Huyu ndiye Ruge ninayemfahamu!

Kama Ruge anasimamia ukweli atueleze uhusika wake na Kinje kuhusu yule aliyepasukiwa na madawa South Afrika! Nini kilimsababisha akaingia gharama kuhakikisha mwili unarudi na kituo chake kutoka coverage ile? Ruge ni vizuri ukanyamaza kuna Mengi wasiyoyajua WENGI JUU YAKO, UKIBISHANA SANA WATAYAANIKA ITAKUWA SHEEEDA!
Ni umbea tu pelekeni ushaidi mahakamani sio kutuletea umbea huku jf.Story za Kwenye kahawa ndio hizi mnaongea mtadhani mnamaana
 
Miiko iwe upande wote,miiko gani wakati mtu anatumia rushwa ya ngono kwa wafanya kazi wake hadi anazaa nao.
Lete ushaidi wowote wa nani kafanyiwa hayo.Ni kosa kisheria rushwa ya ngono,peleka pccb ushaidi huo vinginevyo ni umbea
 
Kama 'yule bwana' na Ruge ni marafiki kwa nini Ruge hakumuita chemba wakamalizana kirafiki badala ya kumuexpose kwenye jamii?usidhan tunaakili za nyumbu !tunajua kilichokuwepo nyuma ya pazia!Ruge anatumiwa!ametumika!
Ruge alimpa muda yule bwana mpaka siku mbili yule bwana hakutokea unahisi tuna akili za kibashite
 
Kama 'yule bwana' na Ruge ni marafiki kwa nini Ruge hakumuita chemba wakamalizana kirafiki badala ya kumuexpose kwenye jamii?usidhan tunaakili za nyumbu !tunajua kilichokuwepo nyuma ya pazia!Ruge anatumiwa!ametumika!
Msitake nicheke Mimi, sio Bwana yule, kama Ruge anatumika na hao mnaowaita wa madawa ya kulevya Bwana yule angeshasema hivyo pale Satr TV na kuwataja hao wa madawa.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Hata kama kwa ubinadamu wetu tutatashindwa kusimama na huyu ndugu hususan kwa kipindi hiki yupo Mungu aliye hai atamtetea.

Ndio, Hakuna binadamu asiye na mapungufu, Ruge kama binadamu inawezekana ana mapungufu yake lakini katika hili suala la Clouds Vs "Yule Bwana" kwa binadamu mwenye akili za kawaida tu utakubaliana nami kwamba Ruge ameonyesha hekima na busara ya kiasi cha juu sana.

Alichoamua Kukisimamia Ruge ni kusema UKWELI, Ukweli kwamba "Yule Bwana" alikosea, pamoja na kwamba walikuwa marafiki lakini Ruge aliamua kusimama katika misingi ya ukweli, misingi ya kikazi, Kwamba "Yule bwana" alikosea. Kuna vitu wala havihitaji degree kuvielewa, yaani kule tu kwenda pale tena usiku tena na silaha bila mhusika kujua, na bila warrant ni kosa kisheria.

Leo baada ya kumsikia Ruge akijibu shutuma za "Yule Bwana" nimejisikia amani sana, Maana badalaa ya kujibu kwa jaziba, kwa matusi, kwa mhemko, Ruge kajishusha kaongea kwa ustaarabu kama binadamu, Pamoja na kuambiwa hana akili, anaimba ngonjera, na maneno mengine mengi ya kuudhi lakini jamaa kajibu ki proffesional na kwa unyenyekevu. U have my respect brother.

Mi nafikiri kama taifa kama tunakuwa na viongozi wa namna hii, ambao wanashindwa kuwa na akiba ya maneno na kuongea tu kama vijana wa mtaani bila kuangalia kuwa kuna watu wengi sana tunawaangalia ili kujifunza kwao, tutakuwa tunaelekea pabaya sana.

Unaweza kusema alionyeaha hekima na busara kwa sababu yeye ndiye aliyepangilia mpango mzima wa tukio. Waziri Mwakyembe atayaweka mambo wazi.
 
video yenyewe inaonesha afisa anaingia in a peace way,anasalimia wenyeji kwa kupungia mkono et uvamizi!!!
Umekariri uvamizi ni tukio la hamaki au taharuki? Wewe bwana yule asikudanganye utapata m.....Uvamizi ni tukio lolote la kwenda mahala bila taarifa na kuingia kinyume na utaratibu
 
Tukiachia mbali tuhuma za Bashite,
Mtu ambaye huwa simuamini kabisa ni Ruge, ni kwanini wengi wa wanaofanya nae kazi kwa karibu huishia kulalamika kudhurumiwa!?
Ila anajua kuongea vizuri aisee na anashawishi sana unapomsikiliza
Hizo kazi wasiokuwa na lawama ni wahindi kwa kuwa wanawanyonya ipasavyo.Lini mhindi akaleta mazoea na mbongo.Ni tatizo kufanya kazi na mbongo ukaweka mazoea utalaumiwa sana.Mbongo hakuna kuchekacheka nae uwapo ktk kazi.Sasa ruge akujua hayo
 
Ruge ni mnafiki Mkuu, alipokubali kutumikia magwiji wa Dawa za kulevya kwa kusingizia kituo chake kimevamiwa.

