Huyu ndugu kanogewa, tunamtoaje huku?

Huyu ndugu kanogewa, tunamtoaje huku?

Nitarudi
Good day citizens.

Mimi sio mwandishi wa stori na sina kipaji hicho, sina kipaji cha utunzi wala uandishi wa stori wowote, so I bear witness kila kitu nachoenda kuandika hapa ni ukweli mtupu niliosimuliwa na huyu ndugu yangu.

Nina ndugu yangu anaitwa Majele, sasa huyu majele kwao ni kijijini sana kule Mwanza ndani ndani, story yake iko ivi:

Mimi Majele nilizaliwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanne, baba yangu alitengana na mama kipindi bado mdogo na kisha kutukataa sisi watoto, hii ilimfanya mama kurudi kwa mama yake (bibi yetu) kijijini na ndipo tulipokulia. Bibi naye alikuwa mjane hivyo tuliishi na bibi na mama tu.

Maisha yangu yote yalikuwa kijijini na nilisoma hapo mpaka kumaliza elimu yangu ya sekondari na kuanza maisha ya kujitafutia kipato nikiwa bado nyumbani.

Watu wengine niliowajua ni majirani wa kijijini na babu yetu mzaa baba aliyekuwa anaishi kijiji kingine cha mbali (Misungwi).

Huyu babu aliitwa Majele (nilichukua jina lake) na alikuwa anapenda kuja kijijini kwetu kututembelea mara moja au mbili kwa mwaka.

Mara nyingi alikuwa akifika nyumbani alimlaumu sana bibi kwanini wajukuu zake (sisi hapa) hajawahi kuwapeleka Misungwi kumtembelea bibi mara nyingi alikuwa anacheka na kumpuuzia tu.

Babu alikuwa akija kijijini majirani wetu walikuwa wanafurahi sana pamoja na wanakijiji wengine na walimpokea kwa furaha, pia siku akiondoka walikuwa lazima wampe vyakula kama mchele, karanga na kumshukuru. Tukimuuliza babu inakuwaje hawa watu wanakupenda hivi, alikuwa anajibu kirahisi rahisi tu kuwa anajuana nao toka kabla hatujazaliwa.

Mwaka jana mwezi wa sita nikiwa tayari mtu mzima mwenye miaka 25, Babu alikuja tena nyumbani kututembelea. Baada ya chakula cha usiku mida ya saa mbili nilikuwa nimekaa naye kwa nje tunapiga stori ndipo akaanza kuongea vitu vya ajabu, akaanza kusema "Mjukuu wangu, hapa nawaonea sana huruma kwasababu kuanzia bibi yenu, mama yenu mpaka nyie wote hamna kitu" nikamuuliza kwanini babu akasema "Majirani zenu hawa huwa wanakuja usiku kuwachezea wanawatoa nje na kuwafanyia uchafu wa kila aina" nikashangaa sana akaendelea kusema "mbaya zaidi wote familia hii hakuna hata mmoja mtaalamu kwahiyo wanawachezea sana"

Nikabaki kushangaa lakini sikumuelewa vizuri mpaka akaondoka nyumbani aliniachia maswali mengi natafakari.

Mwezi uliofuata wa saba akaja mtu mgeni pale nyumbani wa kijijini akiwa na shida na babu Majele. Bibi akamuambia hayupo, amesharudi kwake Misungwi. Yule jamaa akasisitiza sana kuwa ana shida naye na ilibidi bibi amuelekeze jinsi ya kumpata akienda huko Misungwi. Sasa kwasababu babu huwa analalamika sana kuwa wajukuu wake huwa hatumtembelei, bibi akanilazimisha niende na huyo mgeni Misungwi ili tukifika huko nitapitia hiyo hiyo gia na kumsalimia babu. Baada ya kusisitiza sana,nikakubali na tukapanga kesho yake tutaanza safari.

Kwakuwa kutoka kijijini kwetu mpaka Misungwi ni mbali na siyo safari ya siku moja tukapanga kuwa tutoke kijijini tufikie mjini halafu keshokutwa yake tutoke mjini mpaka Misungwi. Kwakuwa tulitaka ku-save cost tukapanga tukifika mjini tutafikia kwa kaka yetu Citizen B ili tupate sehem ya kujistiri kwa usiku mmoja.

Tulifanya hivyo na kesho kutwa tukawa tumefika kijijini misungwi kwa babu yangu Majele.

Babu alipotuona tu alifurahi sana na kutukaribisha kwa furaha isiyo kifani akiniambia "Hatimaye mjukuu wangu leo umefika nyumbani kwangu"

Baada ya kukaribia yule jamaa alieleza shida zake kwa babu akisema kuwa anasumbuliwa na wachawi sana huko kijijini anahitaji dawa. Babu akamwambia asijali atamtengenezea.

Usiku wake tukiwa tumelala mida ya saa saba usiku nikasikia babu ananiita ananiambia "Mjukuu wangu amka! Amka! Tumeshachelewa kwanza amka!"

Nikamuuliza tumechelewa kwenda wapi babu? Akasema "wewe amka! tumeshachelewa''

Nikaamka na kuanza kumuuliza tunaenda wapi akasema "wewe mjukuu wangu nakukubali ni mwanaume sio kama wadogo zako, huyu jamaa uliyekuja naye ni mpumbavu hawezi kufunga safari yote hiyo halafu anakuja kunilazimisha nimpe hizo dawa ambazo sitaki kumpa. Mimi nitampa zingine tu, siyo alizoomba.

"Sasa huyu mpumbavu ngoja tumuache hapa amelala sisi twende" muda huo anaongea hayo huku ameshaanza kunichanja chale chache mwilini, alipomaliza kuongea hayo akanichanja chale machoni na hapo hapo Lo! And behold pakawa peupe kama mchana, nikawa naona kila kitu kama mchana ingawa ilikuwa saa saba usiku.

"Tuondoke mjukuu wangu, nifuate" alisema hayo babu huku akiondoka nje ya nyumba. Namimi nikawa namfuata nikamuambia "Babu mimi naogopa tunaenda wapi?" Akasema "Aaah kumbe wewe huna roho ngumu basi turudi! turudi" Tukarudi nyumbani akachukua dawa fulani akanichanjia akasema hii itaondoa uoga wako wote, hapo hapo nikawa sina uoga tena nikaanza kumfuata babu.

Maeneo aliyokuwa akiishi ni kijijini sana na kulikuwa hakuna dalili ya umeme ni mapori tu na mashamba na milima.

Nikamfuata nakuanza shangaa sio mbali na nyumbani kwake nikakuta kuna nyumba kubwa nzuri ya kisasa, imepambwa na watu walikuwa wengi sana mithili ya harusi. Watu walikuwa wanasherekea wakiwa uchi wa mnyama.

Tulipofika pale, walipomuona babu wote wakasimama na kutoa ishara ya heshima kwa babu. Mtu mmoja nikamsikia anasema "karibu mgeni Majele kutoka kijiji X" nikashangaa ni nani huyo ananijua jina na kijiji nachotokea?

Tulipokaribishwa pale, babu akapewa kiti cha ukuu akakalia (ikumbukwe wote tulikuwa uchi kasoro babu alikuwa amevaa lijoho jeusi) akaombwa amtambulishe mgeni ambaye ni mimi.

Nilishtuka sana pale babu alipoanza kusema:

"Ndugu zangu huyu ni mjukuu wangu Majele ambaye amechukua jina langu, huyu mimi nilimchagua kipindi bado wadogo sana huko kijijini kwao. Huyu ndiye atakuja kurithi mikoba yangu siku nikifa"

Baada ya utambulisho kilichofuata ni wale watu kila mmoja alikuwa ananizonga zonga na kuonesha dalili ya kuniona kama sitaweza kurithi mikoba ya babu kwasababu mimi ni mgeni wa huu ulimwengu.

Kipindi hayo yote yanaendelea Babu akaanza kutoa order pale kuhusu ile sherehe kuwa kuna wengine wanatakiwa wafate viti vya sherehe, wengine wafate vyombo vya kupikia na wengine wafate mboga ya sherehe. Mimi nikapangwa kwenye kundi la wanaofata mboga ya sherehe jumla tulikuwa wanne pamoja na kiongozi wetu wa kundi.

Tukamfuata yule kiongozi tukaenda kupanda fisi kila mtu akakalia fisi yake ,yule kiongozi akasema tumfatilie nyuma"

ITAENDELEA
Mshana Jr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunasubiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gegelaga makanza ga guchagula bhatawala, matanjago angu?
 
Hivi kuna sehemu inaongoza kwa uchawi Tanzania kama kanda ya ziwa
 
Mshasa Jr umeanza na story zako.
 
Kwanza ni hadithi uliyoitunga wewe, kisha unaikana na kudai ulisimuliwa si ya kwako!

Kwanini msimuliaji usimuelekeze Jf ilipo ili aje yeye mwenyewe atusimulie?

Unasimulia kwa umahiri sana, lakini kwa sababu ni hadithi ya mtu mwingine, inaniwia vigumu kuendelea kusoma.

Maana kama kuna sehemu nitakayoshindwa kuielewa, wewe hautanisaidia kujibu kwa kuwa na wewe ulisimuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza mimi alinisimulia kwasababu tu.
Pili kuna maswali namimi nilikuwa namuuliza ananijibu,unaweza ukaniuliza kama niliuliza namimi nitakujibu ila kama sikuliuliza nitakuambia sikufikiria ilo swali.
Kwanza ni hadithi uliyoitunga wewe, kisha unaikana na kudai ulisimuliwa si ya kwako!

Kwanini msimuliaji usimuelekeze Jf ilipo ili aje yeye mwenyewe atusimulie?

Unasimulia kwa umahiri sana, lakini kwa sababu ni hadithi ya mtu mwingine, inaniwia vigumu kuendelea kusoma.

Maana kama kuna sehemu nitakayoshindwa kuielewa, wewe hautanisaidia kujibu kwa kuwa na wewe ulisimuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi,Tukapanda kila mtu fisi yake tukaanza kumfatilia jamaa kwa nyuma,Asikuambie mtu vile vidude vinakimbia hatari.
Baada ya mda mfupi tu tukawa tumeshafika destination, yule kiongozi akaamuru tusimame tulikuwa nje kidogo ya mji wa mtu.
Yule kiongozi akachukua dawa fulani kama unga akaurusha kwenye ule mji,tukatulia kama dakika tano hivi akasema sasa twende...tukashuka fisi tukaingia ndani ya huo mji(ni kijijini hamna fence)... Tukaenda moja kwa moja mpaka kwenye banda la mbuzi,tukajichagulia walionona kila mmoja akabeba wa kwake tukatoka kwenye banda,kwa nje kulikuwa kuna mbwa kama watano hivi wamelala tu wanatuangalia hawafanyi kitu. Nikataka nimbusu mmoja.
Tukabeba mbuzi zetu tukaenda nazo hadi pale tulipopaki usafiri wetu tukapanda tukasogea kwa mbali kidogo yule kiongozi akachukua tena dawa fulani kama unga hivi akarusha tena kwenye ule mji na kuamuru tuondoke,,ule unga ulipofika kwenye ule mji wale mbwa wakaanza kubweka sana wanakimbia kama kuja upande wetu,sisi takapanda usafiri dakika sifuri tumeshawaachia manyoya tukajikuta tumeshafika kwenye sherehe yetu(ngoma).
Tulipofika tukakuta mambo ni mambo akina mama wamewasha majiko wako wanapika,wababa wanafurahi na kupiga stori,mboga tukakabidhi,chakula kikapikwa tukala na burudani zingine..baada ya kula tukaanza kucheza mziki...mziki wa ajabu na hata wanacheza sikuelewa hizo style lakini nikawa nawaiga tu na kufata step zao...tumecheza sana ngoma ila macho yangu yalikuwa kwa binti mmoja mweupee size yangu,binti bado mbichi kabisa matiti yamesimama nikawa namshangaa sana na kumtamani...tumecheza sana ngoma baadaye watu wakawa wanaenda kwa babu wanaeleza matatizo yao.
Mimi nikawa namsikiliza mama mmoja anamuambia babu kuwa kuna mji fulani umemshinda, baba wa ule mji ni adui yake na kila akienda anashindwa kuingia,inaonekana yule baba dawa zake alizozindika zina nguvu sana....Babu akampa dawa fulani za kumsaidia aingie kwenye huo mji. Kisha babu akanifata akanipa fimbo yake.
Baadaye watu tukagawana makundi,mimi nikawa kundi moja na yule mama na yule binti mweupe na jamaa mwingine jumla tukawa wanne,kiongozi wetu akiwa yule mama tukaanza kumfuata mpaka kupanda ungo,wote wanne tukaenea kwenye kale kaungo, hao dakika mbili nyingi tukawa tumefika kwenye huo mji aliokuwa anausemea huyo mama.
Tulipofika kwa juu yule mama akapulizia dawa fulani kama unga unga juu ya ule mji,,mara ya kwanza ulienda ukamwagika....akachukua tena ule aliopewa na babu safari hii akapualizia haukumwagika lakini ukatanda kwa juu ya nyumba,,hii ikawa kama ishara kuwa hapa sasa tunaweza kuingia kwenye huu mji.
Tukashuka tukaingia ndani ya mji alianza yule mama...akaenda mlangoni akageuzia matako huyo tayari kaingia,akafuata yule binti akageuzia matako mlango akasugua kidogo huyo kaingia,akafata yule jamaa namimi nikafata,,,nashangaa ile nageuza matako ile nasugua kidogo tu nikajikuta niko ndani ya nyumba.
Kuingia ndani nakuta yule mama alishaingia mpaka chumba cha mwenye mji ameshambeba ameanza kutoka naye,wale wengine nao wakaingia kwenye vyumba vingine wakabeba watu na kutoka nao(kuna dawa ukibeba mtu anakuwa mwepesi kama mshumaa unaweza shangaa mbaba bonge anabebwa na katoto ka darasa la pili)
Tukatoka nje na hao watu,mimi nikawa nafuatilizia tu kwa wenzangu. tuliwalaza pale nje na kuanza kuwakanyaga,kuwakalia,kuwakojolea na kuwatemea mate....yule mama akawa anafurahi sana anasema "leo nimekuweza mbwa wewe" tumewachezea tumefurahi sana hadi tukachoka,ikafika mda wa kuondoka sasa ikabidi tuwarudishe twende...ile tumeingia ndani tukawarudisha kitandani sasa tukarudi ili tutoke twende...tumefika sebuleni nikaona wenzangu kila mmoja yupo ukutani anasugua matako,namimi nikaiga namimi nikakaa ukutani nasugua,ikawa ni mwendo wa kusugua ukuta na kubadilisha position tu,,,unasugua hapa unamaliza unasugua tena pale, tumesugua sana kadri mda unavyozidi kwenda naona wenzangu woga,frustration, panic inawaingia wanaendelea kusugua tu namimi nawaiga.Tulisugua sana kama lisaa lizima hadi saa 11 ikawa inakaribia. kengele ya kutukumbusha jua linataka litoke ikawa inalia kwa nguvu.
Baada ya kusugua sana ikabidi nivunje ukimya niwaulize bandugu "mbona mnasugua ukuta sana halafu sioni chochote?" Yule mama akanijibu "ina maana wewe huelewi?? Hatuuoni mlango"
Nikashangaa sana kwasababu mda wote huo mimi mlango nilikuwa nauona nikawaambia "mbona mlango huo hapo?" Wakauliza ukowapi mimi nikausonta kwa fimbo ya babu,kila mtu akauona hao wakaenda kusugua pale wakatoka.
Tulipotoka tukapanda ungo wetu na kurudi kule kwenye ngoma. tulipofika tulikuta kila mtu yupo wakawa wanatuuliza kwanini tumechelewa yule mama akawaambia "yaani leo almanusra tukamatike isingekuwa huyu kijana majele leo tungeumbuka,tulikosa mlango wa kutokea yeye ndo akatuonesha"
Watu wote wakaanza kunishangilia,kunisifu na hapo hapo babu akanichanja cheo nikawa nimepanda cheo cha tembo.
Baadaye nikarudi na babu nyumbani njiani akawa ananielekeza baadhi ya dawa na jinsi ya kuzitumia mara ghafla tumeshafika nyumbani tukamkuta yule jamaa mgeni amelala fofofo anajigeuza tu.Nikarudi nikalala nae ilipofika saa 12 jamaa akaamka akaanza kunilaumu nalala sana wakati nipo ugenini,mimi moyoni nikawa najisemea hiiiiiiiiii ahaa huyu hajui tu.
Kesho yake tukakaa kidogo babu akampa yule jamaa dawa namimi akanielekeza baadhi ya dawa mchana tukaaga tuondoke,babu akaniuliza nitakuja lini tena nikamuambia asihofu nitakuja tu.
Tukarudi tena mjini tukafikia kwa Citizen B ili kesho kutwa yake turudi kijijini kwetu.
Usiku wake baada ya kula na kwenda kulala mida ya saa 7 hivi mimi nikiwa nimelala na jamaa yangu chumba cha wageni nikaanza kusikia kengele ya kuita wachawi kwenye ngoma,nikaipotezea baada ya muda nikasikia sauti kama mlango unabamizwa kwa nguvu hivi kama fatuma,mara ghafla nikasikia watu wameingia sebuleni tena wanaongea kwa sauti sana utadhani wapo kariakoo halafu wako umbali wa mita mia....wakawa wanaongea wanasema "twende tukamchukue Kevin (mdogo wake Citizen B) wakaenda chumba chake wakamchukua wakampeleka sebuleni..
Wakaingia chumba chetu cha wageni mmoja akawa anasema " haya ni makina nani??" Wakataka kumbeba yule jamaa wakashindwa nikasikia wanasema "hili linani? Mbona la moto sana" wakaondoka wakarudi sebuleni. Mimi nikaamka nikachukua kibegi changu chenye dawa nilizopewa na babu,nikajipaka dawa fulan nikatoka nikawafata sebuleni.
Nikakuta wamemlaza pale chini kevin wanamvua nguo zote, mimi wakawa hawanioni,nikasikia yule kiongozi wao mmama anasema kama mmewashindwa hao wageni mleteni Citizen B hapa.
Nikaona huu ujinga sasa nikarudi chumbani nikachukua dawa fulani nikapita sebuleni hawanioni nikatoka hadi nje,nikaizungushia nyumba ile dawa halafu nikaanza kuponda bati...wakashtuka kuangalia nje kuna nini,ile wanajaribu kutoka wakashindwa...wakajua wamekamatika,,nikawaambia nani kawatuma?(wanasikia sauti tu) wakaanza kulia tusamehe baba sisi tumetumwa tu.
Nikasema nisubirini nakuja nikaanza kufata sauti iliko ngoma yenyewe,haikuwa mbali sana na pale tulipokuwa.
Nikafika kwenye ngoma kama kawaida nikakuta watu wengi wamekaa kwenye viti utadhani mkutano wa hadhara nilipofika tu nikaanza kusikia sauti "karibu mgeni Majele kutoka kijiji X"
Watu wote wakasimama na kuonesha ishara ya heshima kwangu mimi nikaenda direct mpaka kwa mkuu wao,nikakuta namzidi cheo akanipisha kiti nikakaa.
Nikawaambia watu wote wakae wasikilize kutoka kwangu,,,nikamuuliza yule mkuu
"wale watu mliowatuma ule mji wa Citizen B kuna kosa gani alishawafanyia?"
Yule mkuu akaanza kujikanyaga pale "wasamehe tu baba,wamekosea na hatukujua kama unakaa hapo" nikawaambia "yule bwana ana makosa gani mbona ni mtu mstaarabu sana?" Wakasema "wasamehe tu hawatarudia tena"
Nikasema sasa ili iwe onyo nataka niwafanyie kitu kibaya wale watu
Yule mkuu akawaombea sana msamaha nikamuambia basi twende naye mpaka tukawaone watu wake wanavyohangaika nilivyowafungia mle ndani.
Tukatoka pale kwenye ngoma, mimi na yule mkuu wao mpaka kwenye mji wa Citizen B tukakuta bado wamo ndani wanahangaika kutoka.
 
Back
Top Bottom