Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 53,197
- 132,337
Kabla ya uislamu waarabu nao walikuwa wanafuata imani za mababu zao za kama kuabudu masanamu,na ndio maana huwa inasemwa ulitumika upanga kueneza huo uislamu kwa sababu watu walikuwa hawataki kuacha imani za mababu zao na kuachia dini ya muhammad kuenea na kuondoa imani zao za asili.
Leo hii uislamu unaonekana ndio imani asili ya waarabu na hatuoni waarabu kulalamika uislamu kuwa umeondoa imani asili za mababu zao,na hii sio kwa uislamu na waarabu tu bali hata ukristo na jamii zengine kama wazungu nao walikuwa na imani zao hapo kabla ila ajabu waafrika tu ndio tunalilia imani za mababu zetu na kuona hatufanikiwi kisa tumeacha imani za mababu.
IBADA YA KWELI KWA MUAFRIKA NI TAMBIKO TU.
Tambiko ni ibada yenye asili ya Afrika.Katika tambiko muombaji hufikisha haja yake kwa mungu kupitia sadaka za kuchinja,kuteketeza mali na mengineyo.
Kwakua imani zote zimejenga dhana kwamba mungu ni wa kuogopwa na kuheshimika sana pasi kuruhusu mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Mungu na binadamu,wamewekwa wajumbe wa kuyapokea na kuwasilisha maombi kwa Mungu.
Tambiko katika muktadha huu pia limeweka mjumbe anayeitwa Mzimu kama daraja la mawasiliano kati ya Mungu na binadamu.
MZIMU NI NANI?
Mzimu ni mtu aliyekufa. kwenye ukoo au familia ambaye jamii husika inaamini katika uhai wake aliishi maisha ya kumpendeza Mungu.Kinyume cha mzimu ni Kizuka.
Kwakua inaaminika mtu mwema anapokufa hukaa kwa Mungu ndivyo ndani ya tambiko inaaminika hivyo.Hivyo ni sahihi kuomba kupitia mzimu ili maombi yafikishwe kwa Mungu.
Hivyo ,kuna tofauti ndogo kati ya Mzimu na mtakatifu anayetajwa kwenye ukatoliki.Tofauti yenyewe ni mchakato unafanya huyu aitwe mtakatifu na huyu mwingine Mzimu.Ingawa wote wawili wanafanana katika msingi wa maisha yao kabla ya kufa.
Ndio maana ndani ya ukatoliki kuna watakatifu wengi kama mizimu ilivyokua mingi.
Kwakua Yesu na Mohamed ni bindamu waliokufa katika dhana iliyoelezwa hapo juu ya kuzingatia maisha maisha yao enzi za uhai hawa ni mizimu
Historia kama maarifa Yesu na Mohmed ni wanaharakati waliokua wakifanya harakati zao huko mashariki ya kati karibu na mito Euphrates na Tigris ambapo inaaminika harakati hizi ndizo zilizozaa mtazamo wa kiimani uliopo sasa.
NINI KILITOKEA ?
Kwanza tukubaliane ujio wa ukoloni Afrika hakua na nia njema kwa muafrika mwenyewe.Kama hivyo sawa basi yote yalionzishwa ,kukuzwa na kuimarishwa nao hayawezi kuwa mazuri ikiwamo na dini.
Wakati ule wanafika Afrika kwa lengo la kutunyonya wakakutana na Tambiko.Kwakua ibada hiyo na imani nyingine za kiafrika hazikutoa nafasi ya kutimiza lengo lao,wakaamua kuliua Tambiko .Hvyo wakaanzisha Propaganda Tambiko ni uchawi na ushenzi.
Kwenye Tambiko sadaka hapewi mtu mmoja kama ni chakula kinaliwa na wote walioshiriki ama wote kuacha.Kama wangeacha Tambiko liendelee wangeshindwa timiza lengo lao la unyonyaji kupitia dini.
Hivyo wakaleta ibada ambazo mtu mmoja mwenye afya tele,nguvu na akili anapokea sadaka yote na kuzila au kuzitumia kwa niaba ya Mungu.
NINI MADHARA YA WAAFRIKA KULITUPA TAMBIKO.
Enzi za Tambiko kulikua na utaratibu uliowekwa kwa wote wanaotakiwa kishiriki kwenye ibada hiyo.Baadhi ya jamii watu waliofanya ngono kabla ya ndoa ,wezi,ambao wana ugomvi na wengine hawakuruhusiwa.
Hivyo si tu ilipunguza mmonyoko wa maadili lakini pia magonjwa kama ukimwi,kisonono na mengine hayakuwepo licha ya kutokuwapo kinga kama kondomu.
Na kwakua yalikua maombi stahiki kwa muafrika sehemu kubwa ya maaombi hayo yalijibiwa na Mungu.
Waafrika walipoomba mvua walipata,walipoomba mavuno walipata.Sasa hivi haiwezekani kuomba mvua na ikanyesha kwa sababu mizimu tunayoiomba si ya Keri ni ya warabu na wazungu.Ndio maana warabu na wazungu wanafanikiwa sana kuliko sisi wa Afrika kutokana na usahihi wa kuitumia mizimu yao.
JE TURUDI KWENYE TAMBIKO?
Ndio ,tukirudi kwenye misingi ya Uafrika wetu kizazi chetu kitabaki salama kwenye maeneo mengine yote.
Kama tutairudisha imani yetu basi pia tutapata namna yetu ya kuwapata viongozi wetu kupitia demokrasia yetu wenyewe ambayo haitafanya tuchinjane kama hii.
Tukirudi kwenye tambiko basi tupata namna ya kiimani ya kuendesha mambo yetu pasipo kufuata principles na kanuni za kimgharibi.
Kwakua imani ni tiba ya mambo yote mara tukaporudisha Tambiko Afrika tutagundua pia utajiri wa Taifa la Tanzania ukiupima kwenye kanuni za wazungu hutouona.
Wao wanapima shughuli zifanyazwo na wananchi wanakwepa kwa makusudi kujumlisha milima,madini,,tembo nk kwa sababi wana hakika mtawaamini kama mkishawaamini hata katika namna ya kuabudu.
Noel Nguzo.R.
20/1/2019
Uko sahihi.hakuna dini iliyoumbwa,kilichoumbwa ni kuabudu.Kilichofanyika kwetu nikuletewa namna mpya yakuabudu katika mfumo wa dini.Ila jambo ni lile lile la kuabudu kitu tusichokiona ila kupitia imani tunaamini.Tatizo letu watu weusi tunaamini sana mapokeo kuliko kutaka kujua tulikotoka.Walichotushinda wenzetu nikuweka kumbukumbu ya ustaarabu wao tofauti na sisi ambao ustaarabu wetu haukutunzwa popote kiasi ambacho ilikua ni rahisi kuuona ni ushenzi nakuutupilia mbali.
Sana Mkuu,unashangaa mbona watu zamani walikuwa wanaomba mvua na hapohapo mvua haichelewi inawanyeshea hadi wao,siku hizi unaomba mpaka unapauka na hakuna lolote,alafu tunawaona wale ndio wajinga kumbe mazuzu ni Sisi!Nimekuelewa vyema na huo ndio ukweli kuhusu dini zilizoletwa kuna mengi ya kushangaza/ukifikiria
Wewe uliona yesu akipaa na kufufua watu? Umeambiwa au umesoma katika vitabu vilivyoandikwa ukaviita vitakatifu/umekuwa ulipo kwa kufuata mkumbo wa baba yako ambae nae alifuata mkumbo wa babu yako wa dini elekezikuna babu yetu yeyote mwenye historia ya kufanya mambo aliyoyafanya yesu
kupaa
kufufua watu
kutembea juu ya maji
kulisha watu elfu 5
nk,nk.nk
Kwanza tumepoteza muda Sana,kila sehem Wana Dini Yao,wahindi,waarabu,wazungu waafrika Pia Kwa nini usikomae na Dini zako unaenda kwenye Dini za kigiriki huelewi hata kinaongelewa niniWewe uliona yesu akipaa na kufufua watu? Umeambiwa au umesoma katika vitabu vilivyoandikwa ukaviita vitakatifu/umekuwa ulipo kwa kufuata mkumbo wa baba yako ambae nae alifuata mkumbo wa babu yako wa dini elekezi
Wanalazimisha kusema vitabu vitakatifu je wao wamevipata wapi? Ukweli viliandikwa tu na wajanja hao duniani dini hapana wala Mungu akuleta dini naaminiSana Mkuu,unashangaa mbona watu zamani walikuwa wanaomba mvua na hapohapo mvua haichelewi inawanyeshea hadi wao,siku hizi unaomba mpaka unapauka na hakuna lolote,alafu tunawaona wale ndio wajinga kumbe mazuzu ni Sisi!
Sent using Jamii Forums mobile app
Gospel ya zamani inasema salvation comes from within you,sio kujipanga kwenye ma benchi nk,wewe ndio Dini pekee sio mbele ya mtuWanalazimisha kusema vitabu vitakatifu je wao wamevipata wapi? Ukweli viliandikwa tu na wajanja hao duniani dini hapana wala Mungu akuleta dini naamini
Wajapan wana dini yao wa korea ...kuna mataifa kibao sio wakristo wala waislamu ...hao wanaosambaza dini wanaua watoto wadogo palestine, wanatubagua kwa rangi etcKwanza tumepoteza muda Sana,kila sehem Wana Dini Yao,wahindi,waarabu,wazungu waafrika Pia Kwa nini usikomae na Dini zako unaenda kwenye Dini za kigiriki huelewi hata kinaongelewa nini
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mi now ni mwendo wa mizimu kwenda mbele,Kama itanidhulu Acha inidhulu maana mi mi product Yao,so hakuna shida huku kungine wastage of timeWajapan wana dini yao wa korea ...kuna mataifa kibao sio wakristo wala waislamu ...hao wanaosambaza dini wanaua watoto wadogo palestine, wanatubagua kwa rangi etc
Mkuu mimi nilijitoa kwenye mkumbo tangu nilipojitambua now ninaishi kwa kuongea na mungu mimi kama mimiMkuu mi now ni mwendo wa mizimu kwenda mbele,Kama itanidhulu Acha inidhulu maana mi mi product Yao,so hakuna shida huku kungine wastage of time
Sent using Jamii Forums mobile app
Bora wewe ulishtuka mapema mkuuMkuu mimi nilijitoa kwenye mkumbo tangu nilipojitambua now ninaishi kwa kuongea na mungu mimi kama mimi