@restuter
Nimesoma maelezo yako.....nimeamini kwamba umesema kweli, na si utunzi! Umejaribu kueleza mengi sana (kuna mengine sio relevant kwa ulichotaka kutuambia). Nakupa pole sana kwa maisha uliyopitia, ambayo mengi yamekutokea bila wewe kupanga! Hujapata nafasi ya kuchagua sehemu kubwa ya maisha uliyoisha na unayoisha sasa.
Kuna jambo moja naona katika maelezo yako, kamba umepitia ugumu ambao unakufanya uwe ulivyo! Too negative! Kwa mtazamo wangu hili la kuwa 'negative' sana linafanya ushindwe kuwa na mahusiano muafaka kwako.....pia unaonekana kutegemea uhusino ubebe matatizo yako yote, bila ya wewe kuwajibika kwa uhusiano huo.
Kimsingi hakuna mtu anaependa uhusiano wa kutegemewa sana....kwamba unajiweka kundi la unyonge.....kuhitaji msaada, kutojiamini! Pia nahisi unaweza ukawa huna dira ya maisha yako, kwamba unategemea anayekuja akuamulie kila kitu........SIO RAHISI KUPATA MWANAUME ANAYETAKA MTU WA AINA YAKO.
Ushauri wangu: pamoja na shida zako, jitahidi kuwa 'positive' katika maisha......jenga dira yako ya maisha....ona pale unapotaka kwenda.....na niamini utafanikiwa, katika mahusiano na katika maisha kiujumla! Jitahidi usionekane ni mzigo....kwamba una cha kuchangia kwenye dunia hii!