini anaendelea kuwa IGP wakati jeshi lake limehusishwa na kashfa nyingi sana za uvunjaji wa haki za binadamu na zile za kiraia? Na mara ngapi tumeona jeshi hili likitumia "intelligensia" kuzuia maandamano ya kisiasa lakini ikikosa "intelligence" linapokuja suala la utekaji nyara?

  Waliomuua kijana yule wa Ubungo kule Igunga wamepatikana?
  Waliowapiga wabunge Kirumba wamepatikana?
  Tarime?
  Arusha?
  Songea?

  Bado we don't see this pattern of gross incompetence ya Said Mwema na uongozi wa Jeshi la Polisi? Shemeji yaRais? so what? Ushemeji wao unalihusu nini taifa. Said Mwema must go NOW!!! We have had enough of this level of mediocrity!
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Ngauti ya Rais itandoka na Rais MMMJ
   
 3. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,078
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Du ama kweli mzee wa D**t huwaachii mwaka huu
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa! Tuache wachaga tuitwe wachaga mkuu....siku hizi mambo ili yaende inategemea unamjua nani
   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,538
  Likes Received: 10,460
  Trophy Points: 280
  Said Mwema ni kama mwanasiasa. anaamini ni upepo utapita tu.!!
   
 6. kiagata

  kiagata Senior Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kila mtu atawajibishwa kwa makosa yake mwenyewe,acha amalize muda wake aende.Amejitahidi sana katika sera ya polisi jamii na maboresha katika Jeshi la polisi.Uelewa wake ni mkubwa kuliko afande Nguguli.Kwasasa kuna unafuu wa dhamana na kujua haki yako kabla na baada ya kukamtwa na kosa linalokukabili.BIG UP MWEMA
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Upepo?? Duuuh!! vimbunga vingine vinaanzaga hivi hivi mjue . . .
   
 8. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  kwa mujibu wa sheria anatakiwa astaafu mwaka huu.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  A series of incompetence kwenye handling ya mambo nyeti mpaka tunaogopa!
   
 10. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ushemeji! nani kachukuliwa dada?
  JK anafagilia sana nepotism. Matokeo yake ni kushindwa kuwawajibisha hata wakifanya madudu kiasi gani.
  Mambo yakimzidi sana ataomba mwongozo kutoka NEC kama alivyofanya kwa akina Ngelejaaa na wenzake. Maamuzi mazito hawezi handsome boy.
   
 11. p

  politiki JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwako MM,
  It is a structural problem i don't know why can't you see that. removing individual without doing structural changes can not solve the problem. as long as the individual will be accountable to the president expect no changes will be realized.
   
 12. j

  jigoku JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni mfumo,suluhu hapa Mzee Mwanakijiji ni kubadilisha mfumo mzima,na hapa ni kuing'oa Nyinyiemu maana hiyo ndio kansa.
   
 13. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Na kuna tetesi kua hua akiona hajaonekana kwenye Tv na vyombo vya habari hua anachukua Silaha na kuita wanahabari kua Zimekamatwa mikononi mwa majambazi na wanawashikilia baadhi yao. Kwa haraka nilibisha kabisa ila hivi karibuni aliibuka na styl yake kama kawa. Nilimtazama na kua na ualakini katika presentation yake, kivipi?

  Kwanza hua anazifumbata silaha kana kwamba hazihitaji uchunguzi zaidi mahakamani, hapa namaanisha "Fingure prints" kwani hua hana special gloves hivyo kufuta ushahidi au kujipa jukumu la kua yeye ndie jambazi kuweka Prints zake pale kwenye silaha.

  Pili matukio yote hua amejipanga kwa kua huongelea sehemu iliyotayarishwa kana kwamba anakuja hutubia waandishi wa habari hadi nembo ya Jeshi la polisi inakuepo.

  Tatu katika matukio yote anayoita waandishi wa habari hakuna picha iliyowahi pigwa wala kuonyeshwa kwa vyombo vya habari zaidi ya maelezo yake na kukumbatio silaha za watuhumiwa wa miaka ya 1994 ambao wako jela tayari. Au ulishawahi kumuona katika eneo la tulio akitoa habari zake LIVE? Nikumbushe labda nimesahau.

  KOVA/ MWEMA ni ceremonial figure tu pale hana chochote zaidi ya hayo niliyoweza kudadavua.........
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mnyika alikuwa sahihi kabisa kusema kuwa tumefika hapa kwa sababu ya 'uzembe wa bunge na upuuzi wa CCM'. Bunge na hawa wabunge wa CCM wangekuwa wanawajali watanzania wangeshapitisha azimio la kubadili uongozi wa polisi. Mauaji ya raia yanatisha! Siku hadi siku raia wanauliwa katika mazingira ya kutatanisha, kwa nini IGP asiwajibike? Hivi kweli wabunge wa CCM hawaguswi na mauaji yanayoendelea nchini? Haoni hofu iliyotanda kwa wananchi kila kona nchi hii?

  Pili, kwa taifa lolote ni hatari sana inapofikia hatua kwamba wananchi wakipatwa na tatizo hata la ki-usalama mahali pa kwanza pa kukimbilia ni 'wanaharakati wa haki za binadamu'! Huu ni msiba wa kitaifa na ni mzigo wa CCM, kwamba raia anavamiwa lakini anakimbilia kwa wanaharakati na sio polisi! Watanzania hawana imani na serikali na vyombo vyake! How can we say tuna serikali? How can we say tuna Jeshi la polisi?

  Niseme hivi, ikifika saa 12 leo jioni bila Jeshi la polisi kukamata watu waliohusika na unyama wa Dr Ulimboka, basi wananchi wanayohaki ya kuamini serikali ya CCM ndio mhusika mkuu. Kwa bahati, Jeshi hili hili la polisi walishaonesha kuwa na 'inteligensia' ya hali juu, hivyo haiwezekani yapite masaa 24 bila kujua wahusika wa unyama uliofanyika mbele ya nyuso zao. Mbona wameweza kuwapata wahalifu huko mbugani? Au kwa sababu ni mzungu?

  Tujipe muda hadi saa 12 jioni ili tujue moja, kama serikali ya CCM ina nia ya kulinda usalama wa raia au wako kuwaangamiza.
   
 15. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,508
  Likes Received: 5,626
  Trophy Points: 280
  Mkuu MM, Hii nchi ni kama tumelogwa! Viongozi wa CCM wanatoa kauli za ajabu ajabu kipindi kigumu kama hiki.wanafanya mizaha na muelekeo wa nchi.Vyombo vya usalama vyote vinasubiri nchi ivamiwe na akina Idd Amin ndio watulinde!

  Hatuna viongozi wanaoheshimika wanaoweza kushinikiza bila woga haki kutendeka,hakuna waliotayari kuyaweka rehani maisha yao kwa ajili ya Tanzania ya kesho.

  Nasikitika hata wapinzani ule moto wa kususa,kushinikiza ndani na nje ya bunge umepoa ajabu,wakiambiwa kaa chini wanatii alafu wanalalamikia pembeni! Nani atasimama kupaza sauti watawala wakajua la mgambo limelia? Nani ataongea na wananchi wakamwelewa vizuri bila kugawanyika sana?

  Nakosa majibu ya muelekeo wa Taifa hili.Nyerere alikufa na Tanzania yake tumebaki na photocopy!
   
 16. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  This is our fight! Sisi Watanzania imefikia muda tuache kusubiri mtu kutupigania tunachohitaji ni a unifying voice. Ninaamini nobody is responsible for the well being of my family, my friends and most important my COUNTRY ni mimi mwenyewe ndio nitapigania kama ni kupaza sauti, tunatakiwa kupaza as highest as possible, kama ni kuandamana, tuandamane mpaka! Pale tutapoanza kusimamia maslahi yetu bila kuongozwa na hisia za kisiasa hawatapata pa kutokea.

  We have to chase these crazy baldheads out of town ASAP maana kishanuka!
   
 17. cement

  cement JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sure i agree with you
   
 18. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  You Have Point Mkuu, Umenena vema
   
 19. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi sisi kama wananchi tuna haki gani katika kumshinikiza mteule wa Rais ajiuzulu? Au ndo mapungufu ya katiba tunayoyazungumzia? Maana naona utaratibu wa kujiuzulu kwa makosa ya uwajibikaji ni msamiati mgumu sana hapa kwenye nchi yetu. Na pengine ni kwa kuwa hawa wateule wanajua hatuwezi kufanya kitu, na tutaishia kupiga kelele tu!
   
 20. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mkuu tuanze kwa kujaribu kutoa maoni yetu kwenye mjadala wa katiba mpya.. Kwa kutoa mawazo yetu katika kupata katiba mpya ambayo kwanza itabadilisha mfumo mzima wa uongozi tulio nao..
   
Loading...