JiweLinaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,737
- 2,139
Nina pendekezo - kama kweli uamuzi huu utachukuliwa naomba uchukuliwe hadharani angalau mara hiyo moja kabla hawajaacha kurusha matangazo wapigiwe kura ya kuitwa majina (roll call) ili tujue wabunge wetu ambao wanataka kutuficha wanachofanya Bungeni ni kina nani? Na kama kuna wabunge wa upinzani wanaofikiri hili ni jambo jema wasimame na waseme sasa; kama wapo wabunge wa CCM wanaamini kuwa hili ni jambo jema wasimame na wajitaje kwa majina yao Bungeni kuwa wanaunga mkono kuwaficha wananchi waliowaajiri kujua nini wanafanya.
Angalau tutawajua wachawi wetu kwa majina yao!
Na. M. M. Mwanakijiji
Kama kuna dhambi waliwahi kufanya basi dhambii hii itakuwa kubwa mmno na watahitaji hukumu stahiki 2015
Pendekezo lako zuri sana lakini sijui kama watakubali.....