Ifahamu Nchi ya Scotland (United Kingdom)

Ifahamu Nchi ya Scotland (United Kingdom)

Nikweli tupu ulichosema,Ila ndo maisha,ni changamoto Sana,nakumbuka mwaka wa Kwanza ndo Naingia Glasgow,Maana Mimi nikishukia London nikakakaa wiki halafu ndo nikaja Glasgow,basi Ile mwanzo nimefika,nilikuwa navaaa likoti likubwa Hilo mpka nikawa nahisi kabisa wazungu wananishangaa kimya kimya kwenye Dala Dala,

Nakumbuka Hilo likoti nililinunua KARUME DAR enzi hizo siku chache kabla sijapanda mwewe,

Baada ya miezi sita kuzoea na kujua mji kidogo nilienda litupa lile likoti katika vile vibanda vya kukusanyia nguo za charity,

Sasa hivi nimezoea Sana baada ya miaka mingi Kuishi hapa,idadi ya nguo nnazovaa ni tofauti na Mwanzoni,

Ila kipindi cha jua kuchelewa kuzama na kuwahi kuzamuka kama kipindi hiki,kwangu huwa kinaniletea shida Sana na sijawahi kuzoea kabisa pamoja na Kuishi Sana hapa
Baridi kali na mwenendo wa jua usioeleweka unafanya hata kufurahia maisha iwe mtihani, muda wote umejifunika na manguo mazito mazito au upo kitandani ndani ya blanketi na heater juu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye sredi za namna hii huwa naona kama sisi wazee wa H kunani "tunatengwa" samahani mkuu vipi sisi wazee wa lugha fursa zipo huko?
 
Sana as an interpreter tena ni miongoni mwa fani ambayo ina uhaba,
Masharti lazma ujue lugha zaidi ya mbili Kwa ufasaha kabisa one of which ni kimombo,

Ila pia kuna mitihani ya interpreter lazma uifanye ukiwa hapa au minimum college diploma ya interpreting,

Na Mkuu interpreter Wana hela Ndefu halafu wako bize kama magufuli,

Manake utahutajika council,mahakamani,hospital,serikalini katika charities mbali mbali,mashuleni yaaan kila sehemu mkuu,kama unaqualification nakuinspire Mzee.
Kwenye sredi za namna hii huwa naona kama sisi wazee wa H kunani "tunatengwa" samahani mkuu vipi sisi wazee wa lugha fursa zipo huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kazi kama za kuokota chupa za maji huko zipo?Kama zipo na watu wanaona noma kuzifanya tuunganishie sisi tuje tuungurume na majalala ya ulaya.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Scotland mchezo maarufu ni kandanda,kuna timu mbili watani wa jadi kama Simba na yanga,nazo ni Celtic na Rangers ambayo inafundishwa na Steven Gerrard,

Tamaduni hawa watu wanapiga Sana Ngoma zao za Asili zile zikiongozwa na matarumbeta ya maaana Sana,

Usishangae sehemu za mji na barabara kufungwa kwasababu ya parade ya hizo Ngoma zao,
Mavazi wanayovaa humo ni Scottish vazi la taifa ambalo ni sketi kubwa Kwa wanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante Mkuu
 
Jamani Kwa kuongezea Tu,sekta ya upishi huku ina uhaba WA watu,hata MTU ukiwa ni mpishi wa vyakula vya kiafrika basi unapewa visa vizuri tu kama sijakosea,
Wahindi wao wamejazana huku Kwa kutumia mwanya huu,utamkuta muhindi mmoja ana katestaurant uchwara halafu anawaleta wahindi wenzie wengi kama wataalam labda wa kupika tandoori kumbe wanakuja kuosha vyombo,
Tukipata fursa hizi pia tuzitumie ndugu zanguni
Shida ya hao watu wakifika sehemu wakiwa wengi wanaanza kuwa wabaguzi
 
Kwanza kabisa I declare interest ya member Parabora ambaye alituletea uzi wa Uswiz ambapo tumejifundisha mambo mengi, nami nimeona ni Bora kuwafahamisha watanzania wenzangu kuhusu Nchi ninayoishi,

Scotland ni Nchi ndani ya United Kingdom ingawaje si Nchi katika mipaka ya kimataifa,hii naifananisha kabisa na jinsi ilivyo Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Tanzania,

Mji mkuu wa Scotland unaitwa Edinburgh na ndiko lilipo Bunge la Scotland,Pia ndani ya Scotland kuna jiji la Biashara linaloitwa GLASGOW, mfanano wa Majiji haya mawili kimuundo wa kinchi yalivyo ni Sawa Kabisa na Dar es salaam na Dodoma,

UKARIMU
Watu wengi wa Glasgow ninapoishi ni wakarimu Sana,very welcoming people Kwa wageni,na pia Kwa ufahamu wangu kutokana na muda nilioishi hapa,sijakutana na matukio mengi ya ubaguzi,nadhani hili limechangiwa Sana na Sheria Yao waliyojiwekea ya Hate Crime,na Racism,

USALAMA,
Glasgow ina watu watukutu na wahuni Kiasi,Ila matukio ya kushambuliwa Kwa watu hutokana na Visasi vya magang ya kihuni,Ikiwa wewe ni MTU wa Kuishi life lako la kazini na nyumbani au na jamii yako,utaishi mpka unazeeka hutokumbana na mabalaa,labda itokee Bahati yako mbaya

LUGHA
Kama ilivyo Uingereza yote lugha Yao mama ni kiingereza lakini ni tofauti kidogo na Scotland ambapo wanatumia kiingereza na miji ambayo IPO Scotland ya mbali wanatumia lugha ya GAELIC,ni kawaida kabisa kumkuta mscottish ambaye hajui kiingereza, kiingereza wanachozumza wascottish kina accent tofauti na kiingereza kunachozungumzwa london,Nikawaida kabisa kutokuambulia anachozungumza mscottish hata kama wewe ni bingwa WA lugha ya kiingereza,halafu wanaongea Kwa haraka sana Kiasi cha kukuchanganya kabisa Akili,

WANAWAKE
Wanawake wakiscottish hawanaga time na MTU ingawaje wengi wao wanastress na kuwa masingle,sehemu pekee ambapo wahamiaji wanawapa totoz za kiscotish nikwenye vilabu vya starehe,Kwa wale watu watu wa Tungi kama Pierre liquid watabahatika pia kuwagegeda wascottish,

HALI YA HEWA,
Tunaweza kusema yakuwa Scotland ndo sehemu yenye baridi zaidi ndani ya UK,katika mji ninaoishi wa Glasgow, Mtu nayetaka Kuishi katika mji huu lazma ajipange na suala zima la baridi Kali,

UTOFAUTI WA USIKU NA MCHANA,
Kwa wale mliozoea Giza linaingia saa kumi na mbili na Dar za jioni na jua kuchomoza saa kumi na mbili Asubuhi Dar, hapa Scotland ni tofauti kabisa, wakati wa majira ya Winter jua huchomoza saa tatu Asubuhi na huzama saa nane mchana, Maana yake ikifika saa Tisa mchana kunakuwa na Giza totoro kama usiku wa manane wa dar.

Katika kipindi cha Summer jua huchomoza saa nane usiku na pia huzama saa nne za usiku,hapa Kwa wale waislam na mfungo wa Ramadh huwa wanaipata pata cha Moto Ramadhan ikiangua kipindi hiki,

UHAMIAJI NA UWEPO WA WATANZANIA NA WANAOZUNGUMZA KISWAHILI,
Nafahamu hii ndio sehemu inayongaliwa zaidi na watu walio wengi wabongo wenzangu,Jamii kubwa ya watanzania wanaishi hapa ni Wazanzibar ikifuatiwa na watanga halafu ndo wakina Sisi wabongo,jamii nyengine ya Waswahili ni watu wa Mombasa pamoja na wakenya wengine.

Njia Kuu wanazitumia watu wa Mwambao kuingia Nchi hii ni kujiripua kisomali,wanachukua viza za Shenghen wanaingia mpka ulaya ikisha wanafanya mafekeche ya Kuingia hapa nakujiripua kisomali,
Ingawaje MTU akitaka kuja kujiripua anaweza kutumia njia nyengine pia kufanya hivyo,ikiwemo kuingia na viza ya kiingereza halafu unajiripua utakavyoona inafaa, Serikali hapa haimrudishi MTU nyumbani kwao maadam ameomba hifadhi ya ukimbizi mpaka wasikilize kesi yake, minimum mpka kesi inaskilizwa ni miezi sita,

KAZI,
Nchi hii ni illegal kufanya kazi ikiwa huna makaratasi,ingawaje KAZI nyeusi zipo Ila ujira mchache,kama mnavyojua tena uwepo wa wahindi husaidia Sana watu wasio na makaratasi kufanya kazi,hii inapelekea hata ukiiomba hifadhi ya ukimbizi na kama unao watu wa kukuchanganya basi baada ya miezi mitatu gharama yako uliyokuja nayo hapa itakuwa imerejea,

UHAMIAJI MZURI,
Kuna Aina ya fursa Kwa watu wanaotaka kufanya KAZI katika Nchi hii,kuna fani ambazo ni Shortage ya skilled labor hapa,ikiwemo Kada zote za Afya ambao wanachukuliwa Sana kabisa,unaweza ukaingia katika website Yao na ukaomba na ukapata,fani zengine ambazo wanachukuliwa Sana watu ni Ma engineer,

Mwisho nipende kuwashukuru wote,Najua sijazungumzia yoote Ila kama kuna anayejua zaidi tafadhali Naomba aongezee ili wengine wapate kufaidika,

Na Kwa wale wakosoaji nawashkuru in Advance Maana Najua watakuwepo tu watakaonishambulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Scotland na Scandinavia countries ni nchi nzuri sana ila zinaboa na ngumu sana kujenga utajiri kwa sababu ya uwepo wa Kodi nyingi
 
Scotland na Scandinavia countries ni nchi nzuri sana ila zinaboa na ngumu sana kujenga utajiri kwa sababu ya uwepo wa Kodi nyingi
Bila ya kodi hakuna ustawi wa nchi,lazma kodi ziwepo ili mambo yasonge,Nchi hizi pamoja mambo mengine yanayosemwa na yasiyosemwa ila zilikamuana na wananchi kufikia hatua zilizopo leo,
 
Ndio hivyo huku bongo tunalipa TOZO.
hakuna chakufanya nchi ina watu milioni stini ila walipa kodi waliosajiliwa hawafiki milioni tano,wakati huo huo watu wanaofanya biashara ni lukuki,watanzania sisi wenyewe tunahamasishana na kulindana kutokulipa kodi,Maana yake ni kwamba watu wachache ndio waiendeshe nchi kwa kodi zao,ndio maaana mwishoni tozo zinawekwa ili kupanua wigo wa ulipaji kodi ingawaje pia watanzania wameisusa,hatuna uzalendo
 
Back
Top Bottom