Huyu ndiye Ruge ninayemfahamu!

Mh, wabongo wengi ni mateka wa propaganda!! Naomba mwenye clip ya Ruge anirushie, mana imekuwa adimu
 
Anajijua alivyo na akijibu hovyo wakimuunganishia doti atapotea, ukijijua mapungufu yako lazima uwe mpole. Hujiulizi kwanini kesi ya uvamizi haikuripotiwa polis? Hujiulizi kwanini taarifa ya uvamizi waliitoa wengine wakati mmiliki alitoa ufafanuzi tu? Hujiulizi kwanini bwana yule ametumia maneno chokozi kwa Ruge?. Bwana yule amefanya vile kama mtego na Ruge angejichanganya tu huenda tunge yasikia mengi. Hawa jamaa wanacheza na akili zetu tu, ngoja niingie shamba nikafanye yanayo nihusu
Unaonekana Pamoja na uwezo wa akili yako, unayajua mengi ambayo kwa wengine siye bado sirini. Ebu funguka zaidi kwa faida ya kizazi hiki!!
 
Labda unamaslahi na wauza ngada bosi
Ngada ndio nini au ni udaga? Bahati mbaya sana hilo suala limekuwa kama propaganda ya bwana yule wako.Marekani na utaalamu wao na rasilimali walizonazo hiyo vita ya madawa imewashinda eti aibuke mtu hata vyeti hana eti anapambana kihovyo hovyo namna ile?.Mtuhumiwa unamwambia eti tukutane kituo cha kati ijumaa kwa uchunguzi sasa kwa akili yako hivi kweli ntasubiri mpaka uje unipekuwe hiyo ijumaa unikute nayo? Wewe acha mahaba ya hivyo hapo bashite elewa kabisa alikuwa anawasanua na kuwakimbiza watuhumiwa kijanja mwishoe anakwenda kukamata watu ambao sio kabisa.Unakwenda kumkata Gwajima? Hivi Kweli uko seriazi na vita hiyo?Bahati yake maana alikaribiwa kugeuzwa sembe
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Hata kama kwa ubinadamu wetu tutatashindwa kusimama na huyu ndugu hususan kwa kipindi hiki yupo Mungu aliye hai atamtetea.

Ndio, Hakuna binadamu asiye na mapungufu, Ruge kama binadamu inawezekana ana mapungufu yake lakini katika hili suala la Clouds Vs "Yule Bwana" kwa binadamu mwenye akili za kawaida tu utakubaliana nami kwamba Ruge ameonyesha hekima na busara ya kiasi cha juu sana.

Alichoamua Kukisimamia Ruge ni kusema UKWELI, Ukweli kwamba "Yule Bwana" alikosea, pamoja na kwamba walikuwa marafiki lakini Ruge aliamua kusimama katika misingi ya ukweli, misingi ya kikazi, Kwamba "Yule bwana" alikosea. Kuna vitu wala havihitaji degree kuvielewa, yaani kule tu kwenda pale tena usiku tena na silaha bila mhusika kujua, na bila warrant ni kosa kisheria.

Leo baada ya kumsikia Ruge akijibu shutuma za "Yule Bwana" nimejisikia amani sana, Maana badalaa ya kujibu kwa jaziba, kwa matusi, kwa mhemko, Ruge kajishusha kaongea kwa ustaarabu kama binadamu, Pamoja na kuambiwa hana akili, anaimba ngonjera, na maneno mengine mengi ya kuudhi lakini jamaa kajibu ki proffesional na kwa unyenyekevu. U have my respect brother.

Mi nafikiri kama taifa kama tunakuwa na viongozi wa namna hii, ambao wanashindwa kuwa na akiba ya maneno na kuongea tu kama vijana wa mtaani bila kuangalia kuwa kuna watu wengi sana tunawaangalia ili kujifunza kwao, tutakuwa tunaelekea pabaya sana.

Ruge amemwacha "bwana yule" mbali sana kifikra! Hata kama Ruge ni mtunga ngonjera, kuna haja gani ya kudharau hiyo kazi yake. Nakuhakikishia bwana yule, haendi mbali. Mwisho wake ulishafika na "karma" imeanza kumtafuna. Anajifanya kumjua mungu sana wakati anadharau na kwa hao hao watu wa Mungu. Na haya maneno yake ya kujikomba kwa Mungu mchana wakati usiku yupo kwa waganga ndo atajikuta anajenga Babel siku sio nyingi.

