Ifahamu sheria ya Haki Miliki iliyotungwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya Wasanii

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1620899122628.png

Hapa nchini, mara baada ya sheria ya hakimiliki ya mwaka 1966 kuthibitika kwamba ina upungufu mwaka 1999, Bunge lilitunga sheria mpya ya hakimiliki na hakishiriki, namba 7 ya mwaka 1999.

Sheria hiyo imeletwa kulinda kazi za wasaniii zinazolindwa na haki miliki na hakishiriki na nyingine zote zinazoendana na hizo.

Kwa mujibu wa kifungu cha 2(iii) madhumuni ya kutungwa kwa sheria hii ni kuhakikisha maendeleo ya wasanii, watunzi na wabunifu katika nyanja za nyimbo, maigizo na tasnia nyingine za kisanii.

Sheria hii ina madhumuni ya kuinua kazi za fasihi na za kisanii pamoja na nyingine zinazofanana na hizo.

Kwa mujibu wa sheria hii, kuna makundi makubwa mawili ya haki za wasanii zinazolindwa na sheria hii, ambazo ni haki ya kiuchumi na haki za kitamaduni ambazo mtunzi wa kazi zinazolindwa na sheria hii ana haki nazo.

Kwa mujibu wa kifungu cha 3(i) inatoa angalizo kuwa, kazi zinazolindwa na sheria ni lazima ziwe zimetengenezwa na mtunzi Mtanzania au zile ambazo mtunzi wake si Mtanzania lakini ana makazi ya kudumu hapa nchini au kazi hizo zilizotengenezwa kwa mara ya kwanza hapa Tanzania, au ambazo ni za kusikika na kuona (audio-visual) ambazo mtayarishaji wake ni Mtanzania au makao makuu yake ya kutengeneza kazi hizo zipo hapa nchini.

Na kwa mujibu wa kifungu cha 3(3) wasanii wanaomiliki kazi za kisanii wana hakishiriki pia watapewa ulinzi na sheria hii. Katika kifungu cha 4, msanii ametafsiriwa kama mwigizaji, mwimbaji, mwanamuziki, mchezaji, au mtu anayeigiza, kuchonga au kufanya maonyesho jukwaani.

Sharti la kazi za kisanii kulindwa na kigezo hiki ni iwe katika hali ya kushikika na kwamba mawazo hayatalindwa .

Kwa mfano, kama A na B walio katika sehemu tofauti wana wazo linalofanana la kutengeneza wimbo unaohusu foleni za magari, na A akawa wa kwanza kuimba wimbo na kuurekodi B hawezi kumshitaki A kwa kumuiba wimbo, kwani alikuwa na wazo na wakati mwenzake ana video.

Kifungu hiki kinaendana na maamuzi ya Mahakama ya Uingereza katika shauri la University of London Press Ltd dhidi ya University Tutorial Press, (1916) 2 Ch.601 ambayo ilitafsiri maana ya kazi ya kisanii kumaanisha yaliyomo katika kifungu cha 5 cha sheria ya hakimiliki na hakishiriki ya Tanzania.

Kwa upande mwingine, imetaja baadhi ya kazi ambazo haziwezi kulindwa na sheria yenyewe ikiwa ni pamoja na habari zinazochapishwa au kutangazwa katika vyombo vya habari, sheria na maamuzi ya vyombo vya kutoa maamuzi kama mahakama na mabaraza, na pia wazo la aina yeyote ambalo halijawekwa katika hali ya kushikika na kudumu.

Haki ya kiuchumi katika sheria ya Tanzania, inapatikana chini ya kifungu cha 9, ambayo ni mtunzi wa kazi inayolindwa na sheria hii amepewa haki zote juu ya kazi yake, katika masuala yote yanayohusiana na kutafsiri kazi yake, kuikodisha, kuionyesha umma, kupitia vyombo vya habari, kuisambaza au kuitumia hadharani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom