Idadi ya walipa kodi yapungua

Idadi ya walipa kodi yapungua

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
5,582
Reaction score
10,112
Idadi ya walipa kodi nchini imeshuka kutoka watu 3,336,777 kwa mwaka 2021/2022 hadi watu 2,282,048.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kongamano la kodi na uwekezaji.

Je, unadhani nini kimechangia hali hii?

Je, wewe binafsi unalipa kodi yako na kuhimiza wengine kulipa kwa ajili ya kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo nchini?

Haya wale walio seme hii nchi inaweza kujitegemea wanyooshe mkono juu. Kiufupi tuna safari refu sana kuweza kujitegemea. Kama tupo milion 65 afu waliosajiliwa TRA ni milion mbili 🤣

Screenshot 2025-04-15 201904.png
 
Tuambie maoni yako nasi tutayasoma kwenye #AzamNews ifikapo saa 2:00

Haya wale walio seme hii nchi inaweza kujitegemea wanyooshe mkono juu. Kiufupi tuna safari refu sana kuweza kujitegemea. Kama tupo milion 65 afu waliosajiliwa TRA ni milion mbili 🤣
Hawa viongozi wetu wanatufanya sote ni mapoyoyo ujue!

Enhe, principle za uanzishwaji wa kodi ya VAT ilikuwa ni nini?

Kuwaita raia wote kuwa ni walipa kodi wa nchi hii lengo lake ni nini?

Ni hatua gani za kisheria zilizokwisha chukuliwa kwa waliokwepa kodi halali za Serikali?
 
3,336,777 kwa mwaka 2021/2022 hadi watu 2,282,048.

Hatari sana tumepoteza walipa kodi 1,000,000.

Asilimia kubwa sana, serikali itoke na kutuambia nini kimetokea.

Nchi haijakumbwa na vita kubwa ya kupoteza nguvu kazi wala hakuna gonjwa kubwa la kufuta 33% ya nguvukazi walio walipa kodi iwe binadamu au kampuni.

Haya mambo yanatakiwa yajadiliwe kwa kina ni makosa ya takwimu zilizokusanywa sensa ya walipa kodi au serikali ilitaka kujimwambafai ina idadi kubwa ya walipa kodi.
 
Idadi ya walipa kodi nchini imeshuka kutoka watu 3,336,777 kwa mwaka 2021/2022 hadi watu 2,282,048.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kongamano la kodi na uwekezaji.

Je, unadhani nini kimechangia hali hii?

Je, wewe binafsi unalipa kodi yako na kuhimiza wengine kulipa kwa ajili ya kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo nchini?

Haya wale walio seme hii nchi inaweza kujitegemea wanyooshe mkono juu. Kiufupi tuna safari refu sana kuweza kujitegemea. Kama tupo milion 65 afu waliosajiliwa TRA ni milion mbili 🤣

Acheni kutupanga hivi nchi hii kuna mtu alipi kodi, hivi miamala kwenye sim , malipo kwenye luku , maushuru mbalimbali ikiwemo maegesho ya magari sio kodi

Kwa nini mnataka fanya watz wajinga sana ,pumbavu
 
Acheni kutupanga hivi nchi hii kuna mtu alipi kodi, hivi miamala kwenye sim , malipo kwenye luku , maushuru mbalimbali ikiwemo maegesho ya magari sio kodi

Kwa nini mnataka fanya watz wajinga sana ,pumnavu
Yaani 30% ya walipa kodi wametoweka kwenye thin air ila TRA kasifiwa kukusanya zaidi ya trilioni 2 kwa mwezi.

Na kati ya hao 3.3m, nadhani 500k ni wazee wa paye, hivyo waliobaki kulipa kodi ni kama 1.8m

Itoshe kusema "anaupiga mwingi, mitano tena"
 
Wewe hulipi kodi mkuu. Kama hujakadiriwa na TRA huwezi kujihesabu kama mlipa kodi
Huu ndo upuuzi sasa tunalisha watu, mfanyakazi kila mwezi analipa kodi je lini TRA imemkadiria , so mfanyakazi wa tz sio mlipa kodi kwa sababu hajakadiriwa na TRA ?
Nijibu kabla sijakufuata na fimbo jirani ,nakueshim
 
Hii inaonesha awamu ya sita imekuwa biashara nyingi sana sababu ya sera zake za hovyo na kijinga.kodi inazidi mtaji wa biashara unategemea mwenye biashara ataendelea?
 
Yaani 30% ya walipa kodi wametoweka kwenye thin air ila TRA kasifiwa kukusanya zaidi ya trilioni 2 kwa mwezi.

Na kati ya hao 3.3m, nadhani 500k ni wazee wa paye, hivyo waliobaki kulipa kodi ni kama 1.8m

Itoshe kusema "anaupiga mwingi, mitano tena"
Mkuu ikikupendeza ebu fafanua vizuri, sijaelewa mkuu wangu
 
Sema hii hainishangazi maana kuna kipindi wife wangu alienda TRA wakamkadiria kodi kubwa tofauti na mauzo na faida anayopata. Alivyolalamika sana jamaa wa TRA akamwambia kama unaona unaonewa funga biashara yako. Hapo bado hujakutana na purukushani za service levy,leseni ya biashara,mchango wa taka na mlinzi, kodi ya pango n.k.
Biashara iliyumba ikabidi aifunge tu. Jamaa wa TRA hawana huruma kabisa.
 
Kupungua kwa idadi ya walipa kodi nchini kunaweza kuhusishwa na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na :

  1. kuzorota kwa uchumi,
  2. mabadiliko ya sheria na sera za kodi, na
  3. mabadiliko ya idadi ya watu.
Janga la COVID-19, kwa mfano, liliathiri kwa kiasi kikubwa mapato ya kodi duniani kote, kwani kufunga nchi kitu ambacho Magufuli hakufanya karantini yoyote, na vikwazo vya kiuchumi vilisababisha kupungua kwa shughuli za kiuchumi na misamaha (tax holiday) ya kodi.

Hata hivyo, kwa muda mrefu, mambo kama vile kukwepa kodi, na mabadiliko katika soko la ajira mfano kuwa na taifa lenye bodaboda, wachuuzi, wategemezi walio watu umri zaidi ya miaka 18+ wahitimu wa vyuo (shule za upili na msingi) bila ajira au kwenda VETA wengi badala ya ajira rasmi viwandani n.k yanaweza pia kuchangia mabadiliko katika idadi wa walipa kodi.

Hata tunahitaji mchumi kama Dr. Dr. Philip Isidori Nzabhayanga Mpango, Dr. Mwigulu Lameck Nchemba watoe kauli kwa kina nini kimejiri Tanzania badala ya hotuba
 
Halafu unaambiwa TRA inavunja record kwa mapato kila mwezi toka mwaka uanze.

Dr Mpango ni mkweli mno mpaka wameamua kumpumzisha.
 
NO REFORMS NO ELECTION ndiyo jibu la kupata viongozi na watunga sera wenye maono ya kuhusu uchumi, ajira, masoko badala ya hawa waliopo wizarani na bungeni

09 April 2025
Mbamba Bay, Nyasa
Tanzania

HOTUBA YA NISHATI YA MAKAA YA MAWE ILIYOMLETEA MATATIZO TUNDU LISSU

View: https://m.youtube.com/watch?v=TdCkjaIH2rU
Tundu lissu amehutubia wananchi wa mji wa Mbambabay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Hotuba ambayo ameirudia tena Mbinga mjini kuhusu madini mkakati kwa uanzishaji viwanda vikubwa vya kimkakati kuzalisha nishati, bidhaa na maelfu ya ajira kama pia serikali ikiamua makaa ya nayo yatumike nchini Tanzania mbali ya kuuza makaa nje ya nchi.

TOKA MAKTABA :
18 February 2025

Mradi wa Uchimbaji Chuma cha Liganga Mchuchuma pamoja na Mlima mdogo wa Maganga Matitu

View: https://m.youtube.com/watch?v=XOTIBat2sjo
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, leo tarehe 18.02.2025 ameendelea na ziara yake ya kikazi Wilayani Ludewa Mkoani Njombe na kufika kwenye Mradi mkubwa na wa Kielelezo wa Chuma cha Liganga pamoja na Mlima mdogo wa Maganga Matitu inayosimamiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)Waziri Jafo amesema mMadi huu unaweza kuanza mwaka huu 2025 kwani wataalum wa NDC kwa niaba ya Serikali pamoja na wawakilishi wa Mwekezaji wanakamilisha vipengele vya kimkataba ili Mradi huo uweze kuanza.

TOKA MAKTABA :

16 December 2024

Biteko - Tanzania kuendelea kuchimba, kuuza makaa ya mawe.

View: https://m.youtube.com/watch?v=l387nMlRQ0E

Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuchimba na kufanya biashara ya makaa ya mawe kutokana faida za kiuchumi kwa taifa hilo, licha ya bidhaa hiyo kuhusishwa na uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Baadhi ya mataifa barani Ulaya yanaachana na matumizi ya makaa ya mawe hususani katika kuzalisha umeme.Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati, Doto Biteko katika mahojiano maalumu na mwandishi wa BBC Florian Kaijage.

Ambapo miongoni mwa mambo mengine aliyoyazungumzia ni pamoja usambazaji wa gesi majumbani, bei ya mafuta ya petroli na dizeli, kuwepo kwa umeme wa kutosha na masuala ya uongozi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom