I got it! Mheshimiwa Spika mnataka kutuloga!!?

I got it! Mheshimiwa Spika mnataka kutuloga!!?

asilimia kubwa ni wachawi..si ndo maana kuna kipindi walishikishana uchawi enzi ya mzee sita
 
Haya ni maamuzi ya nec na cc yao, sikutegemea kama wangekuja na mawazo ya maana, maana mijitu yenyewe imechaguliwa kwa rushwa bila uwezo, wengi hawana uwezo wa kusahili mambo madogo, unategemea nini, mtu anayeshindwa hata kuamua ugomvi mdogo wa kuchinja, hawawezi hata kubuni stategies za kukubaliana na upinzani unaokuwa kwa kasi.



Ccm wanashindwa kufikiri pindi wanapokosea, kila hatua wanayochukua ndio wanazidisha chuki kutoka kwa wananchi, itawakost mno, kwani uongo utatawala kuhusu vikao vya bunge na kwa kuwa watu wanawachukia tayari itakuwa rahisi kwa taarifa yoyote ya uongo kukubalika kwa uma kwa kuwa hakuna ushahidi

ccm inazeeka kwa kazi kuliko tunavyoina na tunavyodhani.
 
Wanataka kuficha taarifa sahihi, then wataleta propaganda kwa maana ya uongo, watatupa taarifa iliyochakachuliwa kupitia vyombo vyao vya habari hasa hasa magazeti yao ya uhuru na mzalendo kwani kwa sasa hayauziki, kwahiyo wanataka kulazimisha biashara ya magazeti yao. Tukae mkao wa kuliwa, bado wanafikiri Watanzania ni MAZOBA au MANDONDOCHA.
wanataka kuficha nini? Si wanachojadili ni kuwawakilisha wananchi? Wanataka sisi tuelewe nini, kwani wanataka kunyonyana ndimi huko bungeni? Hii ni dalili ya uchizi kwa hawa viongozi!
 
Mzeemwanakijiji naona hii post inatoka moyoni kabisa, BIG UP
Ila ungemalizia na nini kifanyika
 
Last edited by a moderator:
Hili halivumiliki. ****** na Makinda ni mashetani. Wabunge wa CCM ni 'mashetani' watoto.
 
Inaudhi tunapopiga hatua mbili mbele kisha tunarudi hatua 50 nyuma. Wenyewe wanafikiri kuwa wanawakomoa wabunge wa upinzani, kumbe wanawamomoa watanzania ambao wanataka nchi yao iendeshwe kwa mujibu wa kanini, sheria na katiba pamoja na kwamba katiba ya sasa ni ya ovyo.

Wananchi watatafuta njia mbadala ili kuweza kukabiliana na U.J.I.N.G.A huu. Ukimbana mtanzania mnyonge atatafuta mbinu nyingine hadi sauti yake itakaposikilizwa. Mwaka huu mtasikia mambo mengi tu.
 
Kwa jinsi hii , CCM itaendelea kushika hatamu ya uongozi wa Nchi hii, tusipokuwa kuwa makini.
Wajumbe wa tume ya katiba wameteuliwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM,
Tume ya uchaguzi imeteuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM,
Wabunge wengi ni wa CCM,
Wakuu wa Idara na Taasisi zifuatazo wateuliwa wa Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM.
Mkuu wa Majeshi,Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Jaji Mkuu ,Kamishna mkuu wa Magereza,
Waziri mkuu, Mawaziri na manaibu wao, Makatibu wakuu wa Wizara, Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi wa maendeleo wa Mikoa na Wilaya, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
KUELEKEA 2015 WATANZANIA KAZI KUBWA NA NGUMU TUNAYO .

,



 
Nadhani kama wakiweza kuthubutu kuweka vikao vya bunge viwe vya siri basi kwa asilimia 90% ni ticket nzuri ya Chadema kuchukua nchi na kila mkoa watakao enda lazima wananchi waambie ukweli na hali halisi, nadhani ni movement nzuri maana wenyewe CCM wanaweza kuona wanafanya vizuri ila ni Big Mistake ambayo watakuja kuijutia......Me naona wacha wafanye hivyo then wananchi ndio wataona ukweli na hali halisi.....
 
Inaudhi tunapopiga hatua mbili mbele kisha tunarudi hatua 50 nyuma. Wenyewe wanafikiri kuwa wanawakomoa wabunge wa upinzani, kumbe wanawamomoa watanzania ambao wanataka nchi yao iendeshwe kwa mujibu wa kanini, sheria na katiba pamoja na kwamba katiba ya sasa ni ya ovyo.

Wananchi watatafuta njia mbadala ili kuweza kukabiliana na U.J.I.N.G.A huu. Ukimbana mtanzania mnyonge atatafuta mbinu nyingine hadi sauti yake itakaposikilizwa. Mwaka huu mtasikia mambo mengi tu.

Mkuu wangu ndio nimesema hapo juu wakifanya hivi nadhani itakuwa njia nzuri sana kwa Chadema na njia itakuwa nyeupe kabisa hapo 2015 maana hamna mwananchi atakubali iwe hivi au sidhani kama kuna nchi ambayo vikao vya bunge wanafanya kwa siri....
 
Moto hauzimwi kwa kufunika na shuka au kumwagia mafuta ya taa au petrol.
Kwa hili Watanzania hatutalikubali, labda wakabadilishe Katiba ya Nchi.


42470281_bbc72ccff5_o.jpg


Vikao vya wachawi hufanyika kwa siri. Sasa sijui kama uchawi upo na una nguvu au ni imani tu lakini ukweli ni kuwa wapo watu wanaamini katika nguvu za uchawi. Vikao vya wachawi hawaalikwi waandishi wa habari. Sababu kubwa ni kuwa vikao hivyo vinahusiana na mambo ya kudhuru zaidi kuliko kitu kingine chochote. Wachawi basi hupenda mambo yao yawe ya siri sana.

Mtu anapoamua kwenda kutafuta msaada wa wachawi (ni wale waganga wa kienyeji wenye uwezo wa kudhuru) ni kwa sababu ameshindwa kukabiliana na kile alichokiona kuwa ni tishio. Mara zote watu wanapoamua kutafuta msaada huo ni kwa sababu wanaamini mbinu za kawaida za kukabiliana na mtu zimeshindikana. HIli ni kweli siyo katika Afrika tu bali hata katika mataifa mengine ambayo imani hizi za kishirikina zipo.

Kwa vile vikao vya wachawi ni vya siri basi ndio maana havirushwi 'live' ila nina uhakika kama tukiwapa nafasi warekodi vikao vyao makaburini watatupatia 'edited versions' ya vikao hivyo. Unafikiria watakapoleta hayo matoleo yaliyohaririwa wataonesha nani wanapanga kumla nyama? Wachawi hawaachi hadi wakamatwe! Sasa kama ni kweli upo uchawi mimi sijui; ila kwamba wapo watu wanaoamini nguvu zake hilo halina shaka. Na kwa wale wenye kuamini nguvu zake, uchawi ni tishio kubwa sana kwani mambo yanayofanywa na wachawi yanavunja kanuni zote zinazojulikana za Fizikia.

Uamuzi wa Bunge kuamua kuleta pendekezo kwenye kikao kijacho kuwa Bunge lisioneshwe moja kwa moja kwa mamilioni ya wananchi wa Tanzania ndani na nje ni uamuzi unaofanana na kikao cha wachawi. Sijui ni nani aliyekuja na wazo hili sasa hivi baada ya wazo hilo kutupwa miezi michache huko nyuma. Lakini kwamba sasa umekuwa ni uamuzi rasmi na kwamba wapo watu wenye akili timamu bungeni wamefikia uamuzi huu ni lazima niulize kama hawa ndugu zetu si vigagula!

Wanachoogopa hawa watu wa Bunge kwa wananchi kuona moja kwa moja vikao vya Bunge ni nini? Kwamba wananchi watawaona wabunge wenye kutoa hoja zisizo na mashiko na hivyo wabunge hao wataanza kupunguza ujiko waliodhania kuwa wanao? Ama wanaogopa kuwa kwa kadiri wananchi wanavyozidi kuwaona wabunge wao wanavyobishana na kulumbana basi kule kulegalega kwa Bunge kutazidi kuwa dhahiri? Au wanaogopa kuona kuwa wananchi watazidi kuona kupwaya kwa serikali yao? Au wanaogopa zaidi kibinafsi kuwa waliodhaniwa kuwa ni viongozi kumbe si lolote na si chochote? Au wanaogopa watu kuona jinsi sera za CCM zisivyoweza kutetewa na jinsi ambavyo kwenye kila kikao sera hizo zikioneshwa kuwa hazitekelezeki huku majibu ya "serikali ina nia" na "serikali iko njiani" yakiendelea kutolewa kwa miaka hamsini sasa?

Lakini mimi nafikiria kuna sababu nyingine ya kutisha zaidi - wanataka kuturoga. Nadhani jaribio lao lile la "unga unga Bungeni" lilikuwa ni jaribio la kwanza kutaka kuliroga taifa zima tuwe mazezeta tusiofikiri, tusiouliza maswali na wenye kuamini kila tunaloambiwa na watawala. Kwa vile ndumba zile nusura zinaswe kwenye luninga jaribio lao la kuturoga lilishindikana. Matokeo yake ni kuwa wananchi wamefunguka zaidi na kuwaelewa wabunge wao; wameilewa serikali yao na kwa kweli wananchi hawakumwogopa kabisa mchawi wao. Aliyedhaniwa ni mchawi mkuu wa taifa aligundulika kuwa ni kilaza tu tena tapeli.

Sasa inaonekana wanataka kujaribu tena. Lakini katika kujaribu huku wameficha nyuma yake dharau. Wametudharau Watanzania na dharau ambayo kwa kweli inapita kwa mbali matusi ambayo Spika na Naibu wake wanadaiwa kutumiwa kwa sms. Maana kudharau taifa zima kwa kweli inataka moyo! Wanaweza vipi kuamua tu kuwa "hatutaki Watanzania watuone tunavyozungumzia mambo yao hadi tuamue tuwaoneshe nini". Sasa kama hii siyo dharau ya taifa (contempt of the nation) tuiite nini? Kwanini wasiamue tu kuvunja Bunge au wafanyie vikao kwenye jumba la spika lile jipya? Au waende kwenye nyumba ya Waziri Mkuu? au wakitaka wakafanyie vichakani baada ya kulishana yamini kwanza!?

Binafsi napinga, nalaani, na ninakataa kudharauliwa hivi. NInakataa kuonekana mjinga na kuwa sisathili kujua wale ambao wamechaguliwa na wananch na waliopita kuomba kura wengine kwa kupiga magoti na kulamba watu miguu leo wana ujasiri wa kusema 'tuwafiche wananchi waliotuchagua". Mtanisamehe - huu ni miongoni mwa maamuzi ya kipumbavu. Mtu mwenye akili akikushauri jambo la kijing akijua wewe nawe una akili halafu ukakubali atakudharau - alisema Baba wa Taifa. Wametuambia jambo la kijinga swali ni je tunajitambua na sisi tuna akili?

Nina pendekezo - kama kweli uamuzi huu utachukuliwa naomba uchukuliwe hadharani angalau mara hiyo moja kabla hawajaacha kurusha matangazo wapigiwe kura ya kuitwa majina (roll call) ili tujue wabunge wetu ambao wanataka kutuficha wanachofanya Bungeni ni kina nani? Na kama kuna wabunge wa upinzani wanaofikiri hili ni jambo jema wasimame na waseme sasa; kama wapo wabunge wa CCM wanaamini kuwa hili ni jambo jema wasimame na wajitaje kwa majina yao Bungeni kuwa wanaunga mkono kuwaficha wananchi waliowaajiri kujua nini wanafanya.

Angalau tutawajua wachawi wetu kwa majina yao!

Na. M. M. Mwanakijiji
 
Mungu wangu kumkomboa mwanamke ni dhambi kabisa tukawajali tukasema tu wape nafasi za juu (Top up aproach), hapo ndio tumejiloga niambie sasa mpaka hoja za maana zinapotezewa tunaangalia tu bila kushout nadhani huu sio utaratibu CDM tupo makini kwa hili njia walioitumia wamefel poleni CCM hamjielewi kabisa hata hamjajua kwamba mmekosa mvuto kwa citizen kwa ujinga mnaoufanya..ombi langu watanzania tuwe makini kwa hili Tv lazima zioneshe kinachojiri bungeni maana bunge ni la watanzania na wala si la Makinda au Jk hatuogopi huu ndio mwanzo...peoples....power.
 


Nina pendekezo - kama kweli uamuzi huu utachukuliwa naomba uchukuliwe hadharani angalau mara hiyo moja kabla hawajaacha kurusha matangazo wapigiwe kura ya kuitwa majina (roll call) ili tujue wabunge wetu ambao wanataka kutuficha wanachofanya Bungeni ni kina nani? Na kama kuna wabunge wa upinzani wanaofikiri hili ni jambo jema wasimame na waseme sasa; kama wapo wabunge wa CCM wanaamini kuwa hili ni jambo jema wasimame na wajitaje kwa majina yao Bungeni kuwa wanaunga mkono kuwaficha wananchi waliowaajiri kujua nini wanafanya.

Angalau tutawajua wachawi wetu kwa majina yao!


Na. M. M. Mwanakijiji

Naungana nawe katika hili mkuu. Na pengine wabunge wa upinzani kama hawaungi mkono wafanye kautaratibu fulani kakuwashtua. Mfano watafute sahihi kadhaa za watanzania wanaopinga mawazo mgando hayo. Madhara ya kutoonesha bunge ni mabaya sana. Why should they give us edited information?
 
Hii hoja ikifika bungeni itapita maana CCM ni wengi. Lakini ili kutumhukumu mtu kimakosa, naunga mkono wazo la kutaka kila mbunge aitwe (mmoja mmoja) wakati wa kupiga kura, ili wananchi wajue pasi na shaka kuwa nani anataka vikao vya bunge viwe siri, na nani anataka bunge liendeshwe kwa uwazi.

Kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake.

Unafikiri watakubali kufanya hivyo? Hakuna mchawi anayetaka aonekane kweupe, ndiyo maana hata kulisema hili kasukumwa Dr Kashilila. Mimi ninnasisitiza tatizo ni huyo Kashilila kukubali kutumika. Ndiye chanzo cha kupindisha kanuni, kwani wale wanaojidai kuzijua kanuni (spika, naibu spika na wenyeviti wake) hawazijui wanawategemea hao hakina Kashilila na kundilake. Walipaswa kusimamia haki na kuhakikisha kanuni zinatumika vyema. Inawezekanaje kanuni moja ikatafsiriwa au kutumika tofauti kulingana na Mbunge ni wa upande gani au Ana msimamo gani!
 
Big up MMM! Haingii akilin kabisa. Huyu katibu wa Bunge achunguzwe akili yake. Nina wasiwasi na uelewa wake wa mambo.
Maswala yanayohusu Tanzania kama Nchi wanayaficha kwani ni ya kifamilia?? Fanyen haya maamuzi kwa wake zenu na waume zenu, msituletee Watanzania.
 
halafu juzi juzi tu yamejiongezea mshahara ili wjadiliane mafichoni.
 
Udikteta wa Hitler haukuanza siku mmoja, alianza taratibu kama tunavyoyaona sasa, mwisho ukawa dikteta halisi. Hata kauli ya Rais kwamba Polisi wasiogope Lawama imenisononesha sana. Lazima tuilaani hatua hii ya kuipeleka nchi kwenye udikteta. Nadhani hata baba zao wanaowafadhili (wahisani) hawatakaa kimya ktk hili. Let us see.
Mkuu Aweda kama utakumbuka kauli ya Sumaye kwenye mbio za urais za 2005, kwamba anayetaka kuingia madarakani kwa risasi ya kalamu, akiingia madarakani atatumia risasi za moto... Kauli hii ni dhahiri kabisa kwa Rais wetu kufuatia maagizo yake hayo kwa jeshi la polisi. Maneno ya Sumaye yanatimia sasa!
 
Mkuu mwanakijiji hata utafiti wa CNN ulionecha mwaka jana kuwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania inaongoza kwa imani za kishirikina kwa asilimia zaidi ya 90. Maneno haya nakubaliana nayo mia kwa mia kwa kuwa si mara moja nimesikia habari za viongozi wengi walio madarakani sasa hivi, kuwa walienda kwa mganga huyu na yule (wa Kienyeji) kutafuta dawa za kujizindika. Naamini hata mauaji ya albino yanaweza kuwa yamechagizwa sana na tabia hii ya viongozi. Wengi wa Viongozi hawaamini kuwa wanaweza kupata vyeo kwa kufanya kazi kwa bidii, badala yake wanaamini kwa nguvu za kishirikina.
 
wapi watanzania mnaongea tu hapa kama mmeguswa hakuna kuwa bembeleza tuanze kuwazomea wabunge wote watakao kuwa hawajatoa tamko la kumpiga bi kiroboto mpaka mwisho wa mwizi huu na bunge lijaro tukutane dodoma tuone kama ukumbi utatosha..
 
Back
Top Bottom