Huyu ndugu kanogewa, tunamtoaje huku?

Huyu ndugu kanogewa, tunamtoaje huku?

Citizen B

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2019
Posts
6,804
Reaction score
9,410
Good day citizens.

Mimi sio mwandishi wa stori na sina kipaji hicho, sina kipaji cha utunzi wala uandishi wa stori wowote, so I bear witness kila kitu nachoenda kuandika hapa ni ukweli mtupu niliosimuliwa na huyu ndugu yangu.

Nina ndugu yangu anaitwa Majele, sasa huyu majele kwao ni kijijini sana kule Mwanza ndani ndani, story yake iko ivi:

Mimi Majele nilizaliwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanne, baba yangu alitengana na mama kipindi bado mdogo na kisha kutukataa sisi watoto, hii ilimfanya mama kurudi kwa mama yake (bibi yetu) kijijini na ndipo tulipokulia. Bibi naye alikuwa mjane hivyo tuliishi na bibi na mama tu.

Maisha yangu yote yalikuwa kijijini na nilisoma hapo mpaka kumaliza elimu yangu ya sekondari na kuanza maisha ya kujitafutia kipato nikiwa bado nyumbani.

Watu wengine niliowajua ni majirani wa kijijini na babu yetu mzaa baba aliyekuwa anaishi kijiji kingine cha mbali (Misungwi).

Huyu babu aliitwa Majele (nilichukua jina lake) na alikuwa anapenda kuja kijijini kwetu kututembelea mara moja au mbili kwa mwaka.

Mara nyingi alikuwa akifika nyumbani alimlaumu sana bibi kwanini wajukuu zake (sisi hapa) hajawahi kuwapeleka Misungwi kumtembelea bibi mara nyingi alikuwa anacheka na kumpuuzia tu.

Babu alikuwa akija kijijini majirani wetu walikuwa wanafurahi sana pamoja na wanakijiji wengine na walimpokea kwa furaha, pia siku akiondoka walikuwa lazima wampe vyakula kama mchele, karanga na kumshukuru. Tukimuuliza babu inakuwaje hawa watu wanakupenda hivi, alikuwa anajibu kirahisi rahisi tu kuwa anajuana nao toka kabla hatujazaliwa.

Mwaka jana mwezi wa sita nikiwa tayari mtu mzima mwenye miaka 25, Babu alikuja tena nyumbani kututembelea. Baada ya chakula cha usiku mida ya saa mbili nilikuwa nimekaa naye kwa nje tunapiga stori ndipo akaanza kuongea vitu vya ajabu, akaanza kusema "Mjukuu wangu, hapa nawaonea sana huruma kwasababu kuanzia bibi yenu, mama yenu mpaka nyie wote hamna kitu" nikamuuliza kwanini babu akasema "Majirani zenu hawa huwa wanakuja usiku kuwachezea wanawatoa nje na kuwafanyia uchafu wa kila aina" nikashangaa sana akaendelea kusema "mbaya zaidi wote familia hii hakuna hata mmoja mtaalamu kwahiyo wanawachezea sana"

Nikabaki kushangaa lakini sikumuelewa vizuri mpaka akaondoka nyumbani aliniachia maswali mengi natafakari.

Mwezi uliofuata wa saba akaja mtu mgeni pale nyumbani wa kijijini akiwa na shida na babu Majele. Bibi akamuambia hayupo, amesharudi kwake Misungwi. Yule jamaa akasisitiza sana kuwa ana shida naye na ilibidi bibi amuelekeze jinsi ya kumpata akienda huko Misungwi. Sasa kwasababu babu huwa analalamika sana kuwa wajukuu wake huwa hatumtembelei, bibi akanilazimisha niende na huyo mgeni Misungwi ili tukifika huko nitapitia hiyo hiyo gia na kumsalimia babu. Baada ya kusisitiza sana,nikakubali na tukapanga kesho yake tutaanza safari.

Kwakuwa kutoka kijijini kwetu mpaka Misungwi ni mbali na siyo safari ya siku moja tukapanga kuwa tutoke kijijini tufikie mjini halafu keshokutwa yake tutoke mjini mpaka Misungwi. Kwakuwa tulitaka ku-save cost tukapanga tukifika mjini tutafikia kwa kaka yetu Citizen B ili tupate sehem ya kujistiri kwa usiku mmoja.

Tulifanya hivyo na kesho kutwa tukawa tumefika kijijini misungwi kwa babu yangu Majele.

Babu alipotuona tu alifurahi sana na kutukaribisha kwa furaha isiyo kifani akiniambia "Hatimaye mjukuu wangu leo umefika nyumbani kwangu"

Baada ya kukaribia yule jamaa alieleza shida zake kwa babu akisema kuwa anasumbuliwa na wachawi sana huko kijijini anahitaji dawa. Babu akamwambia asijali atamtengenezea.

Usiku wake tukiwa tumelala mida ya saa saba usiku nikasikia babu ananiita ananiambia "Mjukuu wangu amka! Amka! Tumeshachelewa kwanza amka!"

Nikamuuliza tumechelewa kwenda wapi babu? Akasema "wewe amka! tumeshachelewa''

Nikaamka na kuanza kumuuliza tunaenda wapi akasema "wewe mjukuu wangu nakukubali ni mwanaume sio kama wadogo zako, huyu jamaa uliyekuja naye ni mpumbavu hawezi kufunga safari yote hiyo halafu anakuja kunilazimisha nimpe hizo dawa ambazo sitaki kumpa. Mimi nitampa zingine tu, siyo alizoomba.

"Sasa huyu mpumbavu ngoja tumuache hapa amelala sisi twende" muda huo anaongea hayo huku ameshaanza kunichanja chale chache mwilini, alipomaliza kuongea hayo akanichanja chale machoni na hapo hapo Lo! And behold pakawa peupe kama mchana, nikawa naona kila kitu kama mchana ingawa ilikuwa saa saba usiku.

"Tuondoke mjukuu wangu, nifuate" alisema hayo babu huku akiondoka nje ya nyumba. Namimi nikawa namfuata nikamuambia "Babu mimi naogopa tunaenda wapi?" Akasema "Aaah kumbe wewe huna roho ngumu basi turudi! turudi" Tukarudi nyumbani akachukua dawa fulani akanichanjia akasema hii itaondoa uoga wako wote, hapo hapo nikawa sina uoga tena nikaanza kumfuata babu.

Maeneo aliyokuwa akiishi ni kijijini sana na kulikuwa hakuna dalili ya umeme ni mapori tu na mashamba na milima.

Nikamfuata nakuanza shangaa sio mbali na nyumbani kwake nikakuta kuna nyumba kubwa nzuri ya kisasa, imepambwa na watu walikuwa wengi sana mithili ya harusi. Watu walikuwa wanasherekea wakiwa uchi wa mnyama.

Tulipofika pale, walipomuona babu wote wakasimama na kutoa ishara ya heshima kwa babu. Mtu mmoja nikamsikia anasema "karibu mgeni Majele kutoka kijiji X" nikashangaa ni nani huyo ananijua jina na kijiji nachotokea?

Tulipokaribishwa pale, babu akapewa kiti cha ukuu akakalia (ikumbukwe wote tulikuwa uchi kasoro babu alikuwa amevaa lijoho jeusi) akaombwa amtambulishe mgeni ambaye ni mimi.

Nilishtuka sana pale babu alipoanza kusema:

"Ndugu zangu huyu ni mjukuu wangu Majele ambaye amechukua jina langu, huyu mimi nilimchagua kipindi bado wadogo sana huko kijijini kwao. Huyu ndiye atakuja kurithi mikoba yangu siku nikifa"

Baada ya utambulisho kilichofuata ni wale watu kila mmoja alikuwa ananizonga zonga na kuonesha dalili ya kuniona kama sitaweza kurithi mikoba ya babu kwasababu mimi ni mgeni wa huu ulimwengu.

Kipindi hayo yote yanaendelea Babu akaanza kutoa order pale kuhusu ile sherehe kuwa kuna wengine wanatakiwa wafate viti vya sherehe, wengine wafate vyombo vya kupikia na wengine wafate mboga ya sherehe. Mimi nikapangwa kwenye kundi la wanaofata mboga ya sherehe jumla tulikuwa wanne pamoja na kiongozi wetu wa kundi.

Tukamfuata yule kiongozi tukaenda kupanda fisi kila mtu akakalia fisi yake ,yule kiongozi akasema tumfatilie nyuma"

ITAENDELEA
Mshana Jr
 
Back
Top Bottom