Yesu ni Mungu kweli 100% na Mtu kweli 100%.
Ninasadiki kwa Mungu mwenyezi,muumba mbingu na nchi, na vitu vyote vinavyo onekana, na visivyo onekana.
Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu. Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote. Mungu aliyetoka kwa Mungu, Mwanga kwa Mwanga, Mungu kweli kwa Mungu kweli. Aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu. Aliyepaa mbinguni, atakują tena kuwahukumu wazima na wafu na wala Ufalme wake hautakuwa na mwisho.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele ijayo. Amina.