Iddi Simba ndiye aliyeua Klabu ya Saigon | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iddi Simba ndiye aliyeua Klabu ya Saigon

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by wimbi la mbele, Aug 4, 2011.

 1. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mtu yoyote wa mjini kabla hujafanya kazi na mtu unatakiwa unamfanyia diligence sasa hao wanaopiga madili na Iddi Simba hawakujua jinsi gani alivyoiua kalbu ya Saigon?

  Kama kaweza kuia ile klabu what makes you think angekuwa na uadilifu huo?

  kama kaweza kuia Saigon angeshindwa kuiimaliza UDA?
   
 2. S

  Saracen Senior Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  duh1 JF kiboko!

  Hivi nyie humu ndani kuna mtu ambaye hamuna habari zake?
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  huyu ndo mzee wa michakato ya noti
   
 4. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu Dar siyo mwenyeji sana. Unaweza kufafanua klabu Saigon? Ilikuwa inashughulika na nini na huyu mwenye heshima zake aliiuaje?
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  hivi JK anawajibishwa vipi kwa teuzi hizi za kirafiki bila ya kujali masilahi ya utaifa wetu?
   
 6. E

  Eddie JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Idd Simba yeye na mambo ya fedha ni kama chura na maji!. Alipokuja kumfanyia kampeni Didas Masuburi pale club hoja yake kuu ilikuwa eti Masuburi atatupatia tenda za jiji watu wa mjini kumbe ana lake la UDA loo
   
 7. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Simba!umezeeka vibaya na kwa aibu sana.sifa ya ufisadi inakumengenya sana japo unajitahidi kujitetea but umekamatika.days are numbered.
   
 8. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii club iliuwa maarufu sana hapa mjini dar kwani ipo mtaa wa sikukuu na narung'ombe kwenye kituo cha big mayai enzi hizo. Hiyo club ilikuwa maarufu sana hata jk alikuwa mwanachama na usalama wa taifa kilikuwa kijiwe chao enzi za nyerere ilikuwa ni club maarufu sana. Mtu kama aden rage, jumanne masimenti, yaani simba club na yanga funs ulikuwa huwezi kuwakosa.
   
 9. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,974
  Likes Received: 6,606
  Trophy Points: 280
  sasa hivi saigon kimebaki ni kijiwe cha kunywea kahawa na kuongelea habari za simba na yanga.wakati wa kampeni wanasiasa hasa wa ccm lazima waende kugawa pale tshirt na kofia.sasa hivi imebaki story tu.ndama mtoto wa ng'ombe kafanya nini,papa msoffe kaenda wapi?shimbo kapata tillion ngapi.mia
   
 10. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  WAJAMENI NYIE WACHENI TU, IDDI SIMBA ANA KAMPUNI INAITWA SERENGETI ADVISERS, ANASHIRIKIANA NA WAMAREKANI KUNUNUA ARDHI TAKRIBANI Ha 200 000 KATIKA MIKOA YA KIGOMA NA RUKWA NA HIYO ARDHI KASHAPEWA. ANAUNGWA MKONO SAAAAAAAAAAAANA NA DC WA MPANDA WA SASA BAADA YA KUONJESHWA SAFARI YA MAREKANI YEYE PAMOJA NA MADIWANI WAKE WA MPANDA.

  MJUE PIA KUWA IDDI SIMBA SIYO MTANZANIA, HILI LINA FAHAMIKA LAKINI SERIKALI INAUMBIA MACHO.

  MIE NAPITATU WAJAMENI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  kwa hili unasikitisha sasa, kama ardhi mamlaka husika zimehamua kumuuzia na gebge lake yeye anakosa gani.

  yes Idd SIMBA sio mtanganyika lakini anaishi na kufanya ufisadi tanganyika. kama mna sheria na mnaogopa kuzitumia hizo sheria ni boramukakaa kimya ukawaacha wakina IDD simba na hawa wahindi waliosambaa kila mahali wanufaike na tanganyika huru
   
 12. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,030
  Likes Received: 8,517
  Trophy Points: 280
  hiyo saigoni ilifanya nini cha mno?
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Heri chura anaweza akabana nchi kavu kwa muda lakini Idi Simba na fedha ni kama FISADI na CCM, kuwatenga kaazi !
   
 14. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ngoma nzito....
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Iddi Simba kwanza kabisa ana matatizo ya utovu wa nidhamu na ndio maana hili la kuia UDA alishiriki kikamilifu kwa sababu hana chembe ya uchungu na UDA.

