Huyu ni wakuoa kweli?

Huyu ni wakuoa kweli?

Ni kama vipi na kama zipi??

Kwahiyo kukataa wewe kumbusu ni sifa ya kiume yaani kwamba wanaume huwa mnakataa kubusiwa na wanawake??
Hapana
nadhan nkisema uromantic wa kike unaelewa
 
Dah! yan huyu angekua hivi alivo afu akawa na zile basics manner zote za kike angekua moto sana
Ushauri wangu nna 14yrs kwenye ndoa! Kabla ya ndoa kujua tabia za mwenzio 100% ni ngumu sana! Angalia kuna wanawake ambao akija kwako hatafanya chochote yaani hagusi sahani wala kijiko mtagegedana ataoga ataondoka! Utasema mwanamke huyu hafai lkn hujawahi kaa nae hata kumwambia mbona ukija kwangu hujishughulishi hata jikoni! Ana sababu zake za msingi ukimsikiliza. Mwingine anaona anajituma bure uhakika wa ndoa upo? Kaona dalili za kuwa wengi wanakuja hapo! Lkn huyu huyu ukishamuoa sasa anajua mji ni wake utashangaa mwenyewe! Unapooa angalia unaoa mwanamke aina gani na anatoka ukanda upi?. Sijataja kabila lkn ukanda. Hiyo kanda unayotaka oa wewe huko ubabeni halafu mfanyabiashara lazima atakuwa business oriented na independent. Usitegemee utegemezi sana na heshima zile za mama zetu. Kubali lifestyle hiyo au tafuta wale wa kanda za nyanda za juu kusini wanaopiga na magoti kabisa. Tambua kuna vitu vinafanyika wakati wa uchumba tu ndani ya ndoa huwezi fanya tena. Mfano nilikuwa nasubiriwa hata saa saba usiku ili mradi tulale muda sawa lkn baada ya ndoa asubuhi ndo naulizwa ulirudi saa ngapi jana. Nilikuwa nikirudi job anakwenda mwenyewe kuniwekea msosi though hatukuwa na microwave. Sasa hivi nakuta chakula kwenye hotpot mezani mzee baba napasha mwenyewe kwenye microwave napiga msosi nasindikizwa na shangwe za watoto mwenzangu yupo kwenye biashara akitafuta mshiko. In a nutshell maisha ya ndoa mkishapata watoto mnakuwa na majukumu mazito kulea, kusomesha, mambo mengi ya show off hamyakumbuki tena. Nilikuwa na dem matata sana alikuwa akinifuata posta kila nnapotoka job namkuta nje ananisubiria, tutapiga story weee atanifuata ninakokwenda ila nikimpa tu mshiko atanitafutia hata daladala la kupanda yeye anasepa zake. Huwezi kumwelewa mwanamke 100%
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom