Kusema kweli wala sijali kabisa kama watakuwepo ambao watautumia huu mkasa dhidi yangu.
Nishakuwa mkongwe vya kutosha [blog-wise] kutobabaishwa na madongo ya watu ambao hata hawakujui na wewe huwajui.
Ngozi yangu ishanenepa vya kutosha na nimejifunza vizuri sana namna ya kupuuza hayo madongo na ndo maana wakati mwingine unaona dhahiri kuwa kuna watu wananirushia madongo lakini nawapuuza kabisa. Sitapungukiwa wala kuongezekewa na chochote na madongo yao.
I AM MADONGO-PROOF these days:becky:.
Ila kwa kweli matumaini yangu juu ya hili ni kwamba labda watajitokeza na wengine ambao pengine kwa sababu moja ama nyingine walikuwa wanashindwa kufunguka kwa sababu ya kuhofia kuhukumiwa.
Binafsi nilipata utanabahi wa uwepo wa hiyo hali nilipokuwa chuoni mwaka wa kwanza kabisa. Si unajua tena mambo course requirements, electives, na GPA boosters, mwishowe unajikuta unachukua Elementary French I & II, Intermediate French I, Introduction to Psychology 101, na kadhalika.
Sasa humo kwenye Intro to Psych 101 ndo kuna hayo mambo ya Oedipus Complex.
Kitu ambacho najaribu kukielewa ni kama hii hali inaendana na tamaduni za mtu/ watu au ni hali iliyo ya kibinadamu bila kujali tamaduni. Yaani inatokea tu pande zote za ulimwengu, Afrika, bara Hindi, Chinani, Ulaya, Marekani, na kwingineko.
So hopefully watu watafunguka.