Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,954
- 30,301
KHITMA YA SAIGON CLUB YA IDDI SIMBA MSIKITI WA MTORO
Msikiti wa Mtoro kwa baadhi yetu tuliokulia Dar es Salaam unatukumbusha wengi katika wapendwa wetu ambao wametangulia mbele ya haki.
Binafsi namkumbuka mzee wangu, baba yangu na rafiki yangu Sheikh Zubeir Said Chanzi ambae yeye kakua na baba yangu toka udogo wao Mtaa wa Kipata katika miaka ya 40.
Sheikh Zubeir alikuwa habanduki Msikiti wa Mtoro toka ule wa asili uliojengwa na Sheikh Mtoro Mwinyi Mangara hadi ulipovunjwa na kujengwa mara mbili na huu ujenzi wa tatu ukajengwa na Said Salum Bakhersa ambao ndiyo msikiti huu wa fahari uliokuwapo hivi sasa.
Wengi tuna kumbukumbu za Msikiti wa Mtoro wakati wa Sheikh Kassin bin Juma akiwa Imam Mkuu katika miaka ya 1980 wakati Waislam walipitia kipindi kigumu sana na kwa bahati nzuri au mbaya Rais wa Tanzania alikuwa Sheikh Ali Hassan Mwinyi.
Huu ulikuwa wakati wa Barua za Kiuchungaji na ulikuwa pia wakati wa Mihadhara ya Biblia na ulikuwa wakati Sheikh Kassim akitoa hotuba kali za Ijumaa zilizosisimua Waislam.
Huu ulikuwa wakati hata gazeti la Chama na Serikali Uhuru na Mzalendo na Daily News zikimshambulia Mwenyekiti wa chama chenyewe na Rais wa nchi.
Haya hayakupata kutokea wakati rais Nyerere yuko madarakani.
Haya ndiyo yaliyompa nguvu Sheikh Kassim Juma kutumia membar ya Msikiti wa Mtoro kutoa majibu.
Katika moja ya khutba nyingi alizopata kutoa hii moja iliniathiri sana mimi na nimeipa jina, ''Leo Nitataja Majina.''
Sheikh Kassim Juma siku ile alianza hotuba yake kwa kusema kuwa ''nitataja majina.''
Khutba hii Sheikh Kassim alitaja majina kama matatu, Rajab Diwani, Abdul Sykes na Maalim Mohamed Matar na kila mtu akimpa sifa zake alizostahili na uhusiano wake na Mwalimu Nyerere katika historia ya uhuru wa Tanganyika ukimtoa Maalim Matar.
Sheikh Kassim alikuwa bingwa wa kuzungumza na alikuwa akijua namna ya kugusa hisia ya hadhira yake.
Siku ile alimtaja Abdul Sykes siku ya maziko yake na vipi yeye na Mwalimu Nyerere walivyoshiriki katika maziko yale.
Sheikh Kassim siku ile kwa mara ya kwanza aliueleza umma akasema, ''Huyu Abdul Sykes alikuwa mtu wake sana Nyerere.''
Nimekaa pale msikitini mengi yaliyopitika pale yakinirudia.
Kwa hakika msikiti unavutia na Sheikh Mtoro wa Mangara ikiwa Allah atamuonesha msikiti wake ulivyo sasa ataukataa atasema msikiti wake haukuwa hivi msikiti wake ulikuwa kibanda cha udongo, fito, mawe na chokaa.
Nimekaa msikitini pale nakumbuka mengi yaliyopita.
Nakumbuka Iddi Simba pale msikitini akiswali safu ya mbele na akimsikiliza Sheikh Kassim akitoa zile hotuba ambazo kabla hazikupata kutolewa.
Wako wenzake wengi waliukimbia msikiti kwa hofu.
Iddi Simba hakuondoa alikuwapo wakati wote ametulia pale mbele akimsikiliza Sheikh Kassim.
Sheikh Kassim kakamatwa kawekwa jela.
Iddi Simba hakuacha kuja kuswali Mtoro.
Iko siku nikamuuliza kwa nini yeye bado yupo Msikiti wa Mtoro hajaukimbia kama wenzake.
Jibu alilonipa ni kuwa yapo mafunzo ya kujifunza na ipo faida kwa pande zote.
Nikiwa msikitini pale nilimtazama Mzee Mwinyi na nikawa nafikiria shida alizopata wakati wa utawala wake na nilifarajika sana kwa kumuona jinsi alivyokuwa ''relaxed,'' hakika kama nahodha ambae juu ya misukosuko ya bahari alikifikisha chombo salama bandarini.
Nakumbuka wakati huu wa utawala wake baada ya kuwa anashambuliwa hata na vyombo vyake vyenyewe vya Chama na Serikali marehemu Ahmed Saleh Yahya alikuja Dar es Salaam kutoka London tukiwa tunakunywa chai, sambusa na kababu katika mgahawa mmoja katikati ya mji akaniomba kwa siri niandike makala ya kumtetea Rais Mwinyi.
Ahmed Saleh Yahya alikuwa Mhariri wa Africa Events jarida maarufu miaka ile.
Angalia picha iliyowekwa ya makala ambayo niliandika kueleza matatizo ya Tanzania katika kipindi kile.
Lakini haya yote yakapita kwa salama na leo imebakia historia.
Chembelecho Mzee Mwinyi anatuasa tuwe hadithi nzuri kusimuliwa pale tutakapoondoka duniani.
Iddi Simba ni hadithi inayopendeza katika kila sikio.
Allah akubali dua zetu ampokee mzee wetu Iddi Simba na atukutanishe pamoja nae Firdaus.