Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Kifo hakizoeleki. Kila mmoja anayo namna yake ya kuonyesha huzuni yake baada ya kufiwa; kwa mfano, wengine hulia kwa kupiga kelele, japo wengine hukaa kimya. Huzuni ni kitu kisichoonekana kwa macho, na mara nyingi huwaweka wahuzunikao kwenye hatari ya kupata sononi na madhara mengine ya kisaikolojia. Yafuatayo ni maneno ya faraja kwa mtu mwenye huzuni kubwa ya kufiwa. Mwandishi wa awali ni GSnow wa Reddit. Maandishi haya yamesambazwa sana mtandaoni, wengi wakisema yamewasaidia wao au wawapendao kukabiliana na huzuni kuu ya kufiwa. Alikuwa akimjibu mtu aliyesema, Rafiki yangu amefariki saa hii, nami sina hali. Hii hapa tafsiri ya Kiswahili:
Haya, inaenda hivi. Umri wangu umeenda. Hiyo maana yake ni kwamba nimeweza kuishi (mpaka sasa) na watu wengi ninaowafahamu na kuwapenda hawakuweza. Nimepoteza marafiki, mabesti, ninaowafahamu kidogo, wafanyakazi wenzangu, mababu na mabibi, mama, jamaa, walimu, waelekezi, wanafunzi, majirani, na kundi kubwa la watu wengine. Sina watoto, na siwezi kueleza machungu ya kufiwa na mtoto. Lakini haya ndio mawazo yangu.
Natamani kusema unaweza kuzoea kufiwa. Sikuweza. Na sitaki. Inabomoa tundu kubwa ndani yangu wakati wowote nimpendaye anapofariki, bila kujali namna gani. Lakini sitaki iwe "sijali". Sitaki iwe ni jambo la kupita tu. Makovu yangu ni ushuhuda wa upendo na uhusiano niliokuwa nao kwa ajili ya au na mtu huyo. Na kama kovu ni kubwa, ndivyo ulivyokuwa upendo. Acha liwe. Makovu ni ushuhuda wa uhai. Makovu ni ushuhuda kwamba naweza kupenda sana na kuishi kwa kuzama ndani sana na kujeruhiwa, na hata kutobolewa, na kwamba naweza kupona na kuendelea kuishi na kuendelea kupenda. Na nyama ya kovu ni imara sana kuliko ile iliyokuwapo awali. Makovu ni ushahidi wa uhai. Makovu huchukiza wale tu wasioweza kuona.
Kuhusu huzuni, utagundua huja kama mawimbi. Wakati jahazi linapozama, unazama maji, huku ukizungukwa na vipande mbalimbali vya jahazi vinavyokuzingira. Kila kitu kinachoelea karibu nawe kinakukumbusha uzuri na ukuu wa jahazi lilivyokuwa, na sasa halipo. Na kitu pekee unachoweza kufanya ni kuelea. Unapoona kipande cha jahazi na unakishikilia kwa muda. Inaweza kuwa kitu halisi. Inaweza kuwa kumbukumbu ya siku mlipofurahi au picha. Pengine ni mtu ambaye naye pia anaelea. Kwa muda, kitu pekee unachoweza kufanya ni kuelea. Kubakia hai.
Awali, mawimbi ni makubwa urefu wa futi 100 na yanakupiga bila huruma. Yanakuja kila baada ya sekunde 10 na hayakupi muda hata wa kuvuta pumzi. Kitu pekee unaweza kufanya ni kubakia ulivyo na kuelea. Baada ya muda, pengine majuma, pengine miezi, unaweza kubaini kwamba mawimbi bado ni ya futi 100, lakini yanakuja kwa kuchelewa zaidi. Na yajapo, bado hukutandika vilivyo na kukuyumbisha. Lakini wakati hayapo, unaweza kuvuta pumzi, na kuendelea na maisha. Huwezi kujua nini kitaibua tena huzuni. Inaweza kuwa ni wimbo, picha, makutano ya mitaa, harufu ya kikombe cha kahawa. Inaweza kuwa kitu chochote... na wimbi linakutandika kisawasawa. Lakini baina ya mawimbi pana maisha.
Siku zikishaenda, na hii ni tofauti kwa kila mtu, unaweza kuanza kona mawimbi yako na urefu wa futi 80 tu. Au urefu wa futi 50. Na ingawa bado yanakuja, huchukua muda mrefu zaidi kuja. Unaweza kuyaona yakija. Siku ya kumbukumbu ya kifo, kumbukumbu ya kuzaliwa, au Krismasi, au kutua katika uwanja wa ndege fulani. Unaweza kuliona likija, na kwa sehemu kubwa, kujiandaa. Na pindi likutandikapo, unajua kwamba unalo tumaini la kutokea upande wa pili. Ukiwa umeloa, harijojo, ukishikilia kipande cha jahazi, lakini utatoka salama.
Sikiliza maneno ya mzee. Mawimbi hayasiti kamwe kuja, na kiaina hutaki yaache. Lakini unaelewa kwamba utasalimika nayo. Na mawimbi mengine yatakuja. Na hayo pia utasalimika nayo. Na ukiwa na bahati, utakuwa na makovu mengi kutoka kwa mapendo mengi. Na majahazi mengi yaliyozama.
==============

====================