Iddi Simba vs Zitto - Kamati ya Madini

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
138
9
Sasa ninaamini kwamba JK anafuata usauri wa WanaJF kijiwe kidumuu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Kikwete amemteua na kumwongeza Mhe. Iddi Simba kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya kuangalia upya mikataba ya uchimbaji wa madini, Kamati ambayo iko chini ya Uenyekiti wa Mhe. Mark Bomani.

Mhe. Iddi Simba ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Ilala.

Wajumbe wengine waliokwisha teuliwa ni:

Mhe. John Momose Cheyo
(Mbunge) - Bariadi Mashariki (UDP) - Mjumbe

Mhe. Zuberi Zitto Kabwe
(Mbunge) - Kigoma Kaskazini
(CHADEMA) - Mjumbe

Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe
(Mbunge) - Kyela (CCM) - Mjumbe

Mhe. Ezekiel Magolyo Maige
(Mbunge) - Msalala (CCM) - Mjumbe

Bw. Peter L. Machunde - Soko la Hisa, DSM
(DSE) - Mjumbe

Bw. David Tarimo - PriceWater Coopers - Mjumbe

Bi Maria N. Kejo - Mkurugenzi wa Madai
na Sheria za Kimataifa
Wizara ya Katiba na Sheria) - Mjumbe

Bi. Salome Makange - Mwanasheria wa Wizara
ya Nishati na Madini - Mjumbe

Bw. Mugisha Kamugisha - Kamishna wa Sera
Wizara ya Fedha - Mjumbe

Bw. Edward Kihundwa - Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi
Wizara ya Ardhi - Mjumbe

Ikulu,
DAR ES SALAAM.
 
Sikubaliani na Uteuzi wa Idd Simba kwa sababu moja nayo ni kuwa mwanawe Simba wa kike kwa jina Sauda ni mwajiriwa wa kampuni ya Barricks (officer) kwa hiyo kuna utata kidogo pamoja na kwamba nafahamu kuwa ni mjumbe mzuri sana ktk maslahi yetu na hasa ktk swala la Uzawa.
 
Mh naona hapa hata akijiteua raisi mwenyewe tutatia neno tu...'mbona yeye si mtaalam wa madini' nk. Nadhani la muhimu ni kwa kamati kuwa huru kupokea michango mbalimbali ya wataalam katika mambo ya mikataba na sheria na madini etc kisha wayafanyie kazi,,,
 
Duh! hili la wataalam wa madini limetoka wapi tena? jamani nimeandika uhusiano wa kidamu kati ya Simba na mwajiriwa wa Barricks ambaye ana position kubwa ktk shirika hilo. Ni mawazo yangu unaweza weka hoja yako inayopingana na ukaeleza sababu zinazokupa imani ktk uchaguzi wa Idd Simba kwenye kamati hii.
 
Bi Maria N. Kejo - Mkurugenzi wa Madai
na Sheria za Kimataifa
Wizara ya Katiba na Sheria) - Mjumbe

Kwa maoni yangu, huyu mama angeondolewa maana huenda na yeye akawa mtuhumiwa when the end ya hii kitu itakapofika, lakini I have all my trust in Dr. Mwakyembe, Zitto, na Idd Simba,

Hapo ninasema kutawaka moto, ambao ni profitable kwetu wananchi maana hawa huita Spade a Spade, na hasa Idd Simba na Zitto, ambao they have nothing to lose but only to gain politically na hii kamati,

Na salam zangu kwa Muungwana, ni kwamba what is next betweeen hizi kamati ndio hasa kutakuwa na hukumu ya kazi yake toka aingie urais, na wananchi tunasubiri kwa hamu jinsi Msekwa( a former Vodacom employeee), Luwassa, na Sitta, watakavyofanya kazi pamoja for the benefit of us wananchi at large!
 
Sikubaliani na Uteuzi wa Idd Simba kwa sababu moja nayo ni kuwa mwanawe Simba wa kike kwa jina Sauda ni mwajiriwa wa kampuni ya Barricks (officer) kwa hiyo kuna utata kidogo pamoja na kwamba nafahamu kuwa ni mjumbe mzuri sana ktk maslahi yetu na hasa ktk swala la Uzawa.

huyo mwanae simba aliajiriwa kwa sababu ni mtoto wa iddi simba au kwa sababu alitimiza vigezo ?? nauliza tu !
 
in the ideal situation JK alitakiwa azingatie: 1. TOR ya kamati 2. Sifa/uwezo anaotakiwa awe nao mjumbe wa kamati 3. ameridhika kwamba katika watanzania wote...hao watu aliowateua ndio wenye sifa ya kufanya hiyo kazi. 4. 'define conflict of interest in this issue 5. decide where there is potential conflict of interest whether the work of concerned member(s) on the committee is still tenable and will not prejudice the outcome of the work of the committee. bottom line: Je are there binding established rules and procedures which the government/ president must follow in appointing such committees? anafuata muongozo upi?
 
Sikubaliani na Uteuzi wa Idd Simba kwa sababu moja nayo ni kuwa mwanawe Simba wa kike kwa jina Sauda ni mwajiriwa wa kampuni ya Barricks (officer) kwa hiyo kuna utata kidogo pamoja na kwamba nafahamu kuwa ni mjumbe mzuri sana ktk maslahi yetu na hasa ktk swala la Uzawa.

Mtoto wa mzee Simba, Bi Sauda Simba-Kilumanga ni mwajiriwa tu wa kampuni hiyo, si mwanahisa, kwa hiyo suala la conflict of interest silioni. Sioni ni kwa nini labda Mzee Simba atetee kampuni ambayo mwanaye ni mwajiriwa tu ambaye anaweza kuhama kampuni hiyo siku yoyote kulingana na mtazamo na utashi wake (Sauda) binafsi. Ikumbukwe kwamba kabla ya huko huyo binti alishafanya kazi IPP media (ITV) na Tanzania Breweries. Sasa kama ni kuwa na conflict of interest na kampuni anakofanyia kazi binti, mzee atashikamana na makampuni mangapi?

Mimi namwamini Mzee Simba kwamba ni mtu makini, mwenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo, na mtetezi mkubwa wa hoja ya kutaka wazawa wawe na nguvu za kiuchumi. Hapo kama ni mchezo wa karata naona kamati imelambishwa dume, kilichobaki wafanye kazi tu basi. Nadhani kwa muundo (composition), hii ni miongoni mwa kamati bora sana zilizowahi kuundwa nchini. Ina vichwa vizuri.
 
Kithuku na Kada,
Niliyotoa ni mawazo yangu binafsi na sababu kubwa nayoweza kuisema ni kutokana na experience yangu ktk maswala kama haya hasa kwetu sisi Wadanganyika inapoingia swala la mahusiano kati ya mwanao na mwajiri wake. Hata uchaguzi wa Jury ktk mahakama zetu huangalia vitu kama hivi kwani sii lazima awe na hisa ila hata ajira ndio inayoendesha maisha ya mwanae - Yote yanahusiana na fedha.
Binafsi namuamini Simba kama nilivyowahi kuwaamini viongozi wengine lakini pamoja na yote haya nimejifunza kitu kimoja kuwa family interest comes first before anything!
Dr. Slaa amezungumza mengi yenye maana zaidi kuhusiana na kamati hii kama utasoma hotuba yake kwa makini na katoa solution nzuri sana kuwa kamati ichaguliwe toka bungeni kuepuka yale yaliyokwisha tokea huko nyuma. Nitarudia kusema ni mawazo yangu binafsi na sii lazima yawe na ukweli ama yafuatwe..
Bi. Sauda kafanya kazi ITV na hiyo kampuni ya bia lakini sidhani kama maswala ya kampuni hizi yapo mezani leo hii wala hazihusiani kabisa na mashaka yangu.
 
huyu slaa sasa anajifungafunga kamba mwenyewe na alivyokuwa jeuri hataki hata kuomba msaada wa kufunguliwa hiyo kamba maana anajizunguka tu mwenyewe na kivuli chake. leo anasema hivi kesho vile keshokutwa vileee yaani tabu kweli !
 
mwaka huu mambo yamewakwama kooni nje hayatoki ndani hayaendi.

na tumewashtukizia muongo muongoze. na tuna msemo mchawi mpe mwana kulea.

sasa tunawaangalia watasemaje
 
mwaka huu mambo yamewakwama kooni nje hayatoki ndani hayaendi.

na tumewashtukizia muongo muongoze. na tuna msemo mchawi mpe mwana kulea.

sasa tunawaangalia watasemaje

itabidi slaa apewe mtoto alee (mwanakijiji preferably) !! teh teh !!
 
Back
Top Bottom