TPA imesifiwa sana kwa kutoa Gawio la Bilioni 153.9 wakati 2018/19 Gawio lilikuwa Bilioni 480. Je, Rais Samia kasahau?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,700
55,688
Maswali chechefu:

1. Je, kwanini Mhe Rais Samia jana aliisifu TPA na kuimwagia minyama kwa "Gawio kubwa ambalo halikuwepo huko nyuma" baada ya kupokea Gawio la Tshs 153.9 toka kwa Mkurugenzi Mkuu, Bw. Mbossa na Mjumbe waBodi, Bw. Minja?

2. Je, Mhe Rais hajui kuwa kuna miaka TPA ilikuwa inatoa Gawio mara tatu zaidi ya Gawio hilo kiduchu la jana ?

3. Je, Mhe Rais Samia anajua kuwa Desemba 21, 2019, Mhe Isaak Kamwele, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano, alimchimba mkwara Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko, kuwa Gawio la Tshs 480 B la 2018/19 ni dogo mno, na kumtaka ahakikishe 2019/20 Gawio linafika Tshs Trillion moja vinginevyo atamfukuza kazi?

4. Je, nini kimetokea hadi nchi yetu tunafurahia kupata gawio la mchango ie Tshs 153.9 B wakati tuliishawahi kujiwekea lengo la Tshs Trillion moja?

🤔🤔

NUKUU

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini, Isack Kamwelwe ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuongeza gawio kwa Serikali kutoka Sh480 bilioni la mwaka 2018/19 hadi Sh1 trilioni mwaka 2019/20.

Amesema jambo hilo lisipotimia atamfukuza kazi mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Deusdedit Kakoko.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 21, 2019 katika uzinduzi wa bodi mpya ya mamlaka hiyo yenye wajumbe saba ikiongozwa na Profesa Ignas Rubaratuka aliyeteuliwa kwa mara ya pili.


=======

UPDATES: 16 JUNI 2024

========


UFAFANUZI KUTOKA TPA JUU YA TOFAUTI YA GAWIO

Ufafanuzi kuhusu Gawio la Tsh. Bilioni 153.9 lililotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kwa Serikali

IMG-20240616-WA0003.jpg

IMG-20240616-WA0003.jpg

IMG-20240616-WA0004.jpg


Pia soma: Rais Samia: Waliosema nimeuza Bandari na Bahari faida yake ndio hii
 
Nje ya mada.

Kagame aliwahi kusema akipewa port ya dar tu atakuwa #1 kwa uchumi africa
Pale kuna fwedhaaa mzee sio kitoto sema tu ndiyo vile iko mikononi mwa mamluki... Ila bandari tu kuifanya nchi kua 1# kiuchumi hapo sina uhakika ila Port ya Dar kuna pesa nyingi sana inaibiwa sana pale..
 
Pale kuna fwedhaaa mzee sio kitoto sema tu ndiyo vile iko mikononi mwa mamluki... Ila bandari tu kuifanya nchi kua 1# kiuchumi hapo sina uhakika ila Port ya Dar kuna pesa nyingi sana inaibiwa sana pale..
Kwa ka nchi kadogo kama rwanda inaweza lkn
 
Back
Top Bottom