Ifahamu historia ya Ziwa Nyasa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
IFAHAMU HISTORIA YA ZIWA NYASA

Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.

Lina urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.
Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania.

N1.jpg

Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.


Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.


Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali


Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.


Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.


Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.


Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa


Kutoka eneo la Ufukwe mpaka kulifikia Pango hili la Pomonda kuna umbali wa kilometa moja na robo. Pango hili la Pomonda limezungukwa na Miti ya Asili ambayo uneune wake hauzidi robo mita na umri wa miti hiyo yapata miaka 100,pango hili la Pomonda pia limezungukwa na Mawe yenye umbo la Mafiga Matatu kuzunguka eneo hilo mpaka kulimaliza unachukua muda wa saa . Hapo Mwandishi wa Habari Adam Nindi baada ya Kuzunguka katika kulifikia pango hilo inaonyesha jinsi gani alivyochoka akiwa amelala chini.


Taarifa zilizotolewa na Wazee waishio katika eneo la Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema kipimo cha ujazo wa Maji ya Ziwa Nyasa kujua yanapungua au yanaongezeka ni alama hizo zinazoonekana mistari mieupe na rangi nyeusi kuwa ziwa limepungua maji kwa kiasi kikubwa ambapo awali yalifikia katika mistari inayoonekana kwenye jiwe hilo ewa.

Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.
Kijiolojia ziwa ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Eneo la ziwa ni 29,600 km². Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya kusini-mashariki ni eneo la Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwepo katikati kufuatana na uzoefu wa kimataifa.

Sababu ya mzozo ni utaratibu wa kikoloni. Wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani palikuwa na mpaka wa kimataifa kaskazini mwa ziwa. Baada ya 1919 Uingereza ilitawala Tanganyika pamoja na Malawi (Nyasaland). Kwa kusudi la kurahisisha utawala mambo yote yaliyohusu ziwa yaliwekwa chini ya serikali ya kikoloni ya Nyasaland.

Baada ya uhuru Malawi ilijaribu kutumia uzoefu huo kama haki yake ya kitaifa. Polisi yake ilijaribu kutawala wavuvi na feri za Tanzania ziwani. Mzozo huu ulisababisha risasi kufyatuliwa baada ya uhuru. Hadi leo hakuna mapatano rasmi lakini nchi zote mbili zinaendelea bila kutumia nguvu. Hali halisi Malawi imeheshimu dai la Tanzania halikusumbua tena wavuvu au feri za jirani ndani ya robo ya kaskazini-mashariki ya ziwa.

Ziwa Nyasa linajulikana kuwa na aina nyingi za samaki (zaidi ya 1500). Aina chache tu zinavuliwa kama chakula lakini aina mbalimbali zinakamatwa na kuuzwa nje ya Afrika kwa wapenzi wa samaki zenye rangi.
 
Thanks! Ni taarifa nzuri sana kwa kweli, lakini kama taarifa hii hujaitayarisha wewe ni vizuri ukamtaja mtayarishaji kama kutambua mchango wake katika kufanikisha kazi hii
 
Hongera sana kwa kutuelimisha vilivyo. Ila hujatutajia sifa za bandari ya Mbamba bay. Hilo pango waweke umeme wa solar watalii na wanafunzi waweze kuona muundo wake ulivyo. Kwetu walichimba mapango chini ya ardhi na vita vikija wanaingia humo na mifugo yao. Waliweka sehemu ya mifugo, kulala, tundu la kutokea mtoni kuchota maji, tundu la kutolea moshi n.k. Kwa kweli sayansi ya nyakati hizo ilkuwa kiboko.
 
Thanks! Ni taarifa nzuri sana kwa kweli, lakini kama taarifa hii hujaitayarisha wewe ni vizuri ukamtaja mtayarishaji kama kutambua mchango wake katika kufanikisha kazi hii
Unaonaje na wewe ukaleta Historia yako na kumuweka aliye tunga hiyo Historia?
 
Asante sana Mzizimkavu kwa habari hii nzuri.
Kweli Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii.
Swali kwa wadau.
Malawi wanasema ziwa Nyasa lote ni lao.
Cha ajabu wanaidai Tanzania pekee lakini
Msumbiji hawawadai wakati ziwa hilo linamilikiwa pia na Msumbiji.
Ivi kwanini Malawi hawawasumbui Msumbiji katika kuwadai ziwa Nyasa na badala yake wanaisumbua Tanzania pekee ?
 
KUMBE HAWA MALAWI WANATAKA KUPIGWAAA.. NAOMBA TUISHI VIZURI NA MAJIRANI ZETU HASA HAWA WADOGO WADOGO WAKINA MALAWI
 
Hapo kwenye hayo mawe ndipo Mzee Chilundu alikuwa akifuga mamba wake,siku akikuhitaji hata kama huna tabia ya kuoga ziwani utaingiwa na hamu ya kuogelea halafu ndio utakuwa mwisho wako!
 
Thanks! Ni taarifa nzuri sana kwa kweli, lakini kama taarifa hii hujaitayarisha wewe ni vizuri ukamtaja mtayarishaji kama kutambua mchango wake katika kufanikisha kazi hii
Nisipokosei alinakili taarifa kwenye makala ya Wikipedia ya Kiswahili ona hapa Nyasa (ziwa) - Wikipedia, kamusi elezo huru

Siri ya mpaka upande wa Malawi / Tanzania ni kipengele katika mkataba wa mwaka 1890 kinachosema:
"In East Africa, Germany's sphere of influence is demarcated thus: ... To the south by the line that starts on the coast of the northern border of Mozambique Province and follows the course of the Rovuma River to the point where the Messinge flows into the Rovuma. From here the line runs westward on the parallel of latitude to the shore of Lake Nyasa. Turning north, it continues along the eastern, northern, and western shores of the lake until it reaches the northern bank of the mouth of the Songwe River. " (Anglo-German Treaty (Heligoland-Zanzibar Treaty) (July 1, 1890), article I,2, tovuti ya German History in Documents and Images, mradi wa German Historical Institute Washington, DC, iliangaliwa Machi 2019

Mwaka 1954 Waingereza walipatana na Wareno kuhusu mipaka baina ya koloni ya Msumbiji na Nyasaland. Kuhusu sehemu ile hakuna matatizo isipokuwa visiwa vya Chizumulu na Likoma vilihesabiwa sehemu za Nyasaland ingawa vimo katika sehemu ya maji ya Msumbiji, hivyo feri baina ya Malawi na visiwa hivi hupita katika maji ya Msumbiji lakini hakuna ugomvi.

1152742


kuhusu jina "Nyasa/Niassa" nimekuta hii: "Although ownership of the islands is not under dispute, the name of the lake is. Malawi obviously prefers "Lake Malawi". Most other nearby nations prefer "Lake Nyasa". According to Wikipedia, the name Nyasa came about from a mistake in translation. Upon arriving at the Lake, David Livingstone reportedly asked his guide for the name of the lake.

The word that came back was "Nyasa". However, nyasa basically meant "lake," the generic word not the lake's proper name (if it had one). Lake Nyasa stuck but should really be translated as "Lake Lake" in other languages. I have seen this happen many times when researching the history behind a place name for my maps. Many of the names for native peoples are the result of this type of confusion between a local population and foreign explorers. " (A Map of the Border between Malawi and Mozambique Near the Islands of Likoma and Chizumulu — am proehl)
 
Kwa Google map wamebadilisha jina ni lake Malawi, mpaka wao unapita kwenye pwani ya Tanzania hivyo ziwa linarudi upande wao
Screenshot_20220318-071926_Maps.jpg
 
Back
Top Bottom