Idd Simba hukueleweka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idd Simba hukueleweka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Oct 11, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,505
  Likes Received: 5,737
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Padri Privatus Karugendo

  TUKIO la kutoeleweka kwa Bwana Iddi Simba, ambaye zamani alikuwa waziri wa serikali ya awamu ya tatu, lilijitokeza katika mkutano wa 17 wa hali ya siasa nchini, uliofanyika kwa siku mbili chini ya maandalizi na uratibu wa Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET), Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, ambako mada kadhaa ziliwasilishwa, ikiwamo ya Iddi Simba iliyohusu Sekta Binafsi, Utawala na Maendeleo.

  Kilichoibua kutoeleweka na mjadala uliokuwa na hasira na jazba nyingi, ni pale Iddi Simba, alipojitahidi kuyajibu maswali mawili ya msingi aliyoyauliza kwenye mada yake. Maswali yenyewe yalikuwa:

  “ Kwa nini wananchi wa Tanzania baada ya miaka yote hii ya utawala wetu huru, bado ni maskini pamoja na neema zote zilizopo nchini mwetu; huku wageni wakifaidika zaidi kwa kusaidiwa na watawala wetu?

  “Kwa nini wasomi na wananchi wenye hali nzuri ya kimaisha, kwa muda mrefu sana katika historia ya nchi yetu huru walidharau na hata kuogopa kuingia katika harakati za siasa?”

  Akijibu maswali haya, alijaribu kushawishi na kuonyesha kwamba tatizo kubwa la taifa letu ni udumavu wa akili. Hoja hii ndiyo iliyoibua hasira. Wasomi wengi waliokuwa kwenye ukumbi wa Nkrumah pale Chuo Kikuu, walichukulia hoja hiyo kama matusi, kudhalilishwa na hawakuvumilia.

  Wakati akijenga hoja yake ya udumavu wa akili, Iddi Simba alisema kwamba: “ Kwa mujibu wa Ripoti ya Mwisho ya Uchunguzi wa Kidemografia na Kiafya nchini Tanzania ya Mwaka 2004/2005 (Tanzania Demographic and Health Survey-2004/2005) asilimia 51 ya watoto wenye umri chini ya miaka 5 wanakabiliwa na udumavu, hususan udumavu wa akili, kutokana na sababu kadhaa zinazohusika na makuzi yao ikiwemo lishe duni”.

  Iddi Simba aliendelea kueleza kwamba kwa vile watoto wa jana ndiyo watu wazima wa leo, hivyo Tanzania kuna hatari tukawa tuna asilimia 51 ya watu waliodumaa kiakili na kwamba “ kimaumbile na kwa kuzingatia nadharia ya mtapanyo (diffusion), si kawaida kwa wenye akili za kawaida kuwaambukiza wenye akili zilizodumaa, bali kinachotokea ni wale wenye akili zilizodumaa kuwaambukiza kitabia wale wenye akili za kawaida.” Ukifuata mantiki ni kwamba mbali na ile asilimia 51 ya watu waliodumaa kiakili kuna asilimia nyingine zaidi inayoongezeka baada ya waliodumaa kuwaambukiza wenye akili nzuri.

  Maprofesa, waliishambulia hoja hii kwa nguvu zote. Kwa kusema kwamba kama hii ni kweli, basi wao wasingekuwa na uwezo wa kufundisha tena, maana kila mwaka wanaingiza chuoni wanafunzi wasiojua kitu, na mwisho wa masomo wanakuwa wameelevuka. Kwa mantiki kwamba walioerevuka wanawaambukiza wasiojua kitu.

  Ingawa sina uhakika kabisa na hoja ya kwamba lishe mbovu inaleta udumavu wa akili, sikuwa na matatizo ya kumwelewa Iddi Simba. Labda ningekuwa ni mimi ninatoa mada hiyo, ningetumia Udumavu wa Fikra, badala ya Udumavu wa Akili. Nina imani Iddi Simba hakumaanisha kutokuwa na akili za kusoma shule na kushinda mitihani. Nafikiri alimaanisha upevu wa fikra, maono, uvumbuzi na ujuzi wa kuyaweka aliyojifunza mtu kwenye matendo.

  Zaidi ya miaka 45 ya uhuru wetu, Tanzania tuna kitu gani cha kuuonyesha ulimwengu kwamba hatukudumaa kifikra? Tumevumbua nini? Tunatengeneza nini cha pekee katika viwanda vyetu? Tuna mchango gani katika dunia hii ya utandawazi? Madini yetu ya kipekee ya Tanzanite, yanaingia sokoni yakiwa na nembo ya Afrika ya kusini. Tumeshindwa kuendesha shirika letu la ndege, tumeshindwa kuendesha shirika letu la reli, tumeshindwa kuendesha viwanda vyetu na tumeshindwa kudhibiti rasilimali – kila mtu anakuja na kuchuma na kuondoka. Kwanini mtu asifikiri kumedumaa kiakili? Ni neno gani zuri? Labda tuseme tumesinyaa kifikra?

  Rais Robert Mugabe na Rais Mwai Kibaki ni wasomi wazuri, matendo yao ya kung’ang’ania madarakani ni dalili za udumavu wa fikra aliotaka kuuelezea Iddi Simba. Watu wamekufa na nchi zao zimeingia katika matatizo makubwa kwa sababu ya tamaa zao binafsi. Huu ni udumavu wa fikra. Hakuna njia nyingine ya kuelezea jambo hili. Kuna mifano mingine mingi ya viongozi wa Afrika, waliozifukarisha nchi zao kwa kuchota utajiri mwingi na kuwekeza nchi za Ulaya. Chanzo chake ni udumavu wa fikra.

  Inawezekana neno hili ni la udumavu wa akili ni baya kwa wale wanaofikiria kwamba wana akili nzuri. Lakini watu hawa watatuelezea nini juu ya wasomi wanaosaliti taaluma zao kwa sababu ya kutaka kupata utajiri wa haraka na maendeleo binafsi. Madaktari wanaokubali kuingiza dawa bandia na kuzisambaza nchi nzima wanakuwa na akili nzuri au wamedumaa kiakili? Au madaktari wanaozikimbia nchi zao maskini na kwenda kutafuta mishahara mikubwa nchi za nje wana akili nzuri?

  Mtu asiyekuwa na uzalendo, anakuwa amedumaa kifikra, vinginevyo hakuna namna nyingine ya kulielezea hili. Wataalamu wanaopitisha mikataba mibovu ambayo wanafahamu itawaathiri wao, watoto wao na vizazi vijavyo wanakuwa na akili nzuri au ni wadumavu wa akili?

  Suala si kusoma, na si kuwa profesa, daktari. Unaweza kusoma, unaweza kuwa Profesa, lakini kama huna fikra pevu na maono ya mbali, unakuwa na udumavu wa fikra. Hadi leo bado kuna mjadala mkubwa wa kutumia lugha yetu ya Kiswahili katika kufundishia. Mtu akianza kujiuliza kutumia lugha yake ama kutoitumia, kunakuwa na kasoro fulani kwenye akili yake.

  Baadhi ya Watanzania wanataka walipwe mshahara bila kufanya kazi. Ni Watanzania wangapi wanafanya kazi saa zinazotakiwa na kutambuliwa na serikali? Kila sekta kuna ugonjwa wa “Ametoka kidogo”. Na huyu mwenye ugonjwa wa kutoka kidogo na kuchelewa au kutofanya kabisa anataka alipwe mshahara mwisho wa mwezi. Je mtu huyu anakuwa na akili nzuri au ni mdumavu wa akili.

  Kwa nini taifa tajiri kama ilivyo Tanzania, tuendelee kuomba misaada kutoka nje, hadi msaada wa kujenga vyoo? Na mbona tunapopata misaada hiyo, badala ya kuendesha miradi ya maendeleo tunakimbilia kununua mashangingi na kupanda daraja la kwanza kwenye ndege? Wanaotoa misaada wanapanda daraja la kawaida kwenye ndege; lakini sisi waheshimiwa wetu ili wawe waheshimiwa ni lazima wapande daraja la kwanza kwenye ndege kwa kutumia fedha za misaada. Je huu si udumavu wa fikra?

  Wasabato masalia, ni wasomi! Lakini baadhi yao walitaka kusafiri hadi nchi za nje bila pasipoti, tiketi na visa. Waliamini kwa nguvu za Mungu, wangeweza kusafiri na kuongea lugha ngeni bila kujifunza. Kama huu si udumavu wa akili ni kitu gani? Lakini pia na wale wote wanaoamini kwamba mkate unaweza kugeuka kuwa mwili na divai kugeuka kuwa damu ya Yesu, au kupona malaria bila kutumia dawa, kutibu ukimwi kwa miujiza, wana matatizo yale yale ya udumavu wa akili. Tunaweza kutofautiana kwa maelezo, lakini hatimaye hoja ya Iddi Simba, ni ile ile ya kuwataka Watanzania kujikomboa kifikra.

  Ni lazima tuwe na fikra pevu na maono; ni lazima kuijenga Tanzania yetu na ya vizazi vijavyo; mbali na ukweli huu ni kukubali bila aibu kwamba tuna ugonjwa wa kudumaa kifikra.
   
 2. s

  shabanimzungu Senior Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iddi simba should know...nyerere nationalized al the industries,,and now we see the result.......
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na Mwinyi na wafuasi wake wakaja wakavigawa bure kwa Makaburu, Wahindi na Wazungu, and now we see the result.... no?
   
 4. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani hilo linapingana vipi na hoja yake kwamba tumedumaa akili? Si amesema ni udumavu wa akili ndio umesababisha hizo results?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hili litakuwa jibu la wiki! classic!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mnaona sasa! wasomi mnaanza tena kutafuta mchawi.. Nilisema kwamba NDIVYO TULIVYO, siku zote ni lazima awepo mchawi..
  Kifupi maneno ya Simba yamegonga katikati ya msalaba. Ndivyo Tulivyo imetokana na Akili kudumaa
  Matokeo yake, sisi sote ni Malimbukeni ama kwa lugha fupi na ya kigeni tunaitwa - Wonna be!..Hata mimi Mkandara kuna mambo mengi tu nimo ktk kundi la Wonna be yaani Limbukeni anayeiga ili kupata maendeleo na sii kukabiri matatizo yanayonirudisha nyuma ili tupata maendeleo.
   
 7. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Idi Simba was 100% right....ni hoja inayohitaji kufanyiwa kazi, ni kweli tumedumaa au mfumo wetu wa kiuchumi, kisiasa na jamii vimetudumaza.....raisi wa nchi anapoona maendeleo yanakuja kwa kwenda kuomba ulaya na marekani, kupigia watu magoti watupe misaada....bajeti tegemezi....
  tumlaumu nani?? CCM??? katika nchi ambayo ni tajiri wa ardhi, madini, bahari, maziwa, mito, milima,mbuga za wanyama....watu...tuwe maskini???
  ni sawa na mtu awe anaishi kijijini awe na mifugo,shamba lenye maji halafu aje mjini kuwa ombaomba.....unaweza kumchapa viboko.......nchi tajiri zinatakiwa zituchape viboko ili kutuamsha....
  na wasomi wasiwe wajinga wakiamini kwamba kumfundisha mtu ndio kumuondolea kule kudumaa kwake.....kwanza hata elimu yenyewe imedumaa....
   
 8. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kudumaa akili au ni wajanja?

  Kama ambavyo watu kutoka nje wanaingia nchini kwetu wanaona opportunity nje nje wanajizolea utajiri, ndio hivyo hivyo watanzania wajanja walioziona huko Namibia, Marekani na kwinginepo kwamba kunalipa na wako huko wanajinufaisha. Hao siwezi kuwaita wamedumaa kiakili bali ni wajanja.

  Mishahara ya wafanyakazi wa serikali hapa ni midogo sana. Mfanyakazi akikaa ofisini kwake kwa dhati siku nzima hadi mwisho wa mwezi, familia itakula mawe. Taka usitake, kamshahara hakifikishi nusu mwezi. Kwa sababu hiyo basi, kama akili imedumaa utakaa hadi mwisho wa mwezi ule mawe. Kwa wajanja wa bongo, hawakubali. Wao huweka koti kwenye kiti kisha hutoka kidogo kwa ajili ya mishemishe za kutafuta ugali. Mimi hao nawaona wajanja na akili zao ziko shapu sana.

  Waheshimiwa waliokabidhiwa madaraka ya nchi hii wana akili sana. Wanajua haki zao na wanajua jinsi ya kuwanyima wengine haki zao. Wakiamua kuingia mikataba feki, wanafanya wakijua fika kuwa wanawaibia wananchi ili kujinufaisha wenyewe. Hata kama manufaa yenyewe ni kidogo kiasi gani. Yote hii ni kwa sababu aidha ya ulafi, kutaka zaidi na zaidi au kutokuwa na uhakika na mambo ya mbeleni baada ya kuachia madaraka.

  Zamani viongozi wenye madaraka walifika muda wao wa kustaaafu wakajikuta hawana future. Wa sasa wamejifunza kurekebisha hiyo hali, wanataka wakistaafu wawe na maisha mazuri. Kama serikali haikuwawekea hayo, inabidi wajitengenezee wenyewe aidha kwa kuchukua rushwa, kuingia mikataba feki au kutumia loop hole nyingine yoyote iliyo ndani ya uwezo wao. Hawa ni wajanja na akili zao zinachaji, wala hazijadumaa.

  Raslimali zetu zimeuzwa sijui ndio ubinafsishaji? Wajanja wamechangamkia tenda kuhakikisha wanaweka maslahi binafsi mbele. Wanajipatia chao cha juu bila kujali ni kidogo kiasi gani ukilinganisha na kinachochukuliwa na anaowapa tenda. Mradi lengo lake la kutia kitu mfukoni mwake litimie.

  Na mambo mengine kadha wa kadha yenye mwelekeo huo. Na jamii inasemaje mambo kama hayo yanapotokea? Angalia watu hawa wawili: kiongozi (nyerere type) versus kiongozi (mkapa type). Jamii inasemaje? Utasikia wanambeza the nyerere type, kwamba alikuwa mtu mkubwa serikalini lakini ona sasa hali yake! The mkapa type watamsifia na kusema jamaa shapu sana amefanya vitu vyake.

  Jamii ndiyo inayolea jamii. Mtu katika jamii hukua na yale jamii yake inayoamini. Unachoita udumavu wa akili ni mtazamo wa jamii gani? Hii jamii ina fikra, mtazamo na dira gani? Hivi vinatoka wapi? Tunaye kiongozi anayeweza kuvipanda au kuendeleza vizuri tunavyotaka?
   
 9. t

  tk JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hawa ma Professor wetu kweli wamedumaa kiakili na wala si kifikra. Hivi kweli watawezaje kuamini kuwa nchi kama Tanzania yenye kila rasilimali uijuayo duniani bado ni maskini wa kutupa kama si kudumaa kiakili kwa watu wake?

  Wao ma Professor wanadhani kuwa na akili ni kutoa changamoto za kitaalamu ambazo hazizai matunda yeyote ya kiuchumi kwa nchi na wananchi wake. Professor Mkandara, kwamfano, tangu aingie Chuo Kikuu kafanya nini cha maana. Migomo tu kila siku, weakati wao wanamchango na nafasi kubwa kuishauri Serikali kuchukua hatua madhubiti za kitaalamu kuinua hali ya nchi. Wao hawafanyi hivyo.

  Wanasiasa wetu nao wameelemea zaidi katika kupata umaarufu hata katika kufanya hivyo wanaathiri uchumi wa nchi. Mfano, hivi leo nchi inatatizo la umeme kwa upungufu wa megawati 75 wakati resources za kuzalisha megawati 100 zipo hapa hapa nchini. Wadumavu wa akili wako tayari nchi iathirike kiuchumi ili tu kulinda hadhi yao wasionekane kuwa walikosea.

  Nadhani wakati umefika tukubali kuwa hili ni tatizo na tutafute njia ya kulitatua badala ya kumshambulia Iddi Simba.

  Hongera Iddi Simba kwa ushupavu wa kuzungumza ukweli ingawa unauma.
   
 10. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Tuko wengi sana hapa nchini tunaona wazi kabisa kwamba hali si shwari. Napenda nikuhakikishie hata wanaoziongoza hizo sekta mbalimbali wanajua kabisa kwamba hali si shwari. Kila mtu anaimba nchi tajiri nchi ina utajiri. Hakuna asiyelijua wala kuliona hilo. Sio maprofesa tu, ukiwataja majina wako kwa mamilioni. Nakataa kuwa sio kudumaa kwa akili. Tujiulize zaidi. Ni kwa nini tunajua na tunaongea kila siku habari za matatizo ya nchi hii, potential areas za nchi hii lakini hakuna cha tofauti kinachofanyika?

  Nakataa tena, nchi ina watu wajanja na waelewa mno; wenye akili kupindukia. Hakuna tatizo la kudumaa akili. Kuna sababu nyingine ya matatizo yetu.
   
 11. K

  Koba JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...bora Mwinyi alibinafsisha hivyo viwanda kama TBL ambavyo vilikuwa ni mzigo kwa walipa kodi na havizalishi chochote lakini makaburu sasa wanalipa billions kama kodi,je mlivyokataa kubinafsisha(kugawa bure) kama TANESCO vina faida gani zaidi ya kuongeza migawo na kuongeza umaskini kwa Taifa na huyo Simba naye asituletee upupu wake aende akagawe vibali vya sukari na siasa zake za kibaguzi AKA uzawa maana ndicho anachoweza tuu!
   
 12. t

  tk JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ambayo ni ipi?
   
 13. t

  tk JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Loo! Mbona umekuwa mkali!! bado swali lipo pale pale tatizo letu Watanzania ni nini?? Tusilaumu makundi machache. Kwani hao viongozi si sisi ndio tunawaweka madarakani. Kama hawafai kwanini tunawachagua? Huo sio udumavu wa akili?
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ni ukweli usiopingika kuwa utawala mbovu ndio unaotufanya tuwe na akili zilizodumaa. Mpaka leo hii Mkulu wetu hajagundua kuwa huko kuomba omba misaada toka nchi za nje sio kunatudhalilisha wadanganyika tu bali ndio kumeipeleka nchi yetu kutokuwa na maendeleo!! Wale mliokaribu na mkulu chonde chonde mnaposafiri nae huko majuu mnunulieni kitabu kimoja kilichoandikwa na binti mmoja Mzambia kiitwacho "DEAD AID BY DAMBISA MOYO" pengine kinaweza kutusaidia kumuelimisha mkulu wetu madhara ya kupitisha bakuli kwa nchi zilizoendelea na athari zake kwa nchi kama yetu!! Kusoma kitabu hiki pia kutamsaidia mkulu wetu kupumzika nyumbani!!
   
 15. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  wanaochangia umaskini wa nchi hii ni bila kusahau taasisi kama PRIDE ambazo maskini wengi WAMENYANG'ANYWA MPAKA VITANDA VYA KULALIA NA VYANDARUA VYA KUJIKINGA NA MALARIA!
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Apr 25, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280


  Wakubwa wote hapo juu, kwanza tuangalie hii hoja ya Idd Simba kuwa tumedumaa kiakili, unajua swala la ukweli huwa haliondolewi kwa hasira na matusi kama walivyofanya hao maprofessor
  1. Je dalili za kudumaa akili ni zaipi na tunawezaje kuzijua?
  2. Nini kulichotufanya tudumae kiakili? asili, wakoloni, elimu n.k
  3. Kama tukihakikisha tuna udumavu wa akili then jtujikwamue vipi
  4. Kama jibu ni siyo, then what makes us poor, political systems? geographical position? history? foreign countries? etc

  Tukijibu maswali kwa kisiasa na kuangalia akina Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, tutakuwa tunatafuta machwi kama alivyosema Mkandara, maana maendeleo haya si TANZANIA WE ALSO NEED TO REFER nchi zingine za kiafrika ambazo ni maskini, !!!! what is the problem??  Naomba mthibitishe huo udumavu wa akili na mlinganishe ni kwa vipi same mtanzania anaweza kwenda ulaya , akasoma , akafaulu vizuri na akafanya kazi ulaya na hata kuwa expert? what makes udumavu wa akili ku-apply hapa?
   
Loading...