Idadi ya nondo katika floor ya ghorofa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idadi ya nondo katika floor ya ghorofa

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Memory, Jun 29, 2011.

 1. M

  Memory Senior Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Naomba nifahamu ghorofa standard yenye urefu wa mita 20 na upana wa mita 10 inahitaji nondo za aina ngapi na kwa idadi ipi ili kukamilisha ile level ya kwanza tu bila kuhusisha zile zilizoko katika foundation na beam. Hapa nataka nifahamu idadi ya nondo kwa kila 10 or 20square meters ya 1st, 2nd....n floors.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwanii usiwasiliane na wakandarasi mbali mbali ili kulinganisha ujuzi?
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  Heshima mbele mkuu,
  Majibu ya humu huwa yanafaida kwa wengi sio kwa muulizaji tu
  kuna watu wako mbali na nyumbani(Tanzania) na hawana uwezo wa kuwaona hao makandarasi na wana plan ya kujenga maghorofa mara wafikapo nyumbani,
  kama unajua weka wazi tu ili watu wakokotoe gharama
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kuna tatizo gani ukiwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki walioko nyumbani ili wakutafutie hizo dataz.
   
 5. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakutahadharisha tena nakuomba sana, ujenzi wa ghorofa (gorofa) maswala ya nondo mwachie Engineer si suala la kukisikia au kuulizia mitaani au kwa fundi mzoefu. Nasema hakuna kitu kama hicho, utakuja juta baadae!! Mahesabu ya nondo yanafanywa kwa utaalamu (calculations) kutumia fomula sio kukisia, ukubwa wa eneo/unene wa zege (floor thickness), matumizi ya jengo na pia ratio (vipimo) vya zege. "Foundation" ndio inabeba kila kilicho juu ya ghorofa, kwa hiyo huwezi kubadili juu bila kurekebisha chini au kujua chini kuna uwezo gani.
  * Tuache njia za mkato, mme sahau mara hii kilichotokea Changombe/Kariakoo/Kisutu na kwengineko?
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  kwani humu hakuna engineerz?
   
 7. M

  Memory Senior Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kila point hapa ni muhimu katika kufanya maamuzi, lakini pia tusisahau kuwa hapa kuna wahandisi wazuri tu ambao wanaweza kutupatia rough estimations ili unapowasililiana na watu wa mbali bado utakuwa na picha ya vitu kadha wa kadha. Tuendelee kuelimishana.
   
 8. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani kupata jibu kwa data hizo tu, inategemea na design ya jengo, aina na concrete mix, hizo nondo zitapangwa vipi etc.

  Pia unasema ghorofa ya n hauwezi kufanya hesabu kihivyo, construction ya ghrorofa ya n iko effected na ghorofa zilizo juu yake na probably chini yake as well. Kwa kifupi zidhani kama unaweza kupata jibu la maana bila kuconsider design nzima.
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  Heshima Mbele mkuu Kang,
  Haya hapa chini ni maelezo muhimu ya jamaa

  "Naomba nifahamu ghorofa standard yenye urefu wa mita 20 na upana wa mita 10 inahitaji nondo za aina ngapi na kwa idadi ipi ili kukamilisha ile level ya kwanza tu bila kuhusisha zile zilizoko katika foundation na beam. Hapa nataka nifahamu idadi ya nondo kwa kila 10 or 20square meters ya 1st, 2nd....n floors."
   
 10. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wapo lakini mkuu kuna taaluma zingine zinahitaji face2face consultations, sio rahisi kuomba ushauri wa daktari unapohitaji upasuaji ni lazima daktari afanye mwenyewe. Mgonjwa huwezi chukua kisu ukapasua tumbo. Kadhalika masuala ya nondo kwenye jengo la ghorofa ni mambo ya calculation si ya makisio kama vile unavyofikiria. Kwa maana ingine ni taaluma ya kulipia, ndio maana lazima Engineer uwe legally registered/licensed ili ukiboronga uwajibishwe.
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kinacho determine idadi na aina/ubora wa ndondo sio ukubwa wa eneo peke yake. Designer atatakiwa kujua pia aina ya mzigo inayokusudiwa kubebwa na hiyo floor (dead and live loads) na location zake. Kwa kifupi ni vigumu mno kwa engineer yoyote kuja hapa kusema ni idadi fulani ya nondo utahitaji unless afanye assumption ya hizo factors zote nyingine.
   
 12. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye Green ndipo pa muhimu, assumption zikiwa kumi mtu atajua pa kuanzia
   
 13. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Best option ....chukua ramani zako muone QUALIFIED ENGINEER atakueleza kila utakacho taka kujua. Maelezo utakayopewa hapa sikushauri kuyapokea.
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
 15. M

  Memory Senior Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Shule tosha kabisa, lakini hawa wajasilimiamali wa kibongo pia hawako serious maana kuna jamaa aliniambia ana mtaalam nikampatia design toa Italy lakini mpaka leo sioni. Lakini nimepata data za kuanzia. Ahsanteni.
   
 16. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Mkuu Urefu wa mita 20 ni average ya ghorafa 5 hadi 6. Mkuu haya mambo hayahitaji blaa blaa. Tafuta Architect akuchoree kwanza kutokana na mahitaji yako then Structural Engineer atamaliza kazi yako

  Structural Engineer atakusaidia kujua utakuwa na slabs za unene upi na saizi ya nondo na idadi yake pamoja na kiasi gani utatumia kwenye slab yako. Atakusaidia kujua utaweka beams za saizi ipi kama ni 230*450mm, 230*500, 230*600 nk pamoja na idadi na saizi ya nondo, atakusaidi kujua pia utatumia nguzo(columns) za saizi ipi na nondo za saizi ipi na idadi yako, njia hizo hizo atatumia kwenye ngazi, vitako(pads) nk.
  Hayo yote yanahitaji mahesabu wala hamna longo longo, yote haya yanafanyika baada ya architect kuchora michoro yake yenye mpangilio wa vyumba, elevations zake na sections pia.
   
 17. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Jaribu nondo mbili halafu tupe jibu...tujifunze toka kwako mkuu itakuwa poa au laah!! Ma injinia wa kariakoo wakiwa kazini kuangalia idadi ya nondo zao hadi raha..sasa kazi hakuna na mtu kachukua tena tayari ya ukandarasi hadi raha....usishangae kuona magorofa ya kko yana ufa kama michoro ya wasanii au ramani ya mito.

  from what i think kama unataka kujenga gorofa, idadi ya nondo inaendana na vitu vingi sana... Best luck mkuu
   
 18. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nondo sio lazima

  Unaweza kutumia njia kama hii inayotumika makoko Nigeria  teh teh teh
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hili halihitaji longolongo sana! Mfuate architect na structural eng's wakusaidie vizuri. Kama uko dar au unaifahamu dar vizuri, jaribu kuchunguza magorofa tofauti tofauti kwa umakini kuhusu matumizi yake, halafu jiulize swali lako barabara.
   
 20. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wingi na ukubwa wa nondo hutegemea aina ya Zege, ubora wake na unene wake.

  Wanasema ni heri uzidishe Zege kuliko kuzidisha nondo. Jengo lililozidiwa uzito na limejengwa na nondo dhaifu, huwa linaanza kupata mipasuko na hiyo kuwajulisha wakazi kuwa janga linakuja. Jengo lililojengwa na Zege dhaifu na nondo nyingi, hatari yake ni kuwa kuvunjika bila kutowa tahadhari (ghafla).

  Kabla hujajua aina ya nondo, kwanza unaangalia upana/urefu wa hizo sakafu zenyewe. Hapo unaanza kupanga zege ya ubora gani itumike. Ukishapata aina ya zege, ndiyo unakuja sasa kupiga mahesabu unene wa nondo, ubora wake, aina na idadi yake. Kumbuka nondo nyingi kwenye jengo ni hatari sana na utakuja kuuwa watu bure.

  Zege imara linasababisha ukubwa wa nondo kupungua. Kama una Zege imara kwa mfano lenye glass fibres, huweki nondo. Naungana na wale waliokupa onyo kuwa usijijengee ghorofa bila wataalamu kulipitia. Nasikitika sana kwa hali iliyopo sasa Tanzania kuwa mtu anajijengea tu jengo lake bila usimamizi wowote imara kutoka kwa wataalamu. Kama waipenda familia yako, sikiliza maonyo ya hao jamaa juu.
   
Loading...