Huyu ndiye PDG Ndama Mutoto ya Ng'ombe

rushwa-mke-mume.jpg
 
aaah hamna kitu... yaani alichotoa hapo ni kati ya laki moja na nusu hadi moja themanini haijafika hata mbili... yaani hao ndio vibopa wenu mjini bac mmeishiwa ... mwereve hawezi kufanya upuuzi huo.....
 
Huyu kweli mtoto wa ng'ombe hana akili sawa sawa. Kwanini asiende kusaidi maskini huko vijijini akaoneka wa maana zaidi?

Walio mwita toto ya ng'ombe hawakukosea maana angekuwa na akili angeitwa the son of a king
 
Acheni wivu na kelele za kujidai mna maadili sana. Anagawa pesa yake anakotaka kama wafadhili wanavyoigawia hela nchi yetu pamoja na kwamba hatujui kuzitumia kwa maendeleo yetu. Suala la kugawa hela sio tatizo. Kwamba kazipata vipi hapo ndo kunawezekana kuwa na tatizo.
 
mshkaji ni mjanja kwa style ya maisha aliyoyachagua...anachofanya si ulimbukeni au kuonyesha ana pesa nyingi,bali ni style za kimjini kujipa promo hususani katika biashara zake za udalali.unaweza usiamini kwa style yake hii ndama kuna washamba kibao wa mikoani wapo tayari kuuziwa na ndama gari la thamani ya milioni 9 kwa milioni 12....hii nimeishuhudia mtu anapigwa bei kali na ndama na anajisikia raha kuuziwa gari na yeye mpaka akawapasha habari ndugu zake kama ni ndama mwenyewe ndiye kamuuzia gari......ni mbinu tu za kukabiliana na maisha magumu ya kibongo!
 
ndama, mtoto wa ng'ombe..........haya majina sijui huwa yana reflect tabia ya mtu
 
Ye mwenyewe anajiita mtoto wa ng'ombe , unategemea atakuwa na akiri za maana? babayake ni ng'ombe mtoto ni ndama. hakuna kitu hapo
 
Eti Ndama PDG, Usilolijua usiku wa kiza. Mi kwangu Ndama always ni hanger on na tapeli tu.
 
yaani mijitu mingine inapewa sifa bila sababu za msingi, eti huyu naye ni role model bongo. period!


Ndama mbaroni kwa wizi



na Betty Kangonga




JESHI la Polisi nchini linamshikilia mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Ndama Shabani (38) au Ndama mtoto wa Ng'ombe kwa tuhuma za kukutwa na gari la wizi.

Pamoja na Ndama, wengine wanaoadaiwa kuhusika na wizi huo ni Sylvester Mashindila (45), Richard Marimi (46), Peter Goyayi (30) au Makoye wakazi wa Mwananyamala kwa Kopa na Charles Mwita (43) mkazi wa Kinondoni.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Kamishna Msaidizi wa Polisi na Kamanda wa Kanda Maalum Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walipora gari aina ya Hino lenye namba FDIJKD 11185 maeneo ya Tunduma mkoani Mbeya.

Kova alisema kikosi Maalum cha Kupambana na Wizi wa Magari ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam kilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wanaodaiwa kumnywesha dawa za kulevya aliyekuwa dereva wa gari hilo kabla ya kumpora.

Alisema gari hilo lilibeba bidhaa mbalimbali vikiwemo vitanda vinne, magodoro, majokofu, makochi na majiko ya umeme ambapo watuhumiwa hao baada ya kutenda tukio hilo walikimbilia mafichoni jijini Dar es Salaam na kuvihifadhi vitu hivyo Mbezi nyumbani kwa Ndama.

Source: Tanzania Daima



Na ile ya albino sijui iliishaje?
 
Back
Top Bottom