njundelekajo
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 310
- 227
IBADA YA KWELI KWA MUAFRIKA NI TAMBIKO TU.
Tambiko ni ibada yenye asili ya Afrika.Katika tambiko muombaji hufikisha haja yake kwa mungu kupitia sadaka za kuchinja,kuteketeza mali na mengineyo.
Kwakua imani zote zimejenga dhana kwamba mungu ni wa kuogopwa na kuheshimika sana pasi kuruhusu mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Mungu na binadamu,wamewekwa wajumbe wa kuyapokea na kuwasilisha maombi kwa Mungu.
Tambiko katika muktadha huu pia limeweka mjumbe anayeitwa Mzimu kama daraja la mawasiliano kati ya Mungu na binadamu.
MZIMU NI NANI?
Mzimu ni mtu aliyekufa. kwenye ukoo au familia ambaye jamii husika inaamini katika uhai wake aliishi maisha ya kumpendeza Mungu.Kinyume cha mzimu ni Kizuka.
Kwakua inaaminika mtu mwema anapokufa hukaa kwa Mungu ndivyo ndani ya tambiko inaaminika hivyo.Hivyo ni sahihi kuomba kupitia mzimu ili maombi yafikishwe kwa Mungu.
Hivyo ,kuna tofauti ndogo kati ya Mzimu na mtakatifu anayetajwa kwenye ukatoliki.Tofauti yenyewe ni mchakato unafanya huyu aitwe mtakatifu na huyu mwingine Mzimu.Ingawa wote wawili wanafanana katika msingi wa maisha yao kabla ya kufa.
Ndio maana ndani ya ukatoliki kuna watakatifu wengi kama mizimu ilivyokua mingi.
Kwakua Yesu na Mohamed ni bindamu waliokufa katika dhana iliyoelezwa hapo juu ya kuzingatia maisha maisha yao enzi za uhai hawa ni mizimu
Historia kama maarifa Yesu na Mohmed ni wanaharakati waliokua wakifanya harakati zao huko mashariki ya kati karibu na mito Euphrates na Tigris ambapo inaaminika harakati hizi ndizo zilizozaa mtazamo wa kiimani uliopo sasa.
NINI KILITOKEA ?
Kwanza tukubaliane ujio wa ukoloni Afrika hakua na nia njema kwa muafrika mwenyewe.Kama hivyo sawa basi yote yalionzishwa ,kukuzwa na kuimarishwa nao hayawezi kuwa mazuri ikiwamo na dini.
Wakati ule wanafika Afrika kwa lengo la kutunyonya wakakutana na Tambiko.Kwakua ibada hiyo na imani nyingine za kiafrika hazikutoa nafasi ya kutimiza lengo lao,wakaamua kuliua Tambiko .Hvyo wakaanzisha Propaganda Tambiko ni uchawi na ushenzi.
Kwenye Tambiko sadaka hapewi mtu mmoja kama ni chakula kinaliwa na wote walioshiriki ama wote kuacha.Kama wangeacha Tambiko liendelee wangeshindwa timiza lengo lao la unyonyaji kupitia dini.
Hivyo wakaleta ibada ambazo mtu mmoja mwenye afya tele,nguvu na akili anapokea sadaka yote na kuzila au kuzitumia kwa niaba ya Mungu.
NINI MADHARA YA WAAFRIKA KULITUPA TAMBIKO.
Enzi za Tambiko kulikua na utaratibu uliowekwa kwa wote wanaotakiwa kishiriki kwenye ibada hiyo.Baadhi ya jamii watu waliofanya ngono kabla ya ndoa ,wezi,ambao wana ugomvi na wengine hawakuruhusiwa.
Hivyo si tu ilipunguza mmonyoko wa maadili lakini pia magonjwa kama ukimwi,kisonono na mengine hayakuwepo licha ya kutokuwapo kinga kama kondomu.
Na kwakua yalikua maombi stahiki kwa muafrika sehemu kubwa ya maaombi hayo yalijibiwa na Mungu.
Waafrika walipoomba mvua walipata,walipoomba mavuno walipata.Sasa hivi haiwezekani kuomba mvua na ikanyesha kwa sababu mizimu tunayoiomba si ya Keri ni ya warabu na wazungu.Ndio maana warabu na wazungu wanafanikiwa sana kuliko sisi wa Afrika kutokana na usahihi wa kuitumia mizimu yao.
JE TURUDI KWENYE TAMBIKO?
Ndio ,tukirudi kwenye misingi ya Uafrika wetu kizazi chetu kitabaki salama kwenye maeneo mengine yote.
Kama tutairudisha imani yetu basi pia tutapata namna yetu ya kuwapata viongozi wetu kupitia demokrasia yetu wenyewe ambayo haitafanya tuchinjane kama hii.
Tukirudi kwenye tambiko basi tupata namna ya kiimani ya kuendesha mambo yetu pasipo kufuata principles na kanuni za kimgharibi.
Kwakua imani ni tiba ya mambo yote mara tukaporudisha Tambiko Afrika tutagundua pia utajiri wa Taifa la Tanzania ukiupima kwenye kanuni za wazungu hutouona.
Wao wanapima shughuli zifanyazwo na wananchi wanakwepa kwa makusudi kujumlisha milima,madini,,tembo nk kwa sababi wana hakika mtawaamini kama mkishawaamini hata katika namna ya kuabudu.
Noel Nguzo.R.
20/1/2019