If Chadema change position it mustt apologize, unconditionally!


Al Gore alitambua matokeo ya uchaguzi Florida directly or by extension, bila hivyo asingetoa concession speech.

Hilo lingine la accused kutoa access kwa watu wengine waweze ku verify ni optional. Kama kila mtu angefungua milango ya nyumba yake ili kusudi tu a refute accusations za every Tom Dick and Harry basi watu wasingeweza hata kwenda kazini.

Bottom line ni, ushahidi wa CHADEMA uko wapi? Au ndizo zile excel spreadsheet ambazo zenyewe ni uchakachuaji wa kuchakachuliwa ?
 

FM:

Lakini kuna tofauti kubwa kati ya Al Gore na Dr. Slaa. Kama unavyosema Al Gore alipeleka kesi na mahakama ilitoa uamuzi. Kwa upande wa Tanzania tunasikia tu kuwa katiba inasema hivi inasema vile. Kwanini mahakama isitumike kufanya maamuzi?

Kuna watanzania wanaosema kuwa majina yao hayakuwemo kwenye daftari. Kwanini hawafungui mashitaka kudai haki zao za kiraia? Kuiba kura za uchaguzi na kumpa mgombea mwingine ni kosa la jinai. Mahakama inaweza isitengue matokeo, lakini ina uwezo wa kusikiliza kesi ya kukiukwa kwa utaratibu.
 

Tofauti ni kuwa hauwezi hapa kwetu kwenda Mahakamani kuiomba itoe hukumu kama ilivyokuwa kwa Al. Gore. Ndiyo maana kuwa pamoja na misgiving zilizokuwepo, Jaji Mkuu aliwajibika kumuapisha mshindi aliyetangazwa na Tume. Pangekuwa na mwanya huo basi uapishwaji ungebidi usubiri resolution ya kesi ambayo bila shaka CDM wangefungua. Na hata Marekani, uamuzi wa Supreme Court ni final kwenye issue kama hiyo. Hata kama Al Gore na wengine wengi wataamimi kuwa Supreme Court ilimpendelea mtu wao, ilimbidi anyanyue mikono.

Hilo la kuishtaki Tume kwa kukunyima haki yako ya msingi sina uhakika nalo.

Amandla........
 

Majaji wote wa mahakama za Tanzania ni appointees wa marais wa CCM. Sasa unategemea nini hapo? Usidhani kuwa hata kwenye mahakama hakuna siasa...zipo.

Supreme Court ya Marekani yenyewe katika kuamua Gore v. Bush ilikuwa split 5-4. Guess wale Justices watano walio side na Bush walikuwa appointed na nani?

Sisi ni hadi tudundane kidogo ndo tutapata akili la sivyo we are doomed.
 

Al Gore ali-concede baada ya wakina Rehnquist kuzuia kura kurudiwa kuhesabiwa Florida akijua kuwa hao ni final authority. Vile vile kwa CDM kumtambua Rais kisheria kwa vile ameishaapishwa na hakuna wanachoweza kufanya kisheria kubatilisha hilo.

Hilo la kutoa access linategemea unavyo-value heshima yako na ni nani amekutuhumu. Kama ukiona kuwa tu wote watakuamini kuliko lofa FM basi hautakuwa na haja ya kufungua mlango. Na kama every Tom, Dick and Harry anakushutumu kuwa kuna unga nyumbani kwako basi itabidi uwatie kibano wote unaoishi nao isije ikawa wanaingiza unga wakati wewe haupo!

Amandla.....
 

.
Mpangilio na mtiririko wa kiuandishi ni omarilyas lakini akili iliyofikiri hapa ni ya Makamba(sisiem Gs).
Mwingiliano wa ID or password hacked??
 
Na hata Supreme Court ya Florida nayo ilikuwa split vilevile. Mkumbuke Gore v. Bush haikwenda moja kwa moja kwenye US Supreme Court
 

Ndiyo maana narudisha swali kwenye substantive measures za kubadili katiba na kuhakikisha haya hayarudiwi tena, CHADEMA ina mkakati gani?

Ama sivyo ttakalia fluff za kutoka bungeni, kupinga matokeo etc, halafu come 2015 hakuna mkakati, haya haya ya 2010 yanajirudia.

Ikiwa hivyo CHADEMA haitaweza kusema kwamba hatukuonya.
 

FM:

Unaposema hapa kwetu huwezi kwenda mahakama, unatoa maoni yako au mahakama yenyewe imesema? Mpaka sasa mnatoa maoni yenu tu.
 

Mbona majaji haohao walimpa ushindi Mtikila kwenye kesi ya mgombea huru? Kumbuka jaji anateuliwa kwanza akiwa na sifa za utaalamu wake.
 
FM:

Unaposema hapa kwetu huwezi kwenda mahakama, unatoa maoni yako au mahakama yenyewe imesema? Mpaka sasa mnatoa maoni yenu tu.

Katiba inakataza Mahakama kuchunguza matokeo yaliyoishatangazwa na Tume. Kama hawawezi kuchunguza basi hata kusikiliza hawataweza. Kichuguu ametubandikia hii: ibara ya 41 kifungu cha 7 kinasema hivi: "Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Watu hawaandikii mate humu!

Amandla......
 

Lakini si hiki ndicho kinachoendelea?

Amandla....
 
Mbona majaji haohao walimpa ushindi Mtikila kwenye kesi ya mgombea huru? Kumbuka jaji anateuliwa kwanza akiwa na sifa za utaalamu wake.

Ushindi wa Mtikila hauku affect matokeo ya ushindi wa mtu yeyote

Unadhani kama wakipelekewa kesi ambayo kuna potential ya matokeo kutenguliwa in favor ya opposition watatenda haki?
 

FM:

Nimekisoma hicho kipengere mara nyingi na nimetoa comments zangu. Kipengere hicho kinasema kuchunguza. Ki-semantic pekee yake kuna utata kwani sio kazi ya mahakama kufanya uchunguzi. Kazi ya mahakama ni kufanya deliberation. Hivyo unaweza kufungua kesi kwa kutumia semantic ya lugha iliyotumika.

Kwa kutumia kipengere hicho ina maana NEC ingeweza kumtangaza mtu yoyote aliyegombea kiti cha urais na watanzania walitakiwa kumkubali. Kwa mfano NEC wangeweza kumtangaza DOVUTWA wa UPDP kuwa rais na mahakama isingeingilia kati na vyama vingine vilitakiwa kumkubali.

Je NEC ingetangaza MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT wa TLP kuwa rais, CCM isingeenda mahakamani? Na kama ingeenda mahakama ingeenda kwa misingi gani?
 
Ushindi wa Mtikila hauku affect matokeo ya ushindi wa mtu yeyote

Unadhani kama wakipelekewa kesi ambayo kuna potential ya matokeo kutenguliwa in favor ya opposition watatenda haki?

Tanzania inafuata common laws. Hivyo ushindi wa mahakama hata kama ni symbolic una-set precedence kwa kesi zinazokuja. Hivyo kufungua kesi mahakama ni lazima JK atenguliwe urais na Dr. awe rais mara moja. Lakini mahakama inaweza kujenga misingi ya uchaguzi wa 2015 na kuendelea.
 

Sorry I just don't see it happening until I see it happen.
 
Lakini si hiki ndicho kinachoendelea?

Amandla....

Mambo yote yanakwenda na wakati. Wanafunzi China walifanya maandamano makubwa 1989. Na watu wakafikiri ndio mwanzo wa demokrasia. Ghafla bin vuu uchumi ukaanza kukuwa 20% kwa mwaka kila mtu kasahau mabadiliko ya kisiasa.
 
Chadema walikuwa na nafasi ya kwenda mahakamani kuzuia tume isiendelee kutangaza matokeo kwa sababu ya injury ambayo they were likely to suffer; jibu tulilopewa tuliouliza wakati ule ni kuwa "sheria inakataza". Hadi hivi sasa sijajua ni sheria gani inakataza chama kuzuia matokeo mahakamani kabla hayajatangazwa.
 

Kuchunguza si kuhoji? Mahakama inapodai ushahidi na kuwahoji mashahidi si wanafanya uchunguzi wa haki iko wapi?

Tatizo la Katiba yetu ndiyo hilo. Hii ni katiba ya chama kimoja iliyowekwa viraka. Nadhani kipengere hiki kililenga uchaguzi wa chama kimoja ambapo kweli pasingeweza kutokea upinzani kutoka ndani ya hicho chama. Au haikuangalia uwezekano wa chama tawala kushindwa au uwezekano wa Tume iliyochaguliwa na rais kufanya uhuni na kumuweka mtu yeyote wamtakaye kwa sababu zake.

Hii ni kama vile hali tuliyokuwa nayo kuwa chama kimoja kinaweza kuwa sehemu ya serikali na kuwa chama pinzani ndani ya nchi hiyo hiyo!

Amandla.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…