  Sisi tumezaliwa na kuishi kwa kupanda UDA na nathubutu kusema kuwa 90% ya waliokulia Dar in the 80's wanajua jinsi gani tulivyo kuwa attached na hili shirika. Kuanzia ma ICARUS na mengineyo. Lakini kwa Iddi Simba haya yote yalikuwa ni bure na hakuangalia how sensitive hii issue ya UDA itakavyokuwa na kasahau attachment ambayo sisi wana Dar tulivyokuwa na hili shirika ambalo wangesema wana float shares naamini watu wangelinunua na likawa shirika letu sote na tungeliokoa tuu kama ambavyo makampuni kama STAGE COACH na mengineyo ya nchi za nje yalivyokuwa PLC.

  Back to Saigon.

  Iddi Simba kwa hakuwa memba pale Klabuni lakini yeye akishirikiana na Khalifa Hamisi waliiingizwa klabuni lakini kumbe nia ya Simba ilikuwa ni kuifanya Saigon kuwa mali yake binafsi na kutokana na matatizo ya njaa (kama ilivyo UDA) bwana Iddi Simba alitumia nafasi yake kujijenga na allies wake mle lakini kama mjuavyo Saigon watu wakaiona ile ndipo wale wazee wa Kiswahili wakafanya mambo ambayo wansiasa wetu walishindwa kuyafanya nalo ni KUWASIMAMISHA na KUWAFUKUZA uanachama yeye Iddi Simba, Khalifa Khamisi, Yule mzee wa Bon City (jina limentoka) na jamaa wengine wawili watatu kwa UTOVU WA NIDHAMU, FITNA, UZANDIKI,UFISADI, RUSHWA, na MENGINEYO ambayo siwezi kuyaweka bayana.

  Sasa kama mnavyojua pale mtaa wa sikukuuu nafasi ilikuwa ndogo ndipo ikabidi Bakhressa atoe jengo lake ili iwe klabu kwa muda...na ile njaa ya pale kama ya UDA for some reasons ikabidi IDDI SIMBA arejee...mind you katiba ya SAIGON haimruhusu kuwa mwanachama pale na pili huo uongozi anautaka hawezi kuupata. Baadaya kurudi uchaguzi wa 2010 nao umewadia sasa ngoma ikawa ni DIDAS MASABURI na HASHIM SAGHAF ndipo hapo corrupt practises za Iddi Simba zivyojidhirisha wazi.

  Iddi Simba ambaye by the way ni MBURUNDI ( japo anadai mama yake ni MZARAMO) akapiga dili yeye na timu yake (Masaburi na yule meya wa Ilala yule dogo ) kuwa wakipewa backing na uongozi uliopo wa Saigon wao watawahakikishia kuwa tenda za soko la Feri na kukusanya kodi za parking mjini. Hivyo ule uongozi uliopo ukaamua kuwakubalia kuwa support .

  Kila mtu wa mjini anajuakuwa Saigon katika social calendar yao kila mwaka wana mambo mawili

  1. Kuwasomea Khitma marehemu

  2. Kuftarisha mwezi wa Ramadhani

  Lakini Iddi simba kwa kujua kuna mwanya wa mambo ya pesa basi huwa tesa weeee wale wazee wa Saigon na hivyo vijisenti vyake vya michango mpaka anapojua wamekosa pa kwenda ndio anatoa kiduchu na hapo ndipo na yeye huja na pre conditions kama vile achapishiwe kadi mpya ya uanachama, mafisadi wenzie wawe supported na mengineyo

  Sasa cha kujiuliza:

  Rizwani anaonekana ni mtoto wa Mjini ameshindwa vipi kuuliza profile ya Iddi Simba kabla hajadeal naye?

  Juma Kapuya ameingia vipi kwenye mtego wa Iddi Simba?

  Serengeti Advisers pamoja na elimu yote waliosheheni nayo ilikuwaje wakamuamini mtu kama Iddi Simba kuwa mmoja kati wa shauri wao ili hali wanajua he has nothing to offer on the table?

  Tumekatiwa tena umeme ...baadae ukirudi nitaendelea
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Mkuu slidingroof unayoyaongea humu kwangu ni muhimu saana
  sikujua kuwa masaburi kumbe alipewa support na saigon club na iddi simba
  mimi nilifikiri ni manji tu peke yake
  naomba umwage yote hapa pamoja na hayo usiyotaka kuya mwaga hapa...
   
 17. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  Msisahau yanga kampuni,na nani aliyeanzisha kundi la yanga kampuni.
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  yule meya wa Ilala ambaye ni swahiba wake Iddi Simba na Masaburi anaitwa Jerry Slaa

  basically, ni kuwa Iddi Simba ana wa control Meya wa manispaa tajiri kuliko zote Tanzania na pia ana mcontrol meya wa Dar, Saigon club na bila kusahau hayo madudu yake ya UDA
   
 19. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wazee ni kweli pia kuwa IDD SIMBA ndiye aliyeiuwa SUKITA?
   
 20. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Kaka Unaulizia kikoyi YEMEN?
   
Loading...