Idadi ya nondo katika floor ya ghorofa

Hii ni proffesion yangu kwa kifupi maelezo yako hayajitoshelezi hata kdogo kama walivyoshauri wengne hapo juu step 1 tafuta architect mzuri atakupa floor plans,elevations,section hata 3d ukitaka ili uione gorofa yako then tutafute maengineer tutakupa idadi ya nondo na sizes za element mbalimbali,tatu nenda kwa quantity surveyor atakupa gharama ya mradi wako wote,
 
Ukienda kwa architect ni vizuri ukawa na ufahamu wa unataka nini na ustick to ur nd kwa mfano unakuta mteja anataka hotel later akijenga anabadilika anasema anataka maduka na ofices hichi kitu hakitakuwa safe kwa sababu design loads tofauti,so try to have a ful picture of wat u want at least for the next 50 years,
 
If u want a safe,durable and beautiful building especially storey building be ready to pay this people
1. Architect
2.Structural engineer
3.Electrical engineer
4.Mechanical enginer
5.Quantity surveyor
6.Good Contractor
with this people in ur project u can sleep and dont expect failure.kama kuna nliesahau u can add,
 
Mkuu unafahamu Architect & Structural Eng yeyote unayemjua utupatie contact zake?







Mkuu Urefu wa mita 20 ni average ya ghorafa 5 hadi 6. Mkuu haya mambo hayahitaji blaa blaa. Tafuta Architect akuchoree kwanza kutokana na mahitaji yako then Structural Engineer atamaliza kazi yako

Structural Engineer atakusaidia kujua utakuwa na slabs za unene upi na saizi ya nondo na idadi yake pamoja na kiasi gani utatumia kwenye slab yako. Atakusaidia kujua utaweka beams za saizi ipi kama ni 230*450mm, 230*500, 230*600 nk pamoja na idadi na saizi ya nondo, atakusaidi kujua pia utatumia nguzo(columns) za saizi ipi na nondo za saizi ipi na idadi yako, njia hizo hizo atatumia kwenye ngazi, vitako(pads) nk.
Hayo yote yanahitaji mahesabu wala hamna longo longo, yote haya yanafanyika baada ya architect kuchora michoro yake yenye mpangilio wa vyumba, elevations zake na sections pia.
Kwa ushauri 0719 021 693
 
Well said Mamzalendo...tuheshimu taaluma za watu walizosotea miaka vyuoni...sioni sababu ya kuomba ushauri hewa online ilihali kuna wataalamu ambao wanafanya design katika view ya economy,beauty na stability! So far as sheria na taratibu za bodi zinavyoelekeza...si jukumu la client kuamua whether mradi wake uwe na nondo za size gani ama kwa idadi gani kwa maana kuna wataalamu ambao muunganiko wao utaleta ufanisi na kuepuka hasara na repair zisizokua na ulazima..
 
Mkuu, asisahau wahusika wa kudesign mabomba ya maji safi na maji machafu (Sanitary) ingawa hapa Architect anaweza kusaidia kwa jengo dogo. Pia kwa kuchukua dunia ya sasa ilivyo, yawepo mabomba na sockets za kupitisha waya za simu, Internet na Home Theatre. Pia waya za TV/Satelite nazo ni muhimu zikapitishwa kabisa ukutani na si miwaya imejaa kwenye sakafu kila sehemu.
If u want a safe,durable and beautiful building especially storey building be ready to pay this people
1. Architect
2.Structural engineer
3.Electrical engineer
4.Mechanical enginer
5.Quantity surveyor
6.Good Contractor
with this people in ur project u can sleep and dont expect failure.kama kuna nliesahau u can add,
 
Sidhani kama utampata mtu kama huyu. Sanasana atakuwa ni Architect au Mhandisi mwenye ofisi na hapo kaajiri watu/mtu mwenye ujuzi tofauti na yeye. Ni masomo ambayo yanafundishwa tofauti kabisa na hata Tanzania, kuna Chuo cha Ardhi ndiyo wanafundisha Architect na elements za Ujenzi na UDSM wanafundisha Ujenzi na elements za Architect.

Kwa majengo hadi ghorofa nne kama sikosei, huwa si lazima sana kuwe na Structural Eng. kwani haya majengo kwa matumizi ya kawaida, hayahitaji kufanyiwa mahesabu zaidi ya uzoefu. Ila kila sehemu yenye uzito usio wa kaiwaida na kama kukiwepo mitetemo mikubwa basi nenda kwa Struct. Engineer aanze kuingiza nguvu za mitetemo ambazo huwa ni hatari sanasana kwa majengo.

Watu wengi wanafahamu kuwa hatari kubwa ipo katikati ya jengo floor/beam wakati ukweli ni kuwa hatari kubwa sana ipo sehemu hizo floor zinaungana na ukuta/beam. Hapo huwa kuna shear stress ambazo ni hatari sana. Nilishawahi kuona kwenye Discovery, ajali ya jengo huko Korea, kisa ni kuwa kwenye floor katikati, kulikuwa na nguzo, na hawakuweka Zege imara na nondo imara na ile nguzo, IKAITOBOA floor na jengo zima likaanguka na watu wengi walikufa.

Mkuu unafahamu Architect & Structural Eng yeyote unayemjua utupatie contact zake?
 
Mkuu Foundation, nishukuru kwa kuwa wazi na msaada kwa jamaa hapo juu. Kama sikosei ni mtu upo siku zote kwenye hii professional.

Nina swali moja kwako: Hivi Tanzania kuna kiwanda cha kutengeneza Pre-Cast Conrete Slab? Hizi zingelisaidia sana watu kama hawa kwani zinakuwa ni rahisi kuzifunga na linakuja gari la Zege na kumaliza kazi. Zipo za aina nyingi na just in case sijaeleweka, ngoja niweke picha hapa chini. Kama kuna mtu anafahamu kuwepo kwa kiwanda kinachotengeneza hizi slab, basi atujulishe.


http://www.structuremag.org/images/0908-en-1.gif

http://www.homebuilding.co.uk/files/ascent-homebuilding/images/0605floors_free.jpg

http://www.ebawe.de/img/bilder-ganze-breite/elementdecken01.jpg
Mimi ni Structural Engineer, Architect yupo, namba yake ni 0713 509 509, 0784 509 509. Huyu ndugu ni Architect mzuri sana. Namba zangu ni 0719 021 693, 0788 869 580

Ushauri mbadala.

Kama nyumba ni ya kuishi na ni ghorofa moja, unaweza ukachanganya nondo na matofali{matofali yatatumika kubeba mzigo(load bearing walls)} na itakusaidia kupunguza idadi ya nondo na size ya nguzo, beams na vitako. Ujenzi wa namna huu unaitwa non framed structure.

Ukitaka usijenge bila kutumia matofali{hapa matofali yatatumika kama partition nk}, lazima utumie nondo nyingi na sizes ya nguzo, beams na vitako itakuwa kubwa. Ujenzi wa namna hiyo unaitwa framed structure. Na ni mzuri sana, very durable
 
Kujenga ghorofa lazima upate building permit.

Building permit haitoki mpaka ulete michoro ya architects na utaje engineers.

Na uweke bango kwenye site, linalosema nani kachora, nani anajenga, na kibali namba ngapi.

Hata hivyo, ni red tape ya bure, nyumba ya ghorofa kibali cha nini, majuu wanajenga na mbao, bila zege, bila nondo. Mbona hazianguki?
.
 
Mkuu Foundation, nishukuru kwa kuwa wazi na msaada kwa jamaa hapo juu. Kama sikosei ni mtu upo siku zote kwenye hii professional.

Nina swali moja kwako: Hivi Tanzania kuna kiwanda cha kutengeneza Pre-Cast Conrete Slab? Hizi zingelisaidia sana watu kama hawa kwani zinakuwa ni rahisi kuzifunga na linakuja gari la Zege na kumaliza kazi. Zipo za aina nyingi na just in case sijaeleweka, ngoja niweke picha hapa chini. Kama kuna mtu anafahamu kuwepo kwa kiwanda kinachotengeneza hizi slab, basi atujulishe.


http://www.structuremag.org/images/0908-en-1.gif

http://www.homebuilding.co.uk/files/ascent-homebuilding/images/0605floors_free.jpg

http://www.ebawe.de/img/bilder-ganze-breite/elementdecken01.jpg

Mkuu sijasikia kama kiwanda cha namna hiyo, Hizo slab iwe slab ya kawaida au Wafle slab au flat slab wanatengeneza hapo hapo site, hii process inaitwa CAST IN SITU. Ubaya wa Pre cast slab inalala tu kwenye beams au ukuta kwa hiyo slab inakuwa non monolithic na beams au ukuta ( bond inakuwa hakuna).
 
Back
Top Bottom