I only wanted simple life but always bad luck in my side

I only wanted simple life but always bad luck in my side

Pole sana.

Usikate tamaa ni habari za kuhuzunisha
sana japo ndefu lakini nimesoma yote
zaidi Muombe Mungu kwa Imani yako

Lakini usijiue utakuwa unafanya vitu vibaya
ni mapito hayo kuna siku utasahau yote
 
Pole sana, kama ambavyo haukuwahitegemea kwamba utamakiza shule ya msingi, Mungu akakusaidia ukamaliza, hali kadhalika mambo yakawa magumu sekondari, kwa uweza wake ukamaliza, ukaenda chuo bado Mungu akawa upande wako, hivyohivyo utavuka kipindi hiki kigumu na ni maombi yangu kwamba Mungu akuangazie rehema zake na kukufungulia milango.

MKATA KIU, ubarikiwe kwa hatua nzuri na nia ya dhati ya kumsaidia restuter
 
kuna kitu kama laana inakufuatilia unahitaji maombi ya ukombozi hata ukipata kazi leo still utapatwa na mikosi,kaa chini kama ni mkristo nenda kwenye kanisa lenyeupako ufanyiwe maombi ya kukutoa kwenye mikosi.... Mzee wa upako mch lusekelo anaweza kukusaidia.

Nadhani ulidhamiria kusema Bwana Yesu anaweza.

BTT:
Dada restuter langu ni kukuombea tu kila heri najua Mungu ana mpango mwema na wewe. If you don't mind ulisomea kozi gani chuoni?
 
Last edited by a moderator:
mmmmmmhhhhhhhhhhh aise pole dear, lkn usikate tamaa hujui Mungu kakuandalia nini kesho.......waswahili wanasema ukiona kamba imekaza sana basi ujue imekaribia kukatika.....hizo shida zooooooooooooooote ulizopata amin nakwambia ipo siku utazisahau, tena si muda mrefu......ndio kawaida hiyo kwani baada ya dhiki faraji....

kuna wkt mi nilipitia kipindi kigumu sana nikawa naomba Mungu anisaidie, naamka usiku nalia naomba lkn Mungu hakunijibu haraka km nilivyowish nikaendelea na matatizo km 2 yrs ivi mwishowe nikakata tamaa kbs nikasema labda Mungu hanipendi mbona hanijibu maombi yangu na haniondolei shida zangu hizi? nikaanza kuwa na chuki moyoni na pia nikawa siombi tena kwa kifupi nilikata tamaa kbs..
Pale nilpokata tamaa ndio Mungu akanijibu dua zangu zoooooooooote nilizoomba huko nyuma, Mungu alinipa faraja ambayo sikuitegemea, in fact alinipa kikubwa zaidi ya nilichoomba hadi nikawa nashangaa...nilishukuru na kutoa sadaka...sikuamini macho yangu...
kwa hivo kuwa na subira mdg wng Mungu hawezi kukupa mateso maisha yako yote kwani umemkosea nini? ni mtihani tu utapita na utasahau yooooote hayo yatakuwa historia..

Kuna member ametoa msaada wa kukupatia kazi hebu ichangamkie walau upate chochote my dear, pole sana.....
 
Rafiki yangu kipenzi alifariki kwa ukimwi kwa sababu hizi. Sitaki kukuhukumu lakini sidhani kama ni sahihi kuutumia mwili wako kujisomesha. Rafiki yangu alifariki baada tu ya kumaliza chuo na siku ya graduation alipigiwa brass band kwa sababu alikuwa best student.

Biblia inasema itamfaa nini mtu apate ulimwengu wote, naye mwenyewe aje apate hasara ya nafsi yake?

Kwa hela ndogo ulizopata kwa babu, bora ungesaka kazi ama ungefanya biashara walau ujikimu. Pole kwa mateso na kwa kumkosa mama yako. Lakini angalia wamama wenye upendo waliokuzunguka na ufurahie upendo wao. Mama yangu amefariki miaka mingi imepita lakini Mungu ni mwema amenipa wamama walezi wa kutosha.

Count your blessings
 
Mh.,sad! Pole sana binti! Only God at his own time will heal you. Amini Mungu hakukuumba upate tabu, but its a lesson he is teaching you on the path to your success.Matatizo yanapozidi amini mlango wa kutokea upo karibu.
 
Nadhani ulidhamiria kusema Bwana Yesu anaweza.

BTT:
Dada restuter langu ni kukuombea tu kila heri najua Mungu ana mpango mwema na wewe. If you don't mind ulisomea kozi gani chuoni?

i second you
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mdada... Mungu ni mwema ns anatuasa tusikate tamaa na kuyakimbia majaribu....

1Wakorintho 10:13
"Jaribu halikuwapata ninyi
isipokuwa lililo la kawaida ya
wanadamu ila Mungu ni
mwaminifu ambaye hatawacha
mjaribiwe kupita mwezavyo
lakini pamoja na lile jaribu
atafanya na mlango wa kutokea
ilimweze kustahimili."

Mungu awe nawe!!"
 
Tena mshukuru Mungu una pa kuanzia "Elimu" kuna watu wana same problems lakini hawana asset kama uliyonayo. Ajira is a matter of time utapata tu uwe na imani na badala ya kukata tamaa jange network na marafiki wa shuleni na chuoni kwa ajili ya kupata imformation mbali mbali za ajira hata kama sio za kudumu.
Eneo ambalo kwa sasa linasaidia watu wasio na ajira ni Reasearch, kuna NGO na taasisi nyingi sana zinafanya research na wanatumia graduates kama research assistants, unaweza kuanzia huko kujiweka bize wakati unaendelea na mapambano maana tatizo la ajira ni janga la faita.
Nitumie cv yako kwenye "vegasotieno@yahoo.com" kuna watu nafanyanao kazi kama consultant kwenye mambo ya research nijaribu kukuunganisha nao, ingawa siwezi ku-guarantee kuwa lazima upate ila ni katika kujaribu.
 
Pole sana
Ila wanasema ukiona mlima ujue upande wa pili kuna mteremko,

Pia Mungu aliekuumba ana makusudi na kila linalotokea kwako, Mtumaini yeye ktk kila kitu utaona matokeo mazuri

Ishi inavyompendeza Mungu, Yeye atatoa majibu


Na wala usimhuikumu na kumlaumu yeyote aliekuumiza, hiyo yote ni kazi ya shetani

Pole Sana, Mungu Aingilie kati maisha yako
 
daaah! yani nimesikia uchungu...........pole sana mdogo wangu!
Nikwambie kitu.....wewe ni fighter wa uhakika! usiruhusu kukata tamaa eti ujiue! hapana-songa mbele ukiwa na watu positive. Ipo siku machungu haya yatapoa! hayo uliyopitia yanaweza kuwa madogo ama yanafanana na ya wengine ni vile tu hatujaamua kuyaleta humu!
Wazazi wanaweza kuwa wamekuleta tu duniani, na kwakuwa umejua hawakujali, achana nao kwanza, usikae kuwaza tuuu kuwa kwanini wamekuacha! Unapoteza muda! Kazi yao imekwisha!!! Wewe ndio una kazi kubwa ya kubadilisha maisha yako!
Wapo watu wengi ambao marafiki wamekuwa ndugu moja, usikate tamaa utapata mama, utapata dada, kaka na mwisho wa siku utapata familia yako!
Ni jambo la kushukuru kuwa umekuja humu JF, hutaondoka bure. Ila tu uendelee kuwa makini mdogo wangu!!
Nasisitiza tena wewe ni fighter na ipo siku utatua silaha chini kwa ushindi utakaokuwa umeupata!
 
pole Mami, km umeyapitia Kweli hakika wewe ni SHUJAA, Na Mungu atafanya njia.. Hakika atakupandisha mlima usioweza kuupanda.. Atakupa wazazi na Mimi ni Dadako mkubwa.. IM with you..
 
This is so touching kwakweli,lakini hilo wazo la kujiua ni lakishetani yaani hata ucliwaze kabisa.
Kwanza mshukuru Mungu kwa elimu umepata kwa tabu lakini atleast una asset....Ajira ni tatizo la wengi sana mpnz lakini cha msingi ni kutokukata tamaa na kumuoma sana Mungu maana pekeako hauwezi kitu,jamo lingine ushauri umepewa hapo juu na members kama kutokuutumia mwili wako kujikomoa kimaisha maana ukiutumia mwili wako vibaya utapata kazi nzuri leo mwezi ujao magonjwa yanakuondoa af kutakua hakuna faida ya mateso yote uliyoyapitia,ivo hapo pia uwe makini na pia kuna mmoja kakushauri vizuri kuhusu kupiga maombi kuvunja malaana tunayoyapataga kutoka kwenye koo zetu ivo mtegemee Mungu na umshukuru kwa kila jambo na utaona matokeo yake.....Pole sana kipenzi lakini kila jariu lina mlango wake wa kutokea
 
