Ifahamu Nchi ya Scotland (United Kingdom)

Adabwash

Member
Feb 11, 2019
69
157
Kwanza kabisa I declare interest ya member Parabora ambaye alituletea uzi wa Uswiz ambapo tumejifundisha mambo mengi, nami nimeona ni Bora kuwafahamisha watanzania wenzangu kuhusu Nchi ninayoishi,

Scotland ni Nchi ndani ya United Kingdom ingawaje si Nchi katika mipaka ya kimataifa,hii naifananisha kabisa na jinsi ilivyo Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Tanzania,

Mji mkuu wa Scotland unaitwa Edinburgh na ndiko lilipo Bunge la Scotland,Pia ndani ya Scotland kuna jiji la Biashara linaloitwa GLASGOW, mfanano wa Majiji haya mawili kimuundo wa kinchi yalivyo ni Sawa Kabisa na Dar es salaam na Dodoma,

UKARIMU
Watu wengi wa Glasgow ninapoishi ni wakarimu Sana,very welcoming people Kwa wageni,na pia Kwa ufahamu wangu kutokana na muda nilioishi hapa,sijakutana na matukio mengi ya ubaguzi,nadhani hili limechangiwa Sana na Sheria Yao waliyojiwekea ya Hate Crime,na Racism,

USALAMA,
Glasgow ina watu watukutu na wahuni Kiasi,Ila matukio ya kushambuliwa Kwa watu hutokana na Visasi vya magang ya kihuni,Ikiwa wewe ni MTU wa Kuishi life lako la kazini na nyumbani au na jamii yako,utaishi mpka unazeeka hutokumbana na mabalaa,labda itokee Bahati yako mbaya

LUGHA
Kama ilivyo Uingereza yote lugha Yao mama ni kiingereza lakini ni tofauti kidogo na Scotland ambapo wanatumia kiingereza na miji ambayo IPO Scotland ya mbali wanatumia lugha ya GAELIC,ni kawaida kabisa kumkuta mscottish ambaye hajui kiingereza, kiingereza wanachozumza wascottish kina accent tofauti na kiingereza kunachozungumzwa london,Nikawaida kabisa kutokuambulia anachozungumza mscottish hata kama wewe ni bingwa WA lugha ya kiingereza,halafu wanaongea Kwa haraka sana Kiasi cha kukuchanganya kabisa Akili,

WANAWAKE
Wanawake wakiscottish hawanaga time na MTU ingawaje wengi wao wanastress na kuwa masingle,sehemu pekee ambapo wahamiaji wanawapa totoz za kiscotish nikwenye vilabu vya starehe,Kwa wale watu watu wa Tungi kama Pierre liquid watabahatika pia kuwagegeda wascottish,

HALI YA HEWA,
Tunaweza kusema yakuwa Scotland ndo sehemu yenye baridi zaidi ndani ya UK,katika mji ninaoishi wa Glasgow, Mtu nayetaka Kuishi katika mji huu lazma ajipange na suala zima la baridi Kali,

UTOFAUTI WA USIKU NA MCHANA,
Kwa wale mliozoea Giza linaingia saa kumi na mbili na Dar za jioni na jua kuchomoza saa kumi na mbili Asubuhi Dar, hapa Scotland ni tofauti kabisa, wakati wa majira ya Winter jua huchomoza saa tatu Asubuhi na huzama saa nane mchana, Maana yake ikifika saa Tisa mchana kunakuwa na Giza totoro kama usiku wa manane wa dar.

Katika kipindi cha Summer jua huchomoza saa nane usiku na pia huzama saa nne za usiku,hapa Kwa wale waislam na mfungo wa Ramadh huwa wanaipata pata cha Moto Ramadhan ikiangua kipindi hiki,

UHAMIAJI NA UWEPO WA WATANZANIA NA WANAOZUNGUMZA KISWAHILI,
Nafahamu hii ndio sehemu inayongaliwa zaidi na watu walio wengi wabongo wenzangu,Jamii kubwa ya watanzania wanaishi hapa ni Wazanzibar ikifuatiwa na watanga halafu ndo wakina Sisi wabongo,jamii nyengine ya Waswahili ni watu wa Mombasa pamoja na wakenya wengine.

Njia Kuu wanazitumia watu wa Mwambao kuingia Nchi hii ni kujiripua kisomali,wanachukua viza za Shenghen wanaingia mpka ulaya ikisha wanafanya mafekeche ya Kuingia hapa nakujiripua kisomali,
Ingawaje MTU akitaka kuja kujiripua anaweza kutumia njia nyengine pia kufanya hivyo,ikiwemo kuingia na viza ya kiingereza halafu unajiripua utakavyoona inafaa, Serikali hapa haimrudishi MTU nyumbani kwao maadam ameomba hifadhi ya ukimbizi mpaka wasikilize kesi yake, minimum mpka kesi inaskilizwa ni miezi sita,

KAZI,
Nchi hii ni illegal kufanya kazi ikiwa huna makaratasi,ingawaje KAZI nyeusi zipo Ila ujira mchache,kama mnavyojua tena uwepo wa wahindi husaidia Sana watu wasio na makaratasi kufanya kazi,hii inapelekea hata ukiiomba hifadhi ya ukimbizi na kama unao watu wa kukuchanganya basi baada ya miezi mitatu gharama yako uliyokuja nayo hapa itakuwa imerejea,

UHAMIAJI MZURI,
Kuna Aina ya fursa Kwa watu wanaotaka kufanya KAZI katika Nchi hii,kuna fani ambazo ni Shortage ya skilled labor hapa,ikiwemo Kada zote za Afya ambao wanachukuliwa Sana kabisa,unaweza ukaingia katika website Yao na ukaomba na ukapata,fani zengine ambazo wanachukuliwa Sana watu ni Ma engineer,

Mwisho nipende kuwashukuru wote,Najua sijazungumzia yoote Ila kama kuna anayejua zaidi tafadhali Naomba aongezee ili wengine wapate kufaidika,

Na Kwa wale wakosoaji nawashkuru in Advance Maana Najua watakuwepo tu watakaonishambulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
images (4).jpeg
images (5).jpeg
images (6).jpeg
 
Utupe story kidogo za huko.Tunaambiwa huko wanaishi madon tupu tunataka kujua uingiaji wake na sehemu za kula bata kwa uhalisia...
Sio madoni tu kaka😃😃 ni nchi ya kiislam ile ni Kama kisiwa Wana watu wacache na rasimali nyingi ya mafuta hakuna mtu analipa kodi na mishahara wanalipwa mikubwa mno
 
Sio madoni tu kaka😃😃 ni nchi ya kiislam ile ni Kama kisiwa Wana watu wacache na rasimali nyingi ya mafuta hakuna mtu analipa kodi na mishahara wanalipwa mikubwa mno
Ok ok kwa hivyo kwa kwenda kutembea kula bata hapafai?
 
Kuna siku moja mtu mmoja aliwahi kua anaandika kitu kwenye simu akiwa mbele yangu,japo si vzr kutazama mambo ya mtu lakini niliona anajinasibisha kua yuko Kigari Rwanda na tulikua nae jijini Mwanza,nikakumbuka tu jinsi wabongo tulivyo

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Back
Top Bottom