Kushindwa kuthibitsha tukio hilo, au kufungua jalada polisi
Leo nimeamini kweli kuna binadamu na mifugo..

Ulichoandika kinaonesha wewe sio binadamu!
Mwenye tuhuma za kuvamia kituo hajakanusha lakini mifugo yake inakanusha licha ya kuwepo kwa ushahidi usioacha shaka yeyote!

Kweli kuna binadamu na mifugo!
 
Achana na Chuki binafsi mbona RC Jana kajieleza vizuri sana na mwenye kutaka kuelewa tulimuelewa sana hatukutegemea kuwa hizo zilikuwa fitina za madawa ya kulevya tumuache achape kazi mbona mazuri haya sifiwi acheni fitina Mungu anawaona
 
Ruge ni mnafiki Mkuu, alipokubali kutumikia magwiji wa Dawa za kulevya kwa kusingizia kituo chake kimevamiwa.

Kushindwa kuthibitsha tukio hilo, au kufungua jalada polisi
Uthibitisho gani unauhitaji wewe?
"Yule bwana" jana kakiri kuwa alivamia na clip za video zimeonyesha kuwa kavamia,wewe unataka nini tena?
Ruge aende Polisi akamshitaki nani kwa nani?
Hivi kwa akili ya kawaida tu,unaweza kumshitaki mtu kwa kosa la kuvamia ilihali wenye mamlaka wanajua kuwa ana kosa la jinai la kughushi vyeti na hajashitakiwa?
TUMIA AKILI,ACHA USHABIKI
 
Acheni ujinga ninyi,hapa hakuna kinachoendelea ni usanii mtupu,hakuna mtu anaevamiwa na asiende kutoa taarifa kituo cha polisi,na kingine unavamiwa ijumaa usiku,jumamosi asubuhi unaenda kw aliekuvamia na kupiga soga,hii inawezekana kweli?siku zote adui hawezikuwa rafiki ila rafiki anawezakuwa adui.wabeja sana
 
innercircle.png
Mmoja kazungusha.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Hata kama kwa ubinadamu wetu tutatashindwa kusimama na huyu ndugu hususan kwa kipindi hiki yupo Mungu aliye hai atamtetea.

Ndio, Hakuna binadamu asiye na mapungufu, Ruge kama binadamu inawezekana ana mapungufu yake lakini katika hili suala la Clouds Vs "Yule Bwana" kwa binadamu mwenye akili za kawaida tu utakubaliana nami kwamba Ruge ameonyesha hekima na busara ya kiasi cha juu sana.

Alichoamua Kukisimamia Ruge ni kusema UKWELI, Ukweli kwamba "Yule Bwana" alikosea, pamoja na kwamba walikuwa marafiki lakini Ruge aliamua kusimama katika misingi ya ukweli, misingi ya kikazi, Kwamba "Yule bwana" alikosea. Kuna vitu wala havihitaji degree kuvielewa, yaani kule tu kwenda pale tena usiku tena na silaha bila mhusika kujua, na bila warrant ni kosa kisheria.

Leo baada ya kumsikia Ruge akijibu shutuma za "Yule Bwana" nimejisikia amani sana, Maana badalaa ya kujibu kwa jaziba, kwa matusi, kwa mhemko, Ruge kajishusha kaongea kwa ustaarabu kama binadamu, Pamoja na kuambiwa hana akili, anaimba ngonjera, na maneno mengine mengi ya kuudhi lakini jamaa kajibu ki proffesional na kwa unyenyekevu. U have my respect brother.

Mi nafikiri kama taifa kama tunakuwa na viongozi wa namna hii, ambao wanashindwa kuwa na akiba ya maneno na kuongea tu kama vijana wa mtaani bila kuangalia kuwa kuna watu wengi sana tunawaangalia ili kujifunza kwao, tutakuwa tunaelekea pabaya sana.
Anajijua alivyo na akijibu hovyo wakimuunganishia doti atapotea, ukijijua mapungufu yako lazima uwe mpole. Hujiulizi kwanini kesi ya uvamizi haikuripotiwa polis? Hujiulizi kwanini taarifa ya uvamizi waliitoa wengine wakati mmiliki alitoa ufafanuzi tu? Hujiulizi kwanini bwana yule ametumia maneno chokozi kwa Ruge?. Bwana yule amefanya vile kama mtego na Ruge angejichanganya tu huenda tunge yasikia mengi. Hawa jamaa wanacheza na akili zetu tu, ngoja niingie shamba nikafanye yanayo nihusu
 
Back
Top Bottom