Binti kaja kulia hapa ila anahitaji msaada..nadhani wana jf huyu mhitimu wa chuo hatakiwi kuwa ombaomba mtaani na kuishi maisha ya ajabuajabu...naomba muhusika uweke hapa sifa zako za elimu ya chuo watu waone wanawezaje kukusaidia...ajira au hata mtaji kidogo ujiendeleze kimaisha..at your age sipendi ulielie..just hit the point n people will resolve the rest of your matters.
1- umesoma chuo na kuhitimu katika fani gani?
2- una-mawazo au nia yoyote ya kufanya biashara au shughuli yoyote binafsi ya kujiongezea kipato?
3- kama jibu hapo juu(2) ni ndio..je unadhani kiasi gani kinahitajika kukuwezesha kuanza kujitegemea mwenyewe
4- unadhani bila mama au baba kuwapo huwezi kuishi duniani?
5- kama jibu hapo juu ni hapana huoni kama unatumia akili nyingi sana kuwazia kujiua badala ya kutumia akili hizo kutafakari njia ya kutoka katika shimo la hali ngumu ya maisha uliyokuwa nayo.
6- haudhani kuwa mchango wangu kwa hii thread yako umebadili kwa kiasi kikubwa fikra zako juu ya maisha?
7-kama jibu ni ndio kwa swali la (7) hapo juu huoni kuwa ni muda muafaka kuanza kutambua thamani yako kama mwanadamu na resources zako ulizozipata kwa elimu ya chuo ukiwa na basic knowledge ya science subjects.

Hitimisho...mleta mada wake-up chukua hatua mahsusi juu ya maisha yako na sio kulialia kama mtoto mdogo..you are a big girl now..n big girls dont cry.
 
Mleta madaaaaaaaa.
Hiii story yako naiomba na aikibidi tukutane tunaweza kuiuza kama kitabu na movie script..n u r a good story teller/writer....kwanini usiwasiliane na shigongo wa global publishers ukaiuza hadithi hii kama true story...na kwa upande wa movie waone mtiti game first quality.....thats an oppertunity in a disguise... U see ur life as a hell of trouble a see an oppertunity in your life story....baby gal soon u gonna be rich..i see u causin havoc to oprah riches in forbes magazine.
 
Pole sana mdogo wangu jamani.mie nakuombea kheri pia nakukaribisha nyumbani kwangu kama hutahitaji sehemu ya kuishi iliyo salama japo sina uwezo sana lakini sishindwi kukusaidia adi pale utakapo pata kazi na kuanza kujitegemea kwa kipato chako.
 
Jamani......!!!Kweli matatizo kaumbiwa binadamu!!!Pole sana bidada.....naomba urudi kwenye sredi na uweke kozi uliyopitia hapo chuoni.!!!:mvutaji:
 
restuter,, upo wapi? Naomba utujibu maswali yetu tujue tunaanzia wapi...
 
Last edited by a moderator:
amu sijapenda ulichokiandika..

restuter pole sana dada, you make me feel bad, sijui kwa nini..

Kama ulichoandika ni kweli haujatunga nitafute haraka nakupa internship ya data entry kupata 10,000 kila siku.. Ni very easy job unakuwa unasaidia kuingiza data tu kwenye system.. Ambazo ukifanya mfululizo hazizidi masaa mawili umeshamaliza za siku nzima.. Na ukifanya vizuri na kama wewe ni graduates utaajiriwa kabisa na kupata mshahara fair kabisa kwa graduate..

Angalizo hii ni kwa restuter tu kwa anayopitia,, maana hiyo kazi nafosi mtu ampe kinguvu.. Pm za graduates wengine naomba zisiwepo..

Niko serious kwenye hili, life ina mambo mengi sana, ni vizuri sana kumshukuru Mungu kwa ulichonacho

Mkata kiu mungu akubariki sana, akupe haja za moyo wako. Ni wachache sana wanaweza kufanya hivyo. Dada ni PM nikutumie hata senti kidog za kukuwezesha kupanda dala dala kwenda kwa mkata kiu kufanya hiyo kazi.

Jamani tuwe na moyo kama wa mkata kiu. be blessed, kind of you!
 
Pole sana restuter, historia yako inahuzunisha but usikate tamaa Mungu atakufungulia milango ya baraka na ninaamini hakuna kinachoshindikana ukimtegemea Mungu. Maadamu umeamua kufungukia hapa jf naamini hakuna kitakachoharibika JF huwa haimtupi mtu.
Pole kwa kuwa na mama asiyejali, amekuwa mzigo badala ya msaada, endelea kumtegemea Mungu
 
Back
Top Bottom