Wadau mimi ni msichana nina miaka 25 kiukweli sijui mapenzi ya mama wala ya baba na kwenye hii dunia najiona nipo peke yangu.Mama yangu alitengana na baba mimi nikiwa mdogo sana nahisi miaka 3 au 4 na ikapelekea mimi kulelewa na bibi kwani mama alikuwa bado hajiwezi kimaishaila baada ya mama kuolewa ikabidi niende kusihi nae na nlianza shule ya msingi nikiishi na mama na baba wa kambo na hapo akazaliwa mdogo wangu mmoja.
Kiukweli sijui kwa nini mama yangu alikuwa ananipiga sana yaani nakumbuka nlivunjika mguu,nilivimba uso na miguu kuwekewa pop mara kibao kipindi nlichokaa wakati naanza darasa la kwanza kwa makosa ya kitoto ya kawaia ya kunikanya mie nlikuwa napigwa na bomba la maji ile mipiraa napigwa nayo na kubamizwa ukutani mpaka kuzimia nakumbuka majirani walikuwa wanauliza huyu ni mama yako kweli?.
Kiukweli mama hakuwa anakunywa pombe wala baba wa kambo hawakuwa wanatumia kileo cha aina chochote mie darasa la kwanza naenda shule,nkirudi nipike nimuogeshe mdogo wangu niangalie nyumba usafi nichote maji mama yeye alikuwa hashindi nyumnbani wala baba.
Nakumbuka darasa la tatu nliunguza maharage nikapigwa na mama mpaka nikashindwa kutembea miguu yote miwili ilikuwa imevimba na kuwa na vidonda kwa kipigo kwa bahati nzuri bibi alikuja kutusalimia alifikia kwa mama mkubwa basi aliponikuta nipo vile siwezi kutembea kwa kipigo na sura imenivimba sana akanichukua na kwenda kuishi nae ambako alinisomesha na kipindi nlichokuwa nakaa na bibi kuanzia darasa la 3 nkawa na akili sana darasani wa kwanza .
Mungu akanisaidia nikamaliza shule ya msingi na wilaya ya ilala hapa Dar es Salaam nilikuwa ni mmojawapo niliyepata alama za juu kabisa.Nikachaguliwa shule ya serikali kuendelea na masomo ya sekondari kwa bahati nzuri bibi yangu alikuwa ana uwezo kidogo na yeye akapata kazi ya kusafirisafiri akahofia akiniacha nyumbani shule ya kwenda na kurudi nitapata shida maana hakuna mtu wa kuniangalia na kunihudumia basi akanipeleka boarding Kibaha(mpaka namaliza darasa la saba na kuanza form 1 kibaha sijawahi kuonana na mama).
Kufika Kibaha nikawa wa kwanza shule nzima naongoza somo moja tu lilikuwa linanishinda nalo ni physics kwa kweli bibi yangu namthamini sana kwa kunipa elimu maana Kibaha boarding nilikuwa sina tofauti na wenye wazazi wao wawili wanaohudumiwa na shule nliyokuwa nasoma ni ya bei sana watoto wa matawi waliokuwa wanasoma hapo tu bibi alikuwa ananivisit shule kila siku ya kujiwa,ananipa matumizi muhimu na ya ziada kikubwa alikuwa kila wiki ananiletea au anatuma ofisi ya shule dar maji yangu ya kunywa ya uhai (hiki sitosahau maana maji ya shule yalikuwa hayachemshwi yanawekwa kwenye filter tu na kusababisha intake kuumwa typhoid) alikuwa na mimi bega kwa bega ila hakunipa malezi ya kibibibi ya kunidekeza alinifundisha maisha jinsi ya kuishi na watu,upendo kazi za ndani na kama akikosa hela ananiambia na matatizo yote ananiambia.
Nilivyofika form 2 ndio siku moja shule mama akaja pamoja na bibi kunisalimia kwa kweli sikuona tofauti yoyote kwanza mama hakushtuka kuniona mwanae hatujaonana siku nyingi pili hakuwa na muda na mie.
Basi nikasoma mpaka nikamaliza o level kwa bahati nzuri nikafaulu kwa daraja la pili na kupangiwa shule ya dar kwa ajili ya advance level.Bibi akafurahi sana na akanipa simu nakumbuka ilikuwa Samsung ya kutouch mwaka huo 2005 na kunilipia ada na kunilipia hostel hapo nlichukua masomo ya sayansi na kusoma nakumbuka huu mwaka ndo bibi akaanza kuumwa na kudhoofika kwa hiyo ikawa shida kupata matumizi ila nikajitahidi hivyo hivyo kufikia 14/8/2006 bibi aliaga dunia na mie nikawa natangatanga maana upande wa baba wapo ila ni watu ambao hata nikiwa na shida hawawezi kunisaidia hata Tshs500 na sijui ni kwa nini na upande wa mama mama zangu wadogo wengi walishafariki na mama zangu wakubwa nakumbuka wengi walikufa kwa ukimwi nahisi ni kwa sababu walikuwa wazuri sana na kipindi kile elimu ya ukimwi haikuwa imesambaa sana .
Bibi alifariki mi nipo form 6 nilihangaika sana bahati nzuri nikapata mkaka mmoja tukapendana na kiukweli alinisaidia sana shule akawa ndo ndugu yangu wa karibu sana yule kaka alikuwa anakaa nje(Uingereza) ila Tanzania alikuwa anakuja kwa mwaka at least mara 3 basi akanisaidia kwenye finance shule na mtaani na kikubwa bibi alikuwa anatulea mimi na dada yangu mtoto wa mamkubwa(mama yake alifariki) ila yeye alikataa shule na akahama tulipokuwa tunakaa akaenda kupanga hakuwa na kazi ila alikuwa anaishi na mwanaume kipindi ambacho bibi alikuwa anaumwa na yeye alirudi nyumbani alikuwa anaumwa HIV bibi alipofariki na yeye akawa anaumwa sana kila wiki tulikuwa tunampeleka kulazwa hospital jkt kwa kusaidiana na mjomba wangu(huyu mjomba ni misheni town tu na akipata tunashukuru anaunua vyakula analeta nyumbani).
Bibi alipofariki mimi na dada yangu huyu yule kaka mpenzi akatusaidia sana akawa anatujali kama familia yake akiwa yuko UK ananitumia western union matumizi na bili ya dada ya maziwa na matunda.
Mungu akasaidia nilimaliza advance level 2008 nikadata daraja la 3 yule kaka akajitolea kunisomesha chuo nikaanza kufatilia kujiunga nikapata chuo kimoja cha mambo ya finance hapa town ikabidi yule dada yangu kuniona mimi busy na chuo na hela zinatumika sana ili kupunguza mzigo ikabidi aende Burundi kule kuna mama yetu mkubwa ameolewa na akaenda kujiuguza huko nami nikaanza kusoma chuo.
Kwa kweli gharama za chuo ni kubwa sana na kwa msaada wa yule kaka nikawa nasoma japo mwaka wa kwanza katikati yule dadangu alifia Burundi na mie sikufanikiwa kwenda kumzika na hakuna ndugu aliyeenda kumzika zaidi ya yule mama yetu mkubwa aliyekuwa amejenga familia huko.
Kwa kweli hili ni pigo jingine kubwa lililonikuta maana yule alikuwa ni dada yangu kama tumezaliwa tumbo moja.Na mpaka kipindi hiki mama hakuwa akinijali yeye akipiga simu ni kueleza matatizo na kutaka hela au vitu kiukweli nilikuwa Nampa sana hela na kumnunulia nguo yeye pamoja na mdogo wangu ili hiyo tabia ilikuwa inanikera sana hajui kunisalimia siku kipiga simu yeye ujue anashida tu.
Bai kwa msaada wa yule kaka tukafanikisha mwaka wa kwanza ukaisha salama. NIkaanza mwaka wa pili hapo naishi chuo hostel mwaka wa pili kuelekea kufanya test 1 chuo kikapandisha ada ghafla kutoka milioni moja kuwa 1,500,000 nikampa habari yule mpenzi wangua aliyekuwa msaada wangu akashtuka sana ila akaniambia nisijali atajitahidi basi nikafanya test exams na kumaliza kuelekea mitihani ya First Semester ada alikuwa hajanitumia nikawa nasoma huku namkumbusha.
Nakumbuka ilikuwa jumamosi ambapo jumatatu tuanze test msg iliingiakwenye simu yangu samahani ahirisha mwaka mambo magumu sana sitoweza kulipa nlichanganyikiwa na kulia sana maana aliniahidi kuwa ningeenda kupokea siku ile ya jumamosi katika kumbanabana nikaelewa kuwa alikuwa anamsafirisha mdogo wake aende Norway alikuwa hana hela.
Nilichokifanya nikaenda kwa registrar nikalia sana ili anipe kibali nifanye final exams ada nitailipa baadae siyo kuahirisha mwaka.Kwa kweli nikafanikiwa japo kwa sharti mtihani hausahihishwi mpaka nilipe ada na nlikuwa kipindi kigumu sana nafanya final hata hela ya kununua chakula sina naingia kwenye mtihani nina njaa au pengine sisomi kisa njaa ila nikafanikiwa nikamaliza mtihani.
Hapo nikaanza kumtafuta boyfriend wangu kwa internet tuongee kiundani ndipo nlipokumbana na kubwa kuliko alikuwa kwenye maandalizi ya kuoa kwa kweli nililia sana nusu nife kwa kuchanganyikiwa nilipiga kelele watu wote wakanishangaa nikamfata rafiki yangu nikamweleza akanibembeleza na akaniambia cha msingi ni kujipanga tu huyo siyo wako tena.
Nawashukuru sana marafiki zangu walikuwa wawili mmoja yatima sema ana kaka zake wakubwa na mwingine kwao wanauwezo kidogo wakanichangia laki 2 hapo bado laki 3 ili mtihani usahihishwe .
Sikuoga siku 2 nakumbuka kwa mawazo kiukweli marafiki zangu wakaamua kunitoaout tukaenda kule chole road kuna kipub wote hatunywi pombe tukaenda kula mishkaki na kutafakari laki 3 itatoka wapi ili zitime 5 mitihani isahihiswe .
Ile tunakaa na kusubiri mishkaki wakaja wababa 3 na mzungu mmoja wakavutiwa na sisi wakaomba meza ziunganishwe tukae pamoja ila wakagundua sipo sawa maana hata kuvaa I was not smart na nlikuwa na mawazo sana I was not happy at all ila wenzangu walikuwa achangamfu.
Baba mmoja alikuwa anafanya kazi ikulu akatokea kuvutiwa na mimi sana ila kiukweli hata kuongea nlikuwa nimeshindwa naona kero kwa shida nlizonazo akawa anaongea na rafiki yangu kwa kweli without you (mwajei)sijui ningekuwa wapi leo maana uchakaramu wako uliniokoa mambo mengi sana maana wale watu wakasema waturudishe nyumbani hapo tulikuwa tunaenda makumbusho kwa nyumbani kwa rafiki yetu kisha tutoke wao wanapenda taarab mzee Yusuf alikuwa anapiga bilicanas mi nkakataa tukarudi makumbusho wao wakavaa wakatoka mi nikawaambia nalala kumbe kule kabla hawajaingia yule baba akawauliza mbona mwenzenu hajaja na inaelekea kuna kitu kinamuumiza ndo wakamuambia ukweli maana walishakuwa marafiki zao.
Basi yule mzee akasema ujue mie nimempenda sana yule mwenzenu na inaniuma kama anashindwa kumalizia elimu yake kamwambie avae apendeze afurahi kesho nitamtuma mtu awaletee hizo hela wakaja kuniambia kiukweli sikuwaamini nlijua ni janja yao tu mpaka yule mzee alipokuwa nje akapiga simu ndani na kuongea na mimi.
Kiukweli nikavaa nikapendeza sana mashosti wakanisaidia kuninga'arisha na tukaenda mziki tukarudiswhwa alfajiri ambako hatukulala tukawa tunasubiri kuona ni kweli au ndoto.
Kufika saa 7 mchana yule mzee akapiga simu tukaenda kuonana nae steers akanipa bahasha na kuniambia kalipe ada sasa hivi bank. Kiukweli nikafurahi sana na tukaenda kulipa.
Huyu mzee alinipa laki 5 akaniambia nikalipe hiyo kisha mwisho wa mwezi angenimalizia zilizobaki ambazo ni laki 3.
Kumbuka tulikuwa tunalipa awamu tatu laki 5 laki 5 awamu ya kwanza my ex bf alilipa 500,00 na rafiki wakanichangia 200,000.
nilimuona kama Mungu yule mzee japo alikuwa akinitaka kimapenzi ilihali yeye ni mubwa sana kwangu .
Yule mzee sijawahi kumpa penzi mpaka leo sababu yule rafiki yake mmoja alikuwa anatembea na rafiki yangu yule muongeaji akamuambia kuwa mwambie rafiki yako (mimi)awe makini yule mzee kaathirika kiukweli nilimuogopa sana yule mzee.
Japo nlikuwa naonana nae namfata kinondoni pale Hombus au masaki chole road lakini nlikuwa namuogopa maana ni mkubwa sana kwangu na yale ya kuwa yeye muathirika na kila nkionana nae alikuwa ananipa 80,000 au 70,000 nlionana nae kama mara 3 ikabidi nianze kumkwepa kwa nliyoyasikia japo ahadi ya laki 3 aliitimiza mwisho wa mwezi alinipa nikaenda kulipa ada yote na nikawa sidaiwi.
Baada ya kukata mawasiliano yule mzee akawa ananitafuta sana mie nikawa namkwepa hivyo hivyo mpaka akahamishiwa Kigoma kikazi ndo ikawa salama yangu.
Likizo ya first semester iliisha na nikaanza shule tena kiukweli shule maisha yalikuwa ya shida sana kwani though rafiki zangu walikuwa kila wanachokula wao na mie nakula hicho hicho walinisaidia sana ila mie mwenyewe sikuwa na amani ya moyo pigo la bibi,dada bf kaniacha mama hajui naishije wala baba.
Ila nikawa nasonga mbele baada ya mda nikapata bf alikuwa kijana tu na kazi yake nzuri alikuwa anasoma chuo masters na alikuwa anafanya kazi basi yule kijana alinipenda sana na akawa ananisaidia sana mambo mengi pale chuo alikuwa zaidi ya rafiki kwangu.
Nikamaliza mwaka wa 2 na kuingia wa tatu kimbembe cha ada kikaanza bahati nzuri wanafunzi walikishtaki chuo kwa kupandisha ada ghafla na wanafunzi wakashinda kesi ikabidi washushe ada ile ile 1,000,000 waicarryforward laki 5 na sie tumalizie kulipa laki 5 tu.
Bsi yule bf wangu akanilipia hiyo hela na kunisadia baadhi ya vitu na wale marafiki zangu wakaendelea na system ile ile wanachokula wao nakula mie kama nikiwa chuo tupo wote na wao walikuwa wanapenda yule bf wangu nimalize chuo tuoane na kuwa pamoja milele ambacho na mie pia nilikuwa nakiombea.
Too bad mwishoni wa semester ya kwanza nikamfumania kwake na mwanamama mkubwa kidogo na tukagombana sana akaomba msamaha sana ila kiukweli nilimpenda sana na sikuwahi kumchit japo nlikuwa natongozwa sana na watu hapa mjini ila sikuwahi kumchit niliumia sana sana na sikumsamehe nikaachana nae na kuendelea na maisha yangu kwa msaada wa marafiki na tukamaliza chuo japo sikufaulu sana ila nashukuru.
Baada ya kuachana na huyo kaka mpaka leo hii sijawahi kupata mwanaume ambaye anaonyesha usiriaz na mimi mie nampenda wanaishia kuniumiza tu na mpaka leo hii maisha yangu ya tabu sana sijapata ajira naishi kwa kutanga tanga na msaada wangu ni yule rafiki yangu ambae na yeye hajapata kazi ila ameolewa ndo mtu wa karibu yangu na mama nae tabia ni ile ile akinipigia simu mpaka awe na shida japo anajua maisha yangu japo yule mdogo wangu wanamsomesha chuo yeye na baba wangu wa kambo hicho kitu kinaniuma sana maana mie tokea nianze kusoma na shida sana zote hizo nilizopitia hata 5000 au nguo hajawahi kuninunulia mama .
Baba nae hata nikionana nae hanijali cha lolote nisipomkumbuka mimi yeye hana habari na mimi japo ana maisha yake mazuri.
Nina bahati mbaya nimesoma kwa shida sana maisha yatabu nimepitia mpaka leo sijapata ajira naishi maisha ya ovyo tu saa nyingine natamani kujiua na nanhisi mda wowote wakati wowote nitajiua kwa karaha za dunia na sina mpenzi anayenipenda labda sababu sina family, sina ndugu sina kazi sina hela wanaume wananiona mzigo wanaishia kuniumiza moyo tu.
Ila kinachonitia moyo ni zile Nguvu za marehemu bibi alizohangaika kila nikijifikiria kujiua naona sitommtembea haki maana alihangaika sana na mimi.
Na kwa sasa nimekosa confidence ya maisha naona Mungu alinipangia masiha haya niishi ya kutokuwa na amani tele.
Nimeandika yote haya sababu tarehe 12/5/ ni Happy Mothers day na sina wa kumuwish maana sijui kama huyu kweli ni mama yangu anayenifanyia haya au nini?
Nimekubali na kuvumilia ila mapenzi ya mama yananiuma sana leo hii nikiwa na tatizo la kiundani sina mtu wa kumwambia zaidi ya my rafiki.
Mama anaweza kukaa miezi 3 asinipigie simu mpaka awe na shida.
Am not lucky at all natamani ningekuwa na familia iwe na mama au na na mume ingenipa faraja ningesahau yote hayo ila sina wa kunipa faraja maisha haya.
Sijui nimemkosea nini Mungu maana miaka 25 najihesababia yatima nisiyekuwa na kitanda wala godoro kula kwa rafiki, sina cha maana kila mtu ananiona mzigo sasa.