Adui wa muafrika ni muafrika mwenyewe

Adui wa muafrika ni muafrika mwenyewe

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
985
Reaction score
2,370
Kila siku tumekuwa tukitafuta mchawi wa umaskini wa Afrika. Tunalaumu ukoloni, tunalaumu Marekani, tunalaumu Ulaya. Lakini ukweli mchungu unaouma zaidi ni kwamba: Hakuna adui wa nje anayeweza kumuangamiza Mwafrika bila kumtumia Mwafrika mwenzake mwenye tamaa!

Ubinafsi na roho ya "Mimi na tumbo langu" si tu kwamba umetufanya masikini, bali unamwaga damu za ndugu zetu kila siku.

Vijana wa Congo wanachukua silaha na kukubali kulipwa fedha kidogo na wafanyabiashara wa madini ili kwenda kuwaua, kuwabaka, na kuwafukuza Wacongo wenzao kwenye ardhi yao. Wako tayari kumwaga damu za wenzao kwa ajili ya bahasha ya dola chache!

Wanasiasa wanatumia maelfu ya dola kuiba kura, kuvuruga uchaguzi, na kuingiza nchi kwenye machafuko... SI kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, bali ili kulinda matumbo yao, familia zao, na akaunti zao za benki.

Majaji na mahakama zinapokea rushwa ili kuwasafisha wauaji, wafanyabiashara wa dawa za kulevya, na mafisadi wakubwa, huku maskini asiye na pesa akiozea jela kwa kuiba kuku.

Injinia anachukua asilimia 10 ya rushwa na kufumba macho wakati barabara, madaraja, na majengo yakijengwa chini ya kiwango. Miezi michache baadaye jengo linaporomoka na kuua raia wasio na hatia kwa sababu tu mtu mmoja alitaka kununua gari la kifahari!
Ukweli mchungu usiotaka kusikilizwa ni huu: Hakuna Mzungu, Mchina, wala Mmarekani anayekuja Afrika kumlazimisha Mwafrika kumdhulumu au kumpiga risasi Mwafrika mwenzake.

Mkoloni haji hospitalini kuiba dawa za wagonjwa ni muuguzi au daktari wa Kiafrika.

Balozi wa kigeni haingii kwenye chumba cha kura kuvuruga matokeo ni raia na viongozi wa Kiafrika.

Wafanyabiashara wa Magharibi hawaji kuweka saini kwenye miradi ya barabara za hovyo ni mainjinia wetu wenyewe wanaopokea bahasha chini ya meza!

Kila mara tunapokimbilia kulaumu ukoloni, historia, au mataifa ya nje, tunawapa kisingizio cha bure waovu waliopo miongoni mwetu. Afrika haitabadilishwa na misaada ya Ulaya wala na rais mpya; itabadilishwa siku tutakapoacha kutumia umaskini kama halali ya kuwa wabinafsi. Change haianzii Ikulu inianzia pale unapokataa kupokea au kutoa rushwa kwenye nafasi yako.
 
Ni kweli Waafrika tunasafari ndefu sana.
 
Back
Top Bottom