Huwa sielewi watu wanatoa wapi Uhalali wa kumfananisha Mwanamuziki Fally Ipupa na Feregola!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Hivi huwa mko Serious au huwa mnatania?,yaani Mwanamuziki Fally Ipupa mnamfananisha na Fere Golla?

Sijajua aliyeanzisha huu mpambano kama yuko timamu kichwani.

Koffi olomide amewahi kukaliliwa akisema "Moja kati ya waimbaji na wana jumuia wangu wa bendi ya QUARTIER LATIN ambao sitoweza kuwasahau ni Fally Ipupa,huyu mtu amebarikiwa kipaji cha aina yake katika muziki,bila shaka ukimtoa Marehemu Papa Wemba na mimi,basi atakuwa anafuata yeye"

Kwa maneno hayo ya Mkongwe na Gwiji la muziki wa Dansi na Rhumba kutoka Africa bila shaka Fally Ipupa ni Habari nyingine kabisa!.Vijana huyu Fally Ipupa uenda mtakuwa mmejua juzi tu baada ya kutoa wimbo wa Bakandja,Maria na Mayday!.

Lakini mimi mkongwe na wakongwe wenzangu tunaomfahamu Fally Ipupa toka Enzo hizo akiwa Stage Show na Singer wa Koffi Olomide kutoka bendi ya QUARTIER LATIN wala hatushangai namna alivyo hatari!

Vijana niwapendekezee tu,kama humfahamu Fally Ipupa hebu nendeni karudieni show aliyoifanya Dar es salaam mwaka 2009 ndo mtaelewa ni mtu wa aina gani!(Nendeni YouTube huko mtaikuta hii show)

Kwenye ile show walipanda wasanii wenu mnaowaaminia Amini & Barnaba wakaimba wimbo unaoitwa KIDIAMFUA,aiseee nilicheka sana maana wale wasanii wenu ni kama walikuwa wanaigiza siyo kuimba😂,hapa ndipo nilijua hakuna msanii kitoka Tanzania anayejua kuimba bali huwa ni wababaishaji tu!

FALLY IPUPA acheni kabisa kumlinganisha na watoto wadogo katika muziki!
 
Back
Top Bottom