Ibada ya kweli kwa Muafrika ni tambiko

Ibada ya kweli kwa Muafrika ni tambiko

Ni vyema ukaja na mfumo kamili na Ustaarabu uliofindishwa kupitia Tambiko

Uislam
ulikuja na kukuta watu wakiabudu Masanamu waliyoyachonga wao kwa mikono yao,ukayaondoa yote
ulikuta ustaarabu mbaya wa unyanyasaji hususan kwa wanawake,ukaondoa uovu huo
Kisha ukatoa elimu,na vitabu vikaandikwa,kuwa hili ni Halali na hili ni Haraam
Kwakuwa mwanaadam ukimpa uhuru moja kwa moja,ni zaidi ya mnyama.
Tukafunzwa kuwa tusitende dhambi,kwani Mola hapendi dhambi
tukaaswa,tufanye mema,kwani Mola anawapenda wafanyao mema

Narudi kwako mkuu

IMANI YAKO YA TAMBIKO,inatufunza nini?!
na je,kuna Vitabu kutoka kwa Mola vilivyoshushwa kwa ajili ya kueneza ushirikina huo?!

HAKIKA YA SHIRKI,NI DHULMA KUBWA MNO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo Ilikuwa njia fyongo ya kumtafuta Mungu.

Bibilia Imekuja kuwaelekeza kwenye Tambiko halisi Kwa Mungu aliyehai sio maiti za mababu zao, na mashetani.

'' Kwa Maana Jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee ili kila amuaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele'' Yohana 3:16.

Kuendelea kukumbatia Giza wakati mwanga upo, ni ujinga.
Kwa miaka na miaka Mungu aliacha watu wamuabudu kupitia njia fyongo kama unavyoita?
 
IBADA YA KWELI KWA MUAFRIKA NI TAMBIKO TU.

Tambiko ni ibada yenye asili ya Afrika.Katika tambiko muombaji hufikisha haja yake kwa mungu kupitia sadaka za kuchinja,kuteketeza mali na mengineyo.

Kwakua imani zote zimejenga dhana kwamba mungu ni wa kuogopwa na kuheshimika sana pasi kuruhusu mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Mungu na binadamu,wamewekwa wajumbe wa kuyapokea na kuwasilisha maombi kwa Mungu.

Tambiko katika muktadha huu pia limeweka mjumbe anayeitwa Mzimu kama daraja la mawasiliano kati ya Mungu na binadamu.

MZIMU NI NANI?

Mzimu ni mtu aliyekufa. kwenye ukoo au familia ambaye jamii husika inaamini katika uhai wake aliishi maisha ya kumpendeza Mungu.Kinyume cha mzimu ni Kizuka.

Kwakua inaaminika mtu mwema anapokufa hukaa kwa Mungu ndivyo ndani ya tambiko inaaminika hivyo.Hivyo ni sahihi kuomba kupitia mzimu ili maombi yafikishwe kwa Mungu.

Hivyo ,kuna tofauti ndogo kati ya Mzimu na mtakatifu anayetajwa kwenye ukatoliki.Tofauti yenyewe ni mchakato unafanya huyu aitwe mtakatifu na huyu mwingine Mzimu.Ingawa wote wawili wanafanana katika msingi wa maisha yao kabla ya kufa.

Ndio maana ndani ya ukatoliki kuna watakatifu wengi kama mizimu ilivyokua mingi.

Kwakua Yesu na Mohamed ni bindamu waliokufa katika dhana iliyoelezwa hapo juu ya kuzingatia maisha maisha yao enzi za uhai hawa ni mizimu

Historia kama maarifa Yesu na Mohmed ni wanaharakati waliokua wakifanya harakati zao huko mashariki ya kati karibu na mito Euphrates na Tigris ambapo inaaminika harakati hizi ndizo zilizozaa mtazamo wa kiimani uliopo sasa.

NINI KILITOKEA ?

Kwanza tukubaliane ujio wa ukoloni Afrika hakua na nia njema kwa muafrika mwenyewe.Kama hivyo sawa basi yote yalionzishwa ,kukuzwa na kuimarishwa nao hayawezi kuwa mazuri ikiwamo na dini.

