Huyu ndiye Freeman Mbowe wa CHADEMA

Kiongozi mahiri asifiwi kwa kuongea sana na watanzania tunapotoka na maneno kuliko vitendo,inanikumbusha siku za nyuma kwamba kulitokea msimulizi wa masuala ya mpira anaejiita Dr Rick kuna watu walidiriki kusema apewe timu ya mpira kuiongoza au hata kumuita profesa kwa kuliongelea soka tu.Mbowe hana uwezo ambao mtoa uzi hapo juu anajaribu kumsifia na hatokuwanao kwani katika nafasi yake ya uenyekiti ameshindwa katika mambo mengi ikiwapo kuleta umoja na mshikamano ndani ya CDM.Sio siri mpasuko ndani ya chama ni mkubwa na unaendelea kukua siku hadi siku lakini na ameshindwa kuona athari zake na kuzuzuka na kelele za mashabiki nje ya majukwaa ambao hana uhakika kama wote wanamuunga mkono ama la.Sitoshangaa kuona mashabiki wa CDM wakiendelea kuwapamba viongozi wao kwa nderemo na sifa lukuki hata kwa yale ya kijinga na kuacha kuwakosoa katika mambo ya msingi.Viongozi wa juu wa CDM wamegueka mitume na manabii,ingekuwa ni vyema kama mtoa uzi angetaja na yale ambayo Mh Mbowe ameyafanya ndani ya chama,bungeni kama kiongozi wa upinzani na jimboni kwake si kuleta hotuba ambayo inawezekana ameandikiwa na kukabidhiwa kuisoma.

SIUNGI MKONO HOJA YA MTOA UZI MPAKA AJE NA DATA.
 
Mkuu nikurekebishe kidogo. Hamwogopi Mungu bali ana hofu ya Mungu. Kuwa na hofu ya Mungu ni kutenda anachotaka Mungu bali kumwogopa si lazima utende atakacho.

Hata Lusifa, kama ilivyo kwa wafuasi wake, anaongoza kwa kumwogopa Mungu bali hatendi yaliyo yake. Heri kuwa na hofu ya Mungu kuliko kumwogopa. Ogopa sana mtu anayemwogopa Mungu.
 
Dudus, hukunielewa. Sasa tuhamie kwa wazungu: "Fear of God is the beginning of Wisdom." Ukitaka kiyunani au Kiebrania nijulishe!
 
Unacho kichangia kinasadifu uwezo wako wa kufikiri. Kwenye hotuba nzima umesikia peoplez power peke yake?! Na hiyo peoplez power imetanguliwa na maneno gani?!

Mkuu ritz wewe acha ushabiki na wenge la asubuhi asuhi! Isikilize tena hiyo hotuba, najua itakuwa unasikiliza labda kwa mara ya pili au tatu, usichoke sikiliza tena hata ukiwa umejificha peke yako utapata neno lingine sio hilo la peoplez power peke yake.

Wanao kutumia waambie wasikutumie vibaya au kama unapenda kutumika vibaya jitwishe utashi kidogo kichwani mwako.

Kazi njema kama utakwenda kazini.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.

Wewe kweli kauzu unavyotumwa wewe na Mbowe unadhani watu wote ni watu wa kutumwa.

Wewe Mbowe ndio unamuona kiongozi makini sababu alikuwa DJ na anakupa kula, lakini mbele ya jamii ya watanzania Mbowe ana lolote kama unakumbuka aligombea urais kilichomkuta kamuulize atakuambia kura alizopata au ulikuwa bado mtoto Chadema naijua toka enzi za Mwenyekiti Mtei, