Ifahamu dola ya Maya iliyooneshwa kwenye filamu ya Mel Gibson "Apocalypto"

Niunganishe na yoyote tu napenda kuandika andika
Daa mkuu mimi nilikuwa nafanya hobi tu,blog zenyewe nimezitelekeza sababu ya majukumu yangu mengine kunibana,wala sina connection na yeyote.Labda nikuachie blog moja ambayo haina post nyingi,lakini utakuwa na kazi ya kuvuta audience maana haina content na haijapostiwa kitambo
 
No mimi nilitaka tu niandike for fun. Yaani kama kuna mwenyewe anaisimamia mimi namsaidia tu kuandika hata bila malipo. Just for fun..
 
Miaka kadhaa tangu kutolewa kwa filamu ya Apocalypto(mwaka 2006),bado nimeguswa kuandika makala yangu ya kwanza kwenye blogu hii kuhusu filamu hiyo.Ninaipenda sana filamu hii.

Mel Gibson na Farhad Safinia ndio walioiandika Apocalpto.Wawili hawa walikutana kwenye matengenezo ya mwisho mwisho ya filamu nyingine nzuri iitwayo The Passion Of Christ,huko walipata muda wa kuzungumzia mapenzi yao kwenye mambo ya filamu.

Mazungumzo hayo ndiyo yalizaa wazo kuu la Apocalypto"mtu akikimbia kuokoa maisha yake,wakati huo huo akikirudia kitu anachokithamini mno"

Shauku ya kuonesha na kupitia utamaduni wa kizamani zaidi katika uhalisia wake kabla ya ujio wa wazungu,iliwafanya Gibson na Safinia kutumia dola ya zamani ya MAYA kwenye filamu ya Apocalpto.

Wasichokijua watu wengi ni kwamba mengi kati ya yaliooneshwa kwenye filamu ya Apocalpto ni mambo halisi kuihusu dola mashuhuri iliyopata kuwepo America ya kati(mexico ya sasa) miaka ya 2000BC,dola hiyo iliitwa MAYA.

Tamaduni nyingi zilizooneshwa kwenye Apocalpto, ni uhalisia wa tamaduni za WAMAYA halisi.Majengo ya piramidi yaliyooneshwa kwenye filamu,kilimo cha mahindi,kutoboa masikio,silaha za kijadi,kuishi katika jamii ndogondogo, lugha, na mfumo wa tarakimu ni miongoni mwa tamaduni halisi za Wamaya zilizooneshwa kwenye Apocalypto.

Kama ilivyooneshwa kwenye filamu,majengo ya piramidi ya WAMAYA ni ndogo kiasi ukilinganisha na zile za Wamisri.Watu wa make-up walifanya kazi nzuri kurefusha masikio ya waigizaji,kuyatoboa(kisanii tu,sio kiuhalisia) na kuyawekea plug ili wafanane na WAMAYA HALISI

Silaha zilizooneshwa kwenye Apocalpto ni za kutengenezwa na msanii wa kiingereza Simon Atherson ambaye kabla alizisoma na kuzifanyia tafiti silaha halisi za WAMAYA.

Kwenye filamu ya Apocalypto,mke wa starring(yule mjamzito) aliigiza kwa jina la Seven,alikuwa na tatuu kwenye mkono wake wa kushoto iliiyoonekana kama kamstari kalikolala na nukta mbili juu yake,hiyo ni alama ya namba saba kwenye mfumo wa tarakimu wa WAMAYA halisi
Lugha iliyotumika kwenye filamu ni KIMAYA cha Yucatec(zipo lugha za Kimaya za aina nyingi) lugha hizi bado zinazungumzwa mexico mpaka sasa.

Lengo la waandaaji wa filamu ya Apocalypto ni kuionesha dola ya MAYA kipindi ambacho ilikuwa inaanguka,dhana hii imebebwa na kukauka kwa mahindi(ukame),ugonjwa wa tauni(rejea kwenye filamu baada ya kuchukua mateka,msafara ulikutana na binti mwenye tauni ambaye alitoa utabiri fulani).

Katika uhalisia wake majanga ya asili na magonwa siyo miongoni mwa vitu vilivyosababisha dola ya MAYA kuanguka
Moja kati ya mafumbo makubwa ya kihistoria ni jinsi gani dola ya MAYA ilipotea,hakuna ushahidi wowote unaoelezea kupotea kwa dola ya MAYA.Hakuna historia ya kushindwa vitani au majanga ya asili(Anaandika Gerald Leinwand kwenye kitabu cha The Pageant Of World History)

Japo ilikwisha potea miaka ya 250 AD (maandishi hutofautiana) mapiramidi ya WAMAYA yanasimama msituni mpaka leo,vizazi vyake bado vinaishi mpaka sasa.

Hata hivyo kafara ya binadamu iliyooneshwa kwenye filamu ya Apocalypto si utamaduni wa kawaida wa WAMAYA halisi bali ni utamaduni wa kawaida sana wa Dola ya Aztec ambayo Gibson na Safinia(watunzi wa filamu) waliwahi kuifikiria kuitumia kwenye filamu ya Apocalypto kabla ya kuamua kutumia MAYAN CIVILIZATION

Safi sana! Niliwahi kufika kwenye kwenye himaya ya Maya huko Chichen Itza, Mexico mwaka 2017. Makala yako imenikumbusha mbali sana!
 
SALUTE COMRADES

Hii mijengo hapa chini ni mijengo iliyojengwa miaka mingi zaidi kabla ya Kristo, enzi hizo teknolojia ya usafiri ilikua chini!

Swali ni je, nani aliyezunguka bara moja kwenda lingine kusambaza hii teknolojia?

Ikumbukwe mpaka leo hii mzungu hajaweza gundua haya majengo yalijengwa vipi. Yapo bara la Africa, Asia na America.

IMG_20180419_184354.jpg

Pia tujiulize kwanini yote yamejengwa na milango mitatu na mmoja mkubwa wa katikati? Nini maana yake? Nini maana ya namba 3?

Leonardo Da'Vinci katika mchoro/picha yake inayofahamika kama The Last Supper, pia ameweka hiyo milango mitatu!

FB_IMG_1517049322221.jpg
misri i Katikati ya Dunia nani alijenga hizi. tofali moja tani 200 how!? nani alizitumia kwa matumizi yepi hizi, kwa technonlojia ya kizamani
, kwa nni zinalenga sayari maalum km Nibiru kingine bana kuba kwa nini Misri iko katikati ya hizi Pyramids, na kidunia pia iko katikati?? UFo walizitumia km rada zao
 
unaweza kuwa sahihi lakini hizo ni nadharia ambazo haziwezi kuwa proved.....yet
 
Pale mwishoni ule mfupa wa nguruwe ulimponza jamaa yule kiongozi kuja kugeuka mtego huu hapa, alikufa kizembe sana.
Halafu mwishoni kabisa zinaonekana meli za wazungu zinakuja ..
 
Miaka kadhaa tangu kutolewa kwa filamu ya Apocalypto(mwaka 2006),bado nimeguswa kuandika makala yangu ya kwanza kwenye blogu hii kuhusu filamu hiyo.Ninaipenda sana filamu hii.

Mel Gibson na Farhad Safinia ndio walioiandika Apocalpto.Wawili hawa walikutana kwenye matengenezo ya mwisho mwisho ya filamu nyingine nzuri iitwayo The Passion Of Christ,huko walipata muda wa kuzungumzia mapenzi yao kwenye mambo ya filamu.

Mazungumzo hayo ndiyo yalizaa wazo kuu la Apocalypto"mtu akikimbia kuokoa maisha yake,wakati huo huo akikirudia kitu anachokithamini mno"

Shauku ya kuonesha na kupitia utamaduni wa kizamani zaidi katika uhalisia wake kabla ya ujio wa wazungu,iliwafanya Gibson na Safinia kutumia dola ya zamani ya MAYA kwenye filamu ya Apocalpto.

Wasichokijua watu wengi ni kwamba mengi kati ya yaliooneshwa kwenye filamu ya Apocalpto ni mambo halisi kuihusu dola mashuhuri iliyopata kuwepo America ya kati(mexico ya sasa) miaka ya 2000BC,dola hiyo iliitwa MAYA.

Tamaduni nyingi zilizooneshwa kwenye Apocalpto, ni uhalisia wa tamaduni za WAMAYA halisi.Majengo ya piramidi yaliyooneshwa kwenye filamu,kilimo cha mahindi,kutoboa masikio,silaha za kijadi,kuishi katika jamii ndogondogo, lugha, na mfumo wa tarakimu ni miongoni mwa tamaduni halisi za Wamaya zilizooneshwa kwenye Apocalypto.

Kama ilivyooneshwa kwenye filamu,majengo ya piramidi ya WAMAYA ni ndogo kiasi ukilinganisha na zile za Wamisri.Watu wa make-up walifanya kazi nzuri kurefusha masikio ya waigizaji,kuyatoboa(kisanii tu,sio kiuhalisia) na kuyawekea plug ili wafanane na WAMAYA HALISI

Silaha zilizooneshwa kwenye Apocalpto ni za kutengenezwa na msanii wa kiingereza Simon Atherson ambaye kabla alizisoma na kuzifanyia tafiti silaha halisi za WAMAYA.

Kwenye filamu ya Apocalypto,mke wa starring(yule mjamzito) aliigiza kwa jina la Seven,alikuwa na tatuu kwenye mkono wake wa kushoto iliiyoonekana kama kamstari kalikolala na nukta mbili juu yake,hiyo ni alama ya namba saba kwenye mfumo wa tarakimu wa WAMAYA halisi
Lugha iliyotumika kwenye filamu ni KIMAYA cha Yucatec(zipo lugha za Kimaya za aina nyingi) lugha hizi bado zinazungumzwa mexico mpaka sasa.

Lengo la waandaaji wa filamu ya Apocalypto ni kuionesha dola ya MAYA kipindi ambacho ilikuwa inaanguka,dhana hii imebebwa na kukauka kwa mahindi(ukame),ugonjwa wa tauni(rejea kwenye filamu baada ya kuchukua mateka,msafara ulikutana na binti mwenye tauni ambaye alitoa utabiri fulani).

Katika uhalisia wake majanga ya asili na magonwa siyo miongoni mwa vitu vilivyosababisha dola ya MAYA kuanguka
Moja kati ya mafumbo makubwa ya kihistoria ni jinsi gani dola ya MAYA ilipotea,hakuna ushahidi wowote unaoelezea kupotea kwa dola ya MAYA.Hakuna historia ya kushindwa vitani au majanga ya asili(Anaandika Gerald Leinwand kwenye kitabu cha The Pageant Of World History)

Japo ilikwisha potea miaka ya 250 AD (maandishi hutofautiana) mapiramidi ya WAMAYA yanasimama msituni mpaka leo,vizazi vyake bado vinaishi mpaka sasa.

Hata hivyo kafara ya binadamu iliyooneshwa kwenye filamu ya Apocalypto si utamaduni wa kawaida wa WAMAYA halisi bali ni utamaduni wa kawaida sana wa Dola ya Aztec ambayo Gibson na Safinia(watunzi wa filamu) waliwahi kuifikiria kuitumia kwenye filamu ya Apocalypto kabla ya kuamua kutumia MAYAN CIVILIZATION

Wiki iliyopita DStv wameirudia hii filamu yaani naipenda sana . Maya CiVIliZATiON 🔥
 
Back
Top Bottom