Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Gharama sana?? Mie nipo Mbeya kwa sasa, wanaposema ni nafuu wanamaanisha nini tena?? Anyway mie kabla sijaona makala yako na kupanua wigo wa ufahamu zaidi niliwahi tu kutengeneza locally kwa kuloweka ulezi mpaka ukachanua na kuku waliushambulia sana. So nikawa narudia na kurudia kwa kutumia biology ya secondary niliyosoma kuwa mbegu kama mbegu hujiwekea chakula chake cha siku saba wakati mimi nawapa kuku baada ya siku tano.

Pia kuna Doctor mmoja wa mifugo nilikutana nae yeye aliniongezea maarifa ya kuongeza ukuaji wa haraka wa hizi foda kwa kuweka nutrients fulani hivi zinaitwa DI Grow au Super Gro ambazo zenyewe hazina madhara kwa mimea, mifugo na binadamu. Nayo ilisaidia ulezi kukua kwa haraka ndani ya siku tatu nawapa kuku

Na mwisho alinifundisha kuepuka fangasi basi niwe naziosha mbegu kwa maji ya malimao ni hayo tu. Hii makala yako imenifungua mengi hasa baada ya kusoma kwenye mitandao zaidi ugomvi ni hizo nutrients, ina maana huwezi kutuwekea hapa formula yake tukasoma tukaelewa!! Ndiyo maana ya mitandao mkuu ni kurahisisha mambo ikiwemo muda na gharama
Mkuu hii ya kuosha kwa kutimia maji ya limao unafanyaje?
 
Wakuu kunasiku nilipost humu kuhusu Hydroponic techinology, Ila kama ilivyo kawaida yetu thread kama hizi huwa watu wanapotezea, Ila ukweli ni kwamba hii tekinolojia ni nzuri sana na inaweza kuwa ndo suluhisho pekee mpaka sasa la chakula cha mifugo.

Inaweza kukupunguzia gharama za chakula kwa 50% na kama tunavyo jua kwenye ufugaji hasa Kuku chakula kinabeba hadi asilimia 85 ya gharama zote za uendeshaji wa kuku.

110846c.jpg

Kanga wakiwa wanakula Hydroponic fodder.
DIY-Fodder4.jpg

Kuku wakila hydroponic fedder.

HYDROPONIC FODDER inaweza tumika kulishia aina zote za mifugo na hii ni njia rahisi sana na isiyo kuwa na gharama sana.
Samahani paka kuanza mradi kama huu unahitaji mtaji wa kiasi gani
 
Habari, napenda kufahamu kama kuna ameshafanya installation ya hydroponic fodder kwa DSM ama Maeneo ya Kibaha, nahitaji kujifunza na ikiwezekana nione jinsi ilivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umenena kweli ila sisi kwa sisi hatupendani licha ya wakenya wenyewe kuna watu anaweza kuwa anajua jambo linaloweza kuwasaidia na wengine ila hupendi ufahamu zaidi ya kujirushia kwenye hizi social media kuwa anafanya hydroponic na hata ukijaribu kutaka ujifunze bla bla nyingi mara unatakiwa uende shule ukasomee wakati nikitu ambacho yeye anaweza kukufundisha ila mtu hadi ufanikiwe unapitia mambo mengi mno kwa hizi jamii zetu za kiafrica

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaa Mkuu umeona mbali sana yaani hata Baba yako anaweza kukutia kauzibe usimzidi
 
Mkuu si kila chombo kinafaa kuoteshewa na ni lazima chombo kisicho ruhusu kutu, au bacteria na gangasi ambao ni hatari sana kama wataingia kwenye hayo mazao.

Mkuu inachukua siku 9 kuweza kuwa imekamilika kwa ajili ya kuwapatia NG'OMBE na kwa kuku ni siku tatu inatosha kabisa.

Maji unakuwa unaongeza ila si mengi sana, ila kama unalima mazao ya muda kama nyanya ndo unakuwa unayabadilisha na si kuyabadilisha unaweza fanya resaiko,

HAYO MAJANI UNAYO YAONA HAPO NDO YAMEFIKIA KUTUMIKA SI KWAMBA NI MPAKA IKOMAE IKAUKE NO,
kwa sehemu zenye shda ya maj hii inawezekana kwel? kiongoz
 
apo nakupata kumbe mbegu ni hz hz mtama ulez ngano sasa utawalsha majan kama apo pchan kangaa wakila majan au mpaka mavuno kwamba uvune mtama au ngano
 
Nilianza kwa kutumia DI Grow, baadaye nikaona bei yake iko juu .. lita moja 35,000/= Nikapata mkenya mmoja akanielekeza kutumia EM.1 na EMO; lita moja ni Tshs. 9,500/= na lita tano ndo Tshs. 40,000/=. Kwa sasa natumia EMO na mambo yanaenda vizuri sana.
Mkuu ucahnganyaji wa hivo virutubisho (vipimo) inakua kwa kiasi kipi kwa ujazo gani?
 
Asante sana kwa elimu hii. Nimepitia uzi wote na kutafuta taarifa zingine. Hii kitu nimegundua unaweza ifanya kwa kutumia resources ulizonazo.

Ninafanya majaribio kwa kilo mbili hizi za ngano nione matokeo yake yakoje.

Process nayotumia

1. Kuloweka ngano kwa masaa 4 ili kutoa uchafu wa nafaka isiyofaa. Ukiloweka uchafu unaelea, unautoa.

2. Vundika kwa masaa 48-INCUBATION. Unapovundika hakikisha unatumia ndoo ya plastic ili kuepusha kutu. Na iwe na matundu juu kwa ajili ya kupitisha hewa, sababu process hii inahitaji hewa ya oxygen.

3. Baada ya masaa 48. Unaanza kuotesha.

Unatumia tray ya plastic au aluminium(kuepusha kutu). Unapojaza tray, mjazo wa mbegu usizidi nusu inch, na pia tray isizidi inchi 2. Eneo halipaswi kuwa giza na lisipate mwanga wa moja kwa moja. Unakuwa unazinyunyuzia maji kila baada ya masaa matatu, day time, ili kupata unyevunyevu. Tray iwe na matundu pembeni upande mmoja ili maji yatoke. Kuepusha fungus.

Mategemeo baada ya siku Nne unaweza anza wapa kuku.

Nitatoa mrejesho kadri navyoendelea.

Nililoweka jana saa 5 asubuhi na kuvundika saa 9 mchana. So kesho saa 9 mchana masaa 24 yatakuwa yamekamilika. Nategemea kuotesha.
IMG_20210512_145701_288.jpg
IMG_20210512_145918_881.jpg
IMG_20210512_145923_405.jpg
 
NAUZA BIASHARA YA CAR WASH:

LOCATION: KINONDONI BLOCK 41
NAMBA YA SIMU: 0717 26 33 77

MAELEZO:

MACHINE ZOTE, UJENZI, VYOMBO, SIMTANK, KODI n.k JUMLA: TZS 7,000,000
NIMEBAHATIKA KUPATA KAZI SERIKALINI NA KITUO CHANGU KIKO MKOANI, SO NIMEAMUA KUUZA HII BIASHARA.
 
Back
Top Bottom