Idd Ninga: Wewe ni nani (shairi)

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,405
1>nauliza wewe nani,na kwangu
wataka nini.
Uniambie kwanini,kwangu waja fanya
nini.
Ili nijue kwanini,kwangu umefata nini.
Niambie wewe nani,wewe janga
duniani.
2>umeingia nyumbani,nyumbani
ulimwenguni.
Umo leo duniani,watutia mashakani.
Mambo yako kishetani,mungu
ashayalaani.
Niambie wewe nani,wewe janga
duniani.
3>umeisahau dini,umeuleta udini.
Utawatia motoni,wale watokuamini.
Ila walo naimani,wataingia peponi.
Niambie wewe nani,wewe janga
duniani.
4>umetuweka vitani,ulikuwa mkoloni.
Na leo upo jikoni,nasi tupo
mashakani.
Itapofika jioni,utalia kilioni.
Niambie wewe nani,wewe janga
duniani.
5>mbinu zako za sirini,zishatoka
hadharani.
Hadi watu mitaani,wahisi wewe
shetani.
Leo twakupa ilani,mwisho wako
karibuni.
Niambie wewe nani,wewe janga
duniani.
Shairi=WEWE NI NANI.
Mtunzi=Iddy Ninga wa Tengeru
Arusha.
0655519736
 
Back
Top Bottom