Wakati ule wanafika Afrika kwa lengo la kutunyonya wakakutana na Tambiko.Kwakua ibada hiyo na imani nyingine za kiafrika hazikutoa nafasi ya kutimiza lengo lao,wakaamua kuliua Tambiko .Hvyo wakaanzisha Propaganda Tambiko ni uchawi na ushenzi.

Kwenye Tambiko sadaka hapewi mtu mmoja kama ni chakula kinaliwa na wote walioshiriki ama wote kuacha.Kama wangeacha Tambiko liendelee wangeshindwa timiza lengo lao la unyonyaji kupitia dini.

Hivyo wakaleta ibada ambazo mtu mmoja mwenye afya tele,nguvu na akili anapokea sadaka yote na kuzila au kuzitumia kwa niaba ya Mungu.

NINI MADHARA YA WAAFRIKA KULITUPA TAMBIKO.

Enzi za Tambiko kulikua na utaratibu uliowekwa kwa wote wanaotakiwa kishiriki kwenye ibada hiyo.Baadhi ya jamii watu waliofanya ngono kabla ya ndoa ,wezi,ambao wana ugomvi na wengine hawakuruhusiwa.

Hivyo si tu ilipunguza mmonyoko wa maadili lakini pia magonjwa kama ukimwi,kisonono na mengine hayakuwepo licha ya kutokuwapo kinga kama kondomu.

Na kwakua yalikua maombi stahiki kwa muafrika sehemu kubwa ya maaombi hayo yalijibiwa na Mungu.

Waafrika walipoomba mvua walipata,walipoomba mavuno walipata.Sasa hivi haiwezekani kuomba mvua na ikanyesha kwa sababu mizimu tunayoiomba si ya Keri ni ya warabu na wazungu.Ndio maana warabu na wazungu wanafanikiwa sana kuliko sisi wa Afrika kutokana na usahihi wa kuitumia mizimu yao.

JE TURUDI KWENYE TAMBIKO?

Ndio ,tukirudi kwenye misingi ya Uafrika wetu kizazi chetu kitabaki salama kwenye maeneo mengine yote.

Kama tutairudisha imani yetu basi pia tutapata namna yetu ya kuwapata viongozi wetu kupitia demokrasia yetu wenyewe ambayo haitafanya tuchinjane kama hii.

Tukirudi kwenye tambiko basi tupata namna ya kiimani ya kuendesha mambo yetu pasipo kufuata principles na kanuni za kimgharibi.

Kwakua imani ni tiba ya mambo yote mara tukaporudisha Tambiko Afrika tutagundua pia utajiri wa Taifa la Tanzania ukiupima kwenye kanuni za wazungu hutouona.

Wao wanapima shughuli zifanyazwo na wananchi wanakwepa kwa makusudi kujumlisha milima,madini,,tembo nk kwa sababi wana hakika mtawaamini kama mkishawaamini hata katika namna ya kuabudu.

Noel Nguzo.R.

20/1/2019
Hii nimeipenda sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vyema ukaja na mfumo kamili na Ustaarabu uliofindishwa kupitia Tambiko

Uislam
ulikuja na kukuta watu wakiabudu Masanamu waliyoyachonga wao kwa mikono yao,ukayaondoa yote
ulikuta ustaarabu mbaya wa unyanyasaji hususan kwa wanawake,ukaondoa uovu huo
Kisha ukatoa elimu,na vitabu vikaandikwa,kuwa hili ni Halali na hili ni Haraam
Kwakuwa mwanaadam ukimpa uhuru moja kwa moja,ni zaidi ya mnyama.
Tukafunzwa kuwa tusitende dhambi,kwani Mola hapendi dhambi
tukaaswa,tufanye mema,kwani Mola anawapenda wafanyao mema

Narudi kwako mkuu

IMANI YAKO YA TAMBIKO,inatufunza nini?!
na je,kuna Vitabu kutoka kwa Mola vilivyoshushwa kwa ajili ya kueneza ushirikina huo?!

HAKIKA YA SHIRKI,NI DHULMA KUBWA MNO

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini hawafundishi jinsi walivyoeneza dini zao hapa Africa

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Mwanamalundi wa usukumani aliweka maziwa yakakaa miaka bila kuganda akiwa kifungoni kisiwani, aliukausha mti mkubwa sana kama ishara yake ya mwisho wakati akikamatwa na askari wa kikoloni, soma historia ya utamaduni wako ndugu usiishie kwenye sunday school tu na madrasa

Sent using Jamii Forums mobile app
hivyo alivyofanya rahisi sana,maziwa hayakuaharibika kwa sababu ya hali ya hewa au aliyaweka dawa,mti kukauka ipo miti mingi tu huwa inakauka kwa sababu zake,hebu angalia hayo machache aliyoyafanya yesu wazee gani wetu walijaribu hata kwa uchache
 
Hayo matambiko yanaongozwa na kitabu gani? manake ukristu kuna biblia, uislamu kuna Koran, embu tujuze Mkuu
 
Mtoa Uzi nakubaliana na wewe kabisa,ila kuna mijitu hapa inakuponda wakati huo ukristo na uislamu umeletwa tu na mkoloni akatumia biblia na kurani ili kuhalarisha wizi wake kwenye rasilimali zetu,hao walioleta ukristo hata awana time nao huko kwao coz washaendelea ila sie huku tunajifanya kuujua sana ukristo na uislamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hakika umesema mkuu. Ni vigumu sana mara baada ya mkoloni kutuvisha IMANI yake na imetukaa BARABARA leo kukubali ukweli huu.

Watu wengi wamekuwa waanga sana baada ya kupokea imani za wakoloni na kusahau kule walipotoka.

Hii imekuwa ni mojawapo ya propaganda za kalne zile tulizotawaliwa na hao jamaa na kufikia hatua hii tuliyo nayo leo.

Hata serikali zote duniani mara baada ya kupoteza dini za awali nazo zimekumbatia UZUNGU na UHARABU pamoja na kwamba serikali wanachotaka ni AMANI tu.

**Namkumbuka marehemu mzee kingunge ambaye yeye inasemekana hakuwa mfuasi wa imani za wakoloni.

NB.
Bado nafasi ipo kila mtu kuamua kuabudu anachoona ni sahihi ili mradi asivunje katiba ya nchi.
Hawa watu wametukalia pabaya wanatumia vitisho vya kuwatenga watu na jamii zao panapotokea mambo yanayo igusa jamii kama misiba,sherehe na mengine ila ukweli ndo huo ibada ya mizimu ni bora na yakweli kuliko kitu chechote ila ndo hivyo tumeshikwa pabaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu wametukalia pabaya wanatumia vitisho vya kuwatenga watu na jamii zao panapotokea mambo yanayo igusa jamii kama misiba,sherehe na mengine ila ukweli ndo huo ibada ya mizimu ni bora na yakweli kuliko kitu chechote ila ndo hivyo tumeshikwa pabaya

Sent using Jamii Forums mobile app
Mleta Mada ana Hoja Ya msingi Sana. Mababu zetu walikuwa wakipata shida Wanakwenda sehemu maalum kwa ajili ya kufanya Ibada za matambiko na Mungu aliwasikiliza shida zao na majibu kupatikana haraka. Kushiriki Ibada hizo Mtu alipaswa kuwa msafi wa nafsi kwa maana asiwe ametoka kuiba, kuzini, etc. Hii yote ilikuwa ishara ya mwafrika kumuomba Mungu wake.

Leo watu wengi wanasali Eti kwa sababu siku Wakifa wazikwe kwa Ibada na mapambio.

Africans Tumeachiwa utumwa wa kifikra mbaya Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa maelezo yaliyoenda shule . Kwa mwafrika mwenye akili atafakari kwa makini hoja hii iliyojaa busara. Mimi nilipobatizwa nikiwa 18 years , nilipewa jina la kizungu na nikashangilia kama zuzu . Hoja hii mbele ya viongozi wa dini inawakera kwani huwanyima sadaka . " angalia kawimbo , toa ndugu toa ndugu ulicho nacho bwana anakuona mpaka rohoni mwako " Ndugu zangu waafrika turudi kwenye mila zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zote hizo ni imani huna proof kama yesu alikuwepo
Hiyo Ilikuwa njia fyongo ya kumtafuta Mungu.

Bibilia Imekuja kuwaelekeza kwenye Tambiko halisi Kwa Mungu aliyehai sio maiti za mababu zao, na mashetani.

'' Kwa Maana Jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee ili kila amuaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele'' Yohana 3:16.

Kuendelea kukumbatia Giza wakati mwanga upo, ni ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom