Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,836
- 730,300
Kwenye sakata la askari aliyedai kutukanwa na mke wa waziri Mahiga, Magufuli aliuagiza uongozi wa jeshi kumpandisha cheo mara moja askari huyo kama morali kwa wengine
Lakini IGP Mangu amekosoa kiaina uamuzi huo kwa kusema kwamba hana taarifa rasmi lakini hata hivyo atakapozipata itabidi askari mhusika aende mafunzoni kwanza
Hapa maana yake ni kwamba huko mafunzoni akifeli asahau kupanda cheo cha matusi! Mangu amesimamia taratibu na kanuni hii itampa heshima kubwa...nimejaribu kujiuliza ingekuwa ni Makonda Magesa na wengine wangeweza kufanya hivi kweli? Jibu ni hapana kwakuwa wamepewa vyeo kama zawadi, Mangu ni professional na kaitendea haki profession yake