Mkuu hii ya kuosha kwa kutimia maji ya limao unafanyaje?Gharama sana?? Mie nipo Mbeya kwa sasa, wanaposema ni nafuu wanamaanisha nini tena?? Anyway mie kabla sijaona makala yako na kupanua wigo wa ufahamu zaidi niliwahi tu kutengeneza locally kwa kuloweka ulezi mpaka ukachanua na kuku waliushambulia sana. So nikawa narudia na kurudia kwa kutumia biology ya secondary niliyosoma kuwa mbegu kama mbegu hujiwekea chakula chake cha siku saba wakati mimi nawapa kuku baada ya siku tano.
Pia kuna Doctor mmoja wa mifugo nilikutana nae yeye aliniongezea maarifa ya kuongeza ukuaji wa haraka wa hizi foda kwa kuweka nutrients fulani hivi zinaitwa DI Grow au Super Gro ambazo zenyewe hazina madhara kwa mimea, mifugo na binadamu. Nayo ilisaidia ulezi kukua kwa haraka ndani ya siku tatu nawapa kuku
Na mwisho alinifundisha kuepuka fangasi basi niwe naziosha mbegu kwa maji ya malimao ni hayo tu. Hii makala yako imenifungua mengi hasa baada ya kusoma kwenye mitandao zaidi ugomvi ni hizo nutrients, ina maana huwezi kutuwekea hapa formula yake tukasoma tukaelewa!! Ndiyo maana ya mitandao mkuu ni kurahisisha mambo ikiwemo muda na gharama