Ifahamu Soju kutokea South Korea

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
522
1,000
Kama umeona series kama ITAEWON CLASS, MASK, K2 na HEALER basi kwa mbaaali utakuwa ushaanza kuhisi uzi huu unahusu nini.

Yes! Ni Soju kinywaji chenye alcohol level ya 16.8% mpaka 53. 8% na chupa moj inauzwa kama Tshs 6000 hivi huko Korea.

Kinywaji hiki maarufu sana nchini South Korea kinatengenezwa na mchele, ngano na shayiri japo siku hizi wanatumia sana Starch kutoka kwenye viazi vitamu.

Kun link hapa inaonesha jinsi ya kutengeneza Soju


Kwa mwaka 2004 pekee zilliuzwa chupa takriban 3B za soju na kulingana na tafitu zilizofanywa mwaka 2006 ni kuwa kwa mwaka mtu mmoja anakunywa chupa 90 za SOJU juko South Korea. Ni nyingi right?

Zishukuriwe sana Korean Dramas kutokana na kuwa maarufu sana mwaka 2008 Kamusi ya Mariam Webster iliingiza ko neno Soju kama msamiati huku miaka nane baadaye yaani 2016 OXFORD DICTIONARY pia iliingiza neno soju kama msamiati.

KWANI SOJU ILIANZIA WAPI?
Well, Sojy imeanza miaka mingi sana tangu 13th Century kipindi cha Goryeo na hii ni baada ya Mongols kuvamia Goryeo hivyo kuanza kutumia kinywaji hiki kwa wingi na mpaka leo ni namna ya utengenezaji tu unabadilika lakini Soju imebaki kuwa Soju.

SHERIA ZA UNYWAJI
Sasa Soju sio Safari Lager ina namna yake ya unywaji na Korean dramas zimefanya kazi kubwa sana kuelimisha dunia juu ya sheria hizo.

Kwanza kabisa siku zote mtu mdogo ndio anammiminia kinywaji mtu mzima, na udogo sio umri hata cheo pia ukiwa na cheo kidogo kazini ni lazima ummiminie soju meneja au mkuu wako wa kazi.

Tena sio kummiminia tu unafanya hivo kwa mikono miwili ili kuonesha heshima na mpokeaji nae inabidi atumie mikono miwili kupokea.

NANI ANATENGENEZA?
Jinra ndiye mtengenezaji mkubwa wa kinywaji hicho nchini South Korea, kwa mwaka 2013 kampuni hiyo iliuza Chupa takribani 750B.

Ukiachana na Jinra pia Soju inatofautiana kulingana na sehemu uliyopo. Kwa mfano pale Busan wenyewe wana aina yao ya Soju iitwayo C1 wakati Daegu aina ya soju inayonyweka sana ni Cham.

Namalizia kwa kuuliza hivi Bongo tuna kinywaji ambacho tunaweza tukasema ni cha kwetu? Au ni Togwa na Gongo?

Uzi Tayari!
poster%2C504x498%2Cf8f8f8-pad%2C600x600%2Cf8f8f8.u3.jpg
flavoured-soju-series-12-pack.jpg
chamisul-soju_shadow.jpg
 

sychellis

Member
Oct 16, 2018
72
125
mkuu inaonekana unapenda tamaduni au mambo yanayohusu korea. Vp lugha yao unaipata vizuri? mi naitaji kujua iyo lugha
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,203
2,000
Chibuku ilikuwa kinywaji cha kitanzania sijui imeishia wapi pia tuna vinywaji vya makabila kama mbege, rubisi, wanzuki na ulanzi
 

Tlg

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
790
1,000
korean language is very easy to learn binafsi nimejifunza mwenyewe through youtube courses, now i can read and write and understand a few words. by the end of this year i think i will be competent enough to start conversing with ppo
mkuu inaonekana unapenda tamaduni au mambo yanayohusu korea. Vp lugha yao unaipata vizuri? mi naitaji kujua iyo lugha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom