If Chadema change position it mustt apologize, unconditionally!

Hizi siasa za Afrika hovyo kabisa. Watu hawana misimamo...wanapelekeshwa na upepo tu. Mara huku mara kule yaani ili mradi tu....
 
Sijawahai kusikia wanasiasa wa ki-afrika hasa Tanzania wanaomba radhi, mambo hayo yapo ulaaaaaya na sio Afrika.
 

Mimi nadhani CHADEMA kama chama hawana cha kuapologize kwani mtizamo ambao ulichakachuliwa kuwa msimamo wa kutomtambua Rais Kikwete ulikuwa ni wa baadhi ya viongozi wa Chadema na sio chama cha Chadema. Viongozi hao ni Katibu Mkuu Dr Slaa na Mkurugenzi wa Sheria Tundu Lissu. Hata Mwenyekiti wao katika matamshi yake alisisitiza kuwa wanamtambua RAis Kikwete ingawa wana malalamiko. Kosa la Mwenyekiti ni kuwa hakuwa tayari kusiamama kidete kukinzana na nia na maslahi ya Dr Slaa. Ama kwa sababu alikuwa akiogopa kupingangana na nguvu za Dr Slaa kisiasa ama kutomtelekeza Dr Slaa ambaye nyakati zote za nyuma alikuwa tayari kuunga mkono mitizamo na misimamo yake (Mwenyekiti) hata kama haikuwa sahihi na inayogharimu CHADEMA.

Kuhus political expediency nadhani msimamo wa kutomtambua RAIS Kikwete ndio ilikuwa political expediency kwani hakulenga hali halisi na wala maslahi ya Taifa zaidi ya maslahi ya nafasi ya kisiasa ya Dr Slaa na kulinda ushabiki ama mtaji wa kisiasa wa Chadema.

Walichokifanya Chadema kama chama yaani maamuzi na mtazamo wa Kamati Kuu yao ni political maturity ambayo kwa jinsi nilivyomuona Dr Slaa anavyospin maamuzi ya hayo (katika press conference ya leo ambayo nadhani wameshindwa hata kuandika full statement kwa kuhofia kulazimika kula matapishi yao) ni wazi yeye na wenzake hawajapata somo hilo. Inaelekea hulka ya kuamini katika siasa za chuki na drama zimeziba kabisa nafasi ya umakini katika utashi wao......

Lakini pia nadhani kitu pekee ambacho viongozi ama wanaCHADEMA wanaoendelea kudai kuwa ushindi wa Rais Kikwete ulitokana na uchakachuaji wa kura kwa upande wa NEC wanapaswa kukifanya ni kuweka wazi huo wanaoita ushahidi wa uovu huo....angalao kwa asimilia 25 ya matokeo yote majimboni....na hapa sio lazima watuonyeshe taarifa za kituo hadi kituo kwani ni wazi hata capacity hyo hawakuwa nayo....

Bila ya kufanya hivi watakuwa wanainajisi ajenda ya katiba mpya kwani wengi tutaendelea kuhoji uthabiti wao katika hili na kudhania ama kuamini kuwa its just another political game (expediency)....
 
MMM,

Wengine tuliona haya kitambo sana... so it is not so far a news to us!
 

Remmy,
Hayo yote uliyoyasema yana ukweli kiasi fulani; nafikiri hoja ya MKJJ ni kwa nini CDM wameshindwa ku-stick ktk hoja za msingi za kutokukubaliana na matokeo ya urais; km ni kweli sasa wanamtambua rais, basi yale matendo yote waliyoyafanya na maneno yote yaliyosemwa mara tu baada ya kutangazwa rais na yale yaliyotokea bungeni bungeni inabidi kuomba radhi kwa yaliyotokea...
 
You can't go to the fight if you all your generals are not in for the fight! u better surrender to spare an onslaught and humiliation.
 

You could not say it better.
 
Mimi nichojua Chadema inapikwa inapitia kwenye tanuru la moto isingekuwa na uongozi imara leo ingekuwa historia, ina viongozi wanaoona mbele kwa sana, nachelea kusema angekuwa Mwenyekiti wake sawa na Mrema leo Zitto angekuwa ametolewa wala CC ya CDM isingeliunda kamati ya wazee angeamua yeye. So chama kiko strategic ndiyo maana kinashangaza wengi kwa maamuzi yao nani alijua Slaa angegombea urais ni wachache sana.

Mimi nina imani soon wananchi wataelewa nini maana ya kumtambua rais leo na si kabla, ile walkout pia ilikuwa strategic imelipa watu leo wanaongelea katiba wazee wa CCM wanaongelea katiba na usione ajabu hata la kumtambua rais lina malipo yake si bure inawezekana kuna mazungumzo kati CDM na CCM na Mabalozi na sharti la kwanza lazima wamtambue rais who knows wait and see.
 
Mwanakijiji this sound like early xmas suprise!!..niaje?!!umeniacha njia panda
 

nakubaliana na wewe mkuu...there iz something going on btwn cdm n goverment
 

Mwanakijiji, I think you are on your death bed, and should continue to remain a mystery. Once upon a time, you were CCJ die hard fan. That came to pass, you jumped CHADEMAS train, and that is becoming history. I can see you are rushing to fly high CCM's flag, Good for you!

in my world, you are a nobody, and those glorifying you are as dumb as you are. I have never seen any man with sanity using so many aliases.Ndulu mwana wa Nzela, and the list goes on. What are you concealing? If you are a good man, then let be known who you ar,e and yout true intents. I guess you have swallowed a big peace of the DOWANS cake?

Of political prostitutes, and hypocrates I have ever come across, You are topping the list. You are more dangerous, than Mrema, Marando and even Zitto Kabwe. I guess you have blood relationship with the CCJ founder, and can only wish you all the best in your effort to scruttle CHADEMA. Good luck in the name of JF where we dare talk freely.
 
To add, MMJ soon you get the destin. We in CDM believe we will get KATIBA mpya kwa amani sio ngangari kama unavyotaka, tutashinda kwa nguvu ya hoja hata roma haikujengwa siku moja. Kikubwa ktk siasa uwe tolerance, na hilo chadema imetumia akili ya hali ya juu kujishusha na kuondoa ujinga wa CCM ambao ulianza kusambazwa kupakaza CDM chama cha fujo, give a time
 

Mwanakijiji,

Nashukuru kwa mwito wako. Naelewa kwamba habari za tarehe 13 Disemba za baadhi ya magazeti zilizoandika habari yenye mwelekeo wa kuashiria kuwa "CHADEMA imebwaga manyanga' katika suala la kumpinga Kikwete. Na habari za tarehe 14 Disemba zikimnukuu Dr Slaa akielezea maamuzi ya kamati kuu zinaweza kuwa zimeleta hisia tofauti kuhusu mwelekeo wa ajenda husika.

Naomba ieleweke kwamba CHADEMA haijabadili msimamo wake katika kuuelezea mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu kwamba haukuwa huru na wa haki na hivyo kutoyatambua matokeo yaliyotangazwa na NEC yaliyompa ushindi Kikwete. Hata hivyo, jambo jipya lililojitokeza kwenye maelezo ya maamuzi ya kamati kuu ni kuipanua ajenda ya katiba mpya kutoka katika kuzungumza zaidi kuhusu tume huru ya uchaguzi na kuingiza masuala ya msingi ya kikatiba kama mamlaka ya Rais, mifumo ya uwajibikaji wa viongozi, haki za binadamu nk. Hii inafanya ajenda ya katiba isiwe ya kiuchaguzi pekee bali ya mfumo mzima wa maisha ya watanzania na kustahili kuungwa mkono sio na vyama vya siasa bali umma wa watanzania kwa ujumla wao.

Sintofahamu hii inaweza kuwa imechangiwa na kauli ya kuanza kushiriki shughuli za kiserikali baada ya kususia hotuba ya Rais pale Dodoma; ni muhimu ikafahamika hali hii haitabadili mwelekeo wa msimamo.

Ajenda ya katiba mpya naamini itaendelea kudaiwa kwa juhudi zote za kibunge na za kuunganisha nguvu ya umma nje ya vyombo vya maamuzi. Binafsi naamini kwamba katiba haipaswi kudaiwa bungeni pekee, inapaswa kudaiwa mitaani kupitia mijadala, maandamano na njia nyingine za nguvu ya umma. Hii ni kwa sababu watawala wa Tanzania wanaelekea kutokuwa tayari kukubaliana na ridhaa ya umma katika suala hili. Hivyo, hakuna kurudi nyuma!

Ni changomoto tu kwamba maamuzi ya kamati kuu kuhusu suala hili kwa maana ya habari yamefunikwa na habari ya hatua ambazo wabunge wa CHADEMA tumechukua dhidi ya wabunge wenzetu wawili katika vikao vililivyopita. Naamini baada ya siku chache mjadala utarudi katika mstari wake kwa sababu mijadala ya masuala hudumu kuliko mijadala ya watu. Nawatakia mjadala mwema!

JJ

JJ
 
We said it and will keep on saying; CHADEMA needs a major overhaul in its leadership given its current growth and influence. The likes of Mbowe can no longer afford to manage such a big party.
The decision of CHADEMA CC is very right though too late, however repairable. We have witnessed alot of inconsistencies with respect to post election decision making and election pledges. We highlighted their applicability from the campaign and after election. CHADEMA as a party should and must have people who can make clear and concise decision. The image of the party is no longer reflect the views of the few. Tanzanians need changes and are ready to vote for any party that can represent their interest as a nation and not a group that is viewed to be affiliated with particular individuals. The kind of inconsistencies that have shown over the recent, literate clearly that the party was not ready to lead the country. Its time now for CHADEMA to make hard decision with respect to any person who is concerned.
 

Mheshimiwa Mnyika,

Kwanza asante sana kwa kurudi dimbani na kuchanganua mengi ambayo yapo hewani. Sote tunakubali swala la uchaguzi kutokuwa huru na haki, na sote tufahamu ya kwamba JK ni tokeo la uchaguzi ambao haukuwa huru na haki.

Lakini statement yako hapo juu inakinzana na maamuzi mliyochukua awali. Lengo la CDM kutoka bungeni ni sababu mlikuwa hamtambui JK. Mlivyosusia kuapishwa ni sababu hamumtambui JK. Sasa leo mnamtambua JK lakini hamtambui process iliyomchagua? I find this statement very confuse, i argue to you and your colleagues to evaluate again what position is necessary for the party.

I find very hard to believe that we're going to win constitution battle ahead of us. It's obvious that poor judgment lead CDM to this grave yard.

Mwisho, tunashukuru sana kwa kurudi kwako hapa jamvini na kuendeleza libeneke la maendeleo ya Tanzania.
 
Hapo kwenye bold ndio hamueleweki. Ukisema hautambui mfumo ulimuweka mtu madarakani halafu ghafla mnamtambua mtu aliyewekwa madarakani, ni tatizo. Hizi kauli za kijanjajanja si muafaka wakati wa sasa. Kama mmeamua kumtambua fanyeni hivyo kwa haraka na ila kugeuka nyuma na kusonga mbele na kama hamumtambui semeni tu wazi hatumtambui bila kuzungukazunguka, mara mfumo mara oh....
Kwenye suala la katiba mnastahili hongera maana mko very clear na ninaamini wananchi wengi wanaopenda maendeleo ya nchi yetu wanaliona hivyo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…