ICC siyo suluhisho

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wana bodi,

Ni vyema kuona kwamba walio wengi wameisha vuka kigingi cha uchaguzi na kwa ambao hawaja vuka, ni muhimu kufanya tathmini na kutambua kwamba tofauti ya kura milioni kumi kati ya Mhe Tundu Lissu na Rais Magufuli ni kubwa sana. Lazima utaelewa kwamba Rais Magufuli alichaguliwa na watanzania walio wengi.

Tunayo yashuhudia sasa hivi ni pamoja na kundi la watu lisilo kubaliana na matokeo ya uchaguzi kupeleka malalamiko ICC. Malalamiko hayo yana ihusisha serikali ya Tanzania na ukiukwaji wa haki za binadamu na upotefu wa demokrasia kwenye uchaguzi.

Wanacho shindwa kutambua ni kwamba kwa miaka mingi, ICC wame onekana kuwa wababe na kama watu wanao penda sana kuingilia masuala ya nchi zingine haswa za Afrika. ICC iliundwa ili kuingilia kati kwenye nchi ambazo mahakama zimeshindwa ku tekeleza wajibu wake. Vile vile umuhimu wa ICC unatambulika zaidi kwenye ku hukumu watu walio hujumu nchi kwa njia moja au nyingine na mahakama za nchini kwao sio imara kiasi cha kuwa wezesha watu hao kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria. Kwa mfano: Mtu maarufu sana, au mtu mwenye wadhifa wa juu.

Sidhani kama Tanzania kuna ukiukwaji wa haki za binadamu wa namna hio au udikteka ulio kithiri ila labda yapo yanayoweza kufanywa ili kuhakikisha kwamba kosa ni kosa kwa wote na haki ina dumu katika mahakama yetu.

Wanao wahi ku peleka malalamiko ICC watakuwa wana amini kwamba kesi hizo haziwezi kusikilizwa nchini na hukumu ya haki kutolewa au wana amini kwamba mahakama zetu zitawa pendelea wana CCM. Kurekebisha mahakama na kuwa na njia rasmi ya kupinga matokeo ya uchaguzi nchini ndio njia inayofaa kutatua migogoro kama hii.
 
Migambo wanaruka na kukanyagana...mijitu masikini alafu unawaletea kiburi wazungu...kuna rafiki yangu Mnigeria aliniambia kwanza Mungu anayefuata Mzungu
 
Sifa kubwa ya dhulma humnyima amani na raha aliye dhulumu. Mateso haya ni sehemu ya adhabu za awali .
Ndio maana mwizi aweza kuua ili afiche wizi wake.
Usione hivi kwenye public watu washamaliza dawa hawapati usingizi

Unasemaaaaaa
ICC vipi?
 
Vipi yale majeshi mliyoyakodi kutoka Burundi na kuvalishwa sare za polisi wa Tz wamesharudishwa kwao au bado wanamlinda waliyemsaidia kuiba kura na kuuwa watu?
 
Ingelikuwa kura zimefanyika kwa haki na ukweli tusingekuwa na tatizi. Lakini wizi umekuwa wakushitusha. Wapinzani kunyang'anywa majimbo ya uwazi kabisa inashangaza. lazima tuwe na walakin. Hata kama baadae wataingia bungeni, sio kwa kuwa wameridhia lakini itakuwa kwa kuendeleza upinzani na kuamini kuwa wananchi pia wana maisha na waendelee kuishi. Ila wizi uliotokea mwaka huu , hata kipofu ameona.
 
Back
Top Bottom