Idadi ya walipa kodi yapungua

Idadi ya walipa kodi yapungua

Hawapendi Kulipa Kodi

WARUDISHE KODI YA KICHWA

Idadi ya walipa kodi ni tofauti na wale wanaokwepa kutoa au kuchukua risiti.

Idadi ya walipa kodi ni kodi ile direct kutoka ktk mishahara, Corp tax n.k siyo ya indirect tax ambayo kila mmoja analipa.

Kuwa na idadi kubwa ya walipa kodi ya mapato kupitia direct tax ni fungu muhimu maana hakuna jinsi ya kukwepa.

Indirect ni fungu la ziada siyo muhimu la uhakika kama direct tax

Na pia kodi zetu zitukime vizuri siyo kufanya watawala waishi kifahari na magari makubwa kwa kodi zetu
 
Sisi sio Wajinga bhana.

Juzi tu nimetoka kulioa 2200 VAT kupitia wakaka luku, Halafu Jinga moja limeshiba Allowance linataka kusema sisi ambao hatukadiliwi mapato na TRA hatulipi kodi...

STUPID
Bado mkuu , wanaolipa direct tax ndio muhimu kuliko hiyo 2000 yako
 
N
WARUDISHE KODI YA KICHWA

Idadi ya walipa kodi ni tofauti na wale wanaokwepa kutoa au kuchukua risiti.

Idadi ya walipa kodi ni kodi ile direct kutoka ktk mishahara, Corp tax n.k siyo ya indirect tax ambayo kila mmoja analipa.

Kuwa na idadi kubwa ya walipa kodi ya mapato kupitia direct tax ni fungu muhimu maana hakuna jinsi ya kukwepa.

Indirect ni fungu la ziada siyo muhimu la uhakika kama direct tax
Nikweli mkuu
 
IMG_0361.jpg

Rais Dk. John Pombe Magufuli, akiwa katika Kikao Maalum kati yake na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ameeleza kuwa, Tanzania haifanyi vizuri katika suala la ukusanyaji wa mapato kulinganisha na Nchi nyingine za kiafrika.
Alieleza kwa kufafanua takwimu za kodi kwa kulinganisha Tanzania dhidi ya majirani zake:
  • Tanzania (milioni 55): walipa kodi milioni 2.2; kodi inayotozwa ni 12% ya GDP.
  • Kenya (milioni 46): walipa kodi milioni 3.9; kodi inayotozwa ni 18% ya GDP.
  • Uganda (milioni 37): walipa kodi milioni 1.2; kodi inayotozwa ni 14% ya GDP.
  • South Africa (milioni 56): walipa kodi milioni 19.9; kodi ni 26% ya GDP.
  • Mozambique (milioni 5.3): walipa kodi milioni 5.3; kodi ni 18% ya GDP.
  • Zambia (milioni 16): walipa kodi milioni ?; kodi ni 15% ya GDP.
  • Botswana (milioni 2): walipa kodi milioni 0.7; kodi 14% ya GDP.
  • Burundi (milioni 10): walipa kodi milioni 0.2; kodi 13% ya GDP.
  • Namibia (milioni 2): walipa kodi milioni 0.6; kodi 12% ya GDP.
Hapa Rais Magufuli amepigilia msumari kwenye ukweli. Watanzania wamekuwa wakilalamika kuwa, kodi ni nyingi na kwamba Sera za sasa siyo rafiki kwa mazingira ya kibiashara na uwekezaji nchini. Sasa ukweli umewekwa wazi kuwa, Tanzania ndiyo Nchi yenye wastani mdogo sana wa walipa kodi katika Nchi zote za Afrika Mashariki.
Vilevile, mapato yatokanayo na kodi nchini Tanzania, ni asilimia ndogo sana kulinganisha na Nchi majirani. Tanzania imepigwa na Kenya, Uganda, Zambia, Msumbiji, Rwanda, Burundi, SA, Botswana na Namibia katika asilimia ya Mapato yatokanayo na kodi (kiwango cha kodi kulinganisha na uwiano wa pato la Taifa).

Sasa wewe fikiria, kama Serikali ya sasa imejitahidi kuziba mianya ya kodi na kuongeza walipa kodi lakini bado Tanzania iko nyuma kulinganisha na majirani zake, je kipindi cha kabla ya Magufuli, hali nchini ilikuwaje?

Tatizo liko kwa Watanzania wenyewe. Sera za ovyo za kuwarahisishia maisha watu wavivu ndizo zilizotufikisha hapa. Tuliifanya Tanzania masikini kuwa Nchi inayotegemea consumer goods na kujisahaulisha misingi ya kiuchumi. Leo bado tuko nyuma kwenye kodi but tunalialia, sasa hali ikifika ya kuifanya kodi kuchangia asilimia 15% itakuwaje.

Tuaje uvivu, majirani walikuwa wanatuchora sana kipindi cha nyuma namna tulivyokuwa tunapotea. Sasa hivi tunaifanya Tanzania kuwa Nchi ya kuzalisha bidhaa zetu na siyo kupokea kila kitu kutoka nje.

Rais Magufuli amewakumbusha Watanzania kuwa: Hapa duniani, mambo ya uhakika ni mawili pekee: kifo na kukusanya kodi
 
Idadi ya walipa kodi nchini imeshuka kutoka watu 3,336,777 kwa mwaka 2021/2022 hadi watu 2,282,048.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kongamano la kodi na uwekezaji.

Je, unadhani nini kimechangia hali hii?

Je, wewe binafsi unalipa kodi yako na kuhimiza wengine kulipa kwa ajili ya kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo nchini?

Haya wale walio seme hii nchi inaweza kujitegemea wanyooshe mkono juu. Kiufupi tuna safari refu sana kuweza kujitegemea. Kama tupo milion 65 afu waliosajiliwa TRA ni milion mbili 🤣

Lakini wanatuambia makusanyo yameongezeka maradufu? Hivi tunatumia njia za kishirikina au kiuchumi?
 
Kuna kazi ya kufanya kama taifa asee. Nchi yenye walipakodi wachache ina maana kuwa hata biashara kubwa ni chache na shughuli rasmi nichache pia. Idadi kubwa tunaganga njaa
 
Idadi ya walipa kodi nchini imeshuka kutoka watu 3,336,777 kwa mwaka 2021/2022 hadi watu 2,282,048.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kongamano la kodi na uwekezaji.

TOKA MAKTABA :
06 September 2023

Ni walipa kodi 4,696,99 tu wamesajiliwa kati ya mil. 33

Hadi kufikia Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.
tra-2pic-1024x576.webp

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Ameir Abdallah Ameir, aliyetaka kujua ni asilimia ngapi ya wafanyabiashara hawajaingizwa katika mfumo rasmi wa kodi na Serikali inachukua hatua gani kuwafikia.

“Hadi Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.
 
Gazeti la kila siku la serikali :

WALIPA KODI 4,696,999 WAMESAJILIWA TRA,

6 Sept 2023 — “Hadi Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia.....
1744743385579.jpeg

DODOMA; SERIKALI imesema hadi kufikia Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi(BLW), Ameir Abdallah Ameir, aliyetaka kujua ni asilimia ngapi ya wafanyabiashara hawajaingizwa katika mfumo rasmi wa kodi na Serikali inachukua hatua gani kuwafikia.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Naibu Waziri Kigahe amesema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kupanua wigo wa kodi.
1744743501791.jpeg

“Hadi Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.

“Idadi ndogo ya usajili wa walipakodi, ikilinganishwa na fursa ya nguvu kazi iliyopo inatokana na sehemu kubwa ya shughuli za kiuchumi hapa nchini kuendeshwa na sekta isiyo rasmi inayokadiriwa kuajiri takribrani watu milioni 27.7.

“Mheshimiwa Spika, hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kurasimisha sekta isiyo rasmi ni pamoja na kampeni ya mlango kwa mlango inayolenga kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara wasiotambulika, kutenga na kujenga maeneo maalumu ya masoko kwa wafanyabiashara wadogo na kuendelea kutoa elimu na ufafanuzi wa kina kwa wananchi kuhusu masuala ya kodi, ili kuhamasisha wananchi kurasimisha biashara na shughuli za kiuchumi kwa hiari,” amesema Naibu Waziri Kigahe

Walipa kodi 4696999 wamesajiliwa na TRA.
Source: Habari Leo
 
Kodi inayoongelewa hapa ni direct tax na sio indirect tax
Direct na indirect tax , ina maana gani wakati zote zinaingia mfuko mkuu wa serikali? Huu ni utapeli wa maneno tu , huwezi sema walipa kodi wanapungua ili hali kila mwananchi analipa kodi kwa njia moja au nyingine .

Kama TRA haiwezi kuja na majibu muhim katika hili basi kuna shida ,kwamba kwao walipa kodi ni wakina Mo n.k ila mwananchi wa chini sio mlipa kodi ,huu upumbavu ukome
 
TOKA MAKTABA :
06 September 2023

Ni walipa kodi 4,696,99 tu wamesajiliwa kati ya mil. 33

Hadi kufikia Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.
tra-2pic-1024x576.webp

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Ameir Abdallah Ameir, aliyetaka kujua ni asilimia ngapi ya wafanyabiashara hawajaingizwa katika mfumo rasmi wa kodi na Serikali inachukua hatua gani kuwafikia.

“Hadi Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.
Nakumbuka mkuu
 
Direct na indirect tax , ina maana gani wakati zote zinaingia mfuko mkuu wa serikali? Huu ni utapeli wa maneno tu , huwezi sema walipa kodi wanapungua ili hali kila mwananchi analipa kodi kwa njia moja au nyingine .

Kama TRA haiwezi kuja na majibu muhim katika hili basi kuna shida ,kwamba kwao walipa kodi ni wakina Mo n.k ila mwananchi wa chini sio mlipa kodi ,huu upumbavu ukome
Kodi gani unayolipa wewe mkuu, au kwa siku unanunua vitu vya tsh ngapi kulipa kodi. Kwa ufupi kama nchi ins walipa kodi wachache ina maana kuwa wananchi hawazalishi au hawana kazi rasmi kinachoongelewa hapa ni direct tax , sio kodi ya tsh 1 unayotoa ukinunua kiberiti huko kwenu
 
Biashara ya umachinga imerahisishwa sana,kuna walipa kodi wakubwa wamejificha kwenye machinga hususani Kariakoo
 
Back
Top Bottom