Big up sana Ruge kwa kuonyesha ukomavu na bwana yule hana uwezo wa kushindana na watu wenye weledi hata siku moja, mind at your passion brother!!
 
Ruge ni mnafiki Mkuu, alipokubali kutumikia magwiji wa Dawa za kulevya kwa kusingizia kituo chake kimevamiwa.

Kushindwa kuthibitsha tukio hilo, au kufungua jalada polisi
tunapotezaga muda tu bwanah ...nadhani tuwaachie tu wenyewe jamani....haya mambo ukiiingia ndani utakutana na mengi pia uko...wanajuana wenyewe tu hao
 
Fabian the jr umeongea point sana kweli hapa tuma watu wawili tofauti nilio waona Ruge mwenye akili na ufahamu na huyu DAB zumbukuku jinga asiyejua anachofahamu big respect kwa ruge
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Aibu kwa nchi,aibu aibu kwa kuwa na tuviongozi kama hutu tu bashite.

Aibuuuuuuu

Hana cheti.
Aisee,Nyerere fufuka baba nchi imekuwa ya hovyo
 
Ngada ndio nini au ni udaga? Bahati mbaya sana hilo suala limekuwa kama propaganda ya bwana yule wako.Marekani na utaalamu wao na rasilimali walizonazo hiyo vita ya madawa imewashinda eti aibuke mtu hata vyeti hana eti anapambana kihovyo hovyo namna ile?.Mtuhumiwa unamwambia eti tukutane kituo cha kati ijumaa kwa uchunguzi sasa kwa akili yako hivi kweli ntasubiri mpaka uje unipekuwe hiyo ijumaa unikute nayo? Wewe acha mahaba ya hivyo hapo bashite elewa kabisa alikuwa anawasanua na kuwakimbiza watuhumiwa kijanja mwishoe anakwenda kukamata watu ambao sio kabisa.Unakwenda kumkata Gwajima? Hivi Kweli uko seriazi na vita hiyo?Bahati yake maana alikaribiwa kugeuzwa sembe
Haya bwana mdogo wake gwajima nilikuwa sijakusoma kumbe unamtetea yule jamaa anayejiita askofu sijui mchungaji
 
Njia ya muongo wala si ndefu ni fupi sana.Angalau hili lina pia ushahidi wa picha japo sina hakika kama kimahakama utapokelewa.Ushaidi mwingine utapatikana kutoka kwa waliokuwa studio ilipovamiwa na wale ni mashaidi na kitakachotolewa kwao ni ushaidi ni hali halisi ya tukio iwe itambana ruge ama bashite huo ni ushaidi na ndio ukweli Ama uongo wa tukio
Dah.... Mbona Kesi zinatengenezwa tu... framed.... cha msingi kuwe na mtandao na pesa
 
Ruge ametumia namna sahihi kabisa kuhakikishia umma kuwa yuko tayari kwa suluhu lakini Bashite kwa kuwa amebebwa na hivyo kutojua umbali wa safari aendayo hataki hili suala liishe.
sasa wakati ambao yeye atakapokuja kufahamu umbali wa safari atakuwa tayari yuko chini ya mgongo ulimbeba na ruge akawa pale alipo.:
maana kashaanza kukimbia dar siku hizi mara utasikia yuko Mwanza,Arusha ,Moshi nk.
Ukiona mtu bado anaendelea kumtetea bashite kwa maelezo hayo aliyoyatoa bwana Ruge,Rudi kwenye ile tafiti kati ya watz wa 4 mmoja ni KICHAA.
Mtihani wa fotm six umeisha?
 
Ruge ni mnafiki Mkuu, alipokubali kutumikia magwiji wa Dawa za kulevya kwa kusingizia kituo chake kimevamiwa.

Kushindwa kuthibitsha tukio hilo, au kufungua jalada polisi
882e272d96ad6e9898e11de7c53dfd69.jpg
 
Yaani umeokoteza uwongo wa Bashite halafu unauleta hapa? Utasemaje kesi ya uvamizi haijaripotiwa polisi wakati Sirro anasema polisi wanaendelea na upelelezi? Kwa akili yako wewe na Bashite mwenzako polisi wanafanya upelelezi kwa tukio ambalo halikuripotiwa polisi?

Sasa hivi tuko kwenye issues za kitaifa tuachane na upuuzi wa Ruge
 
Back
Top Bottom