frolian mwebesa Jr
Member
- Aug 27, 2014
- 26
- 0
Ukweli kuhusu kilichotoke Ifunda tech!!! Kwanza c uzembe Wa viongozi Wa wanafunzi !! Kwan wao ndio walikua wasuluhishi wakuu Wa tatizo hilo!! Baada ya kutokea tatizo la adhabu zilizopita kiasi na kutokusikilizwa kwa viongozi Wa wanafunzi !!! Wanafunzi waliamua kushinikiza vingozi wote kuvua tai za uongozi ili nao wawe kama wanafunzi wengine!!! Tatizo likaanzia hapo ; lakini viongozi wa shule walifanya juu chini kulisuluhisha kwan waliomba kikao na waalimu wanaohusika na ushauri(counceling)!!! Wakiwa na form6 kama wawakilishi wa wenzao na kweli walifikia muafaka wa matatizo ya wanafunzi lakini tatizo la viongoz liliwekwa kando(pending)!!! Lakini usiku Wa siku hiyo(j4-j5) watu wasiofahamika walikata fensi ya wavu ya Shule iliyokua inatumika kukamatia wachelewaji!! Hawakuishia halo tuu Bali waliiba kengele ya Shule na kuchoma kitalu cha miche!! Baada ya waalimu kuona tatizo limefikia hapo ndipo wakafungua macho na kuanza kutafuta suluhu!!! Wakaiita serikali ya iliyopinduliwa (wanafunzi) na kuwataka wakaongee na wanafunzi wenzao kwa kuwaahidi kuwatatilia kero zao zote( viongozi) ;viongozi Wanafunzi walifanya hivyo na wanafunzi wakakubali!! Na kuitikia wito Wa waalimu (j5 majira ya SAA 12:30 jioni) Lakini kwenye kikao hicho ilionyesha dhahiri kwamba wanafunzi hawakuridhishwa na majibu ya waalimu na walihisi wamekula njama na viongozi Wa wanafunzi, na kwakua Giza lilikua limeanza kuingia walianza kurusha mawe mabatini!!! Waalimu kuona hivyo walikimbia (magari) na kuicha Shule katika hali tete na zaidi ya hapo hawakufanya juhudi zozote za kulinda amani ( kuita jeshi la polisi) kwani polisi walifika baadae sana baada ya maafa makubwa kufanyika!!!! Ilihali jeshi hilo lipo karibu sana na Shule(250m) toka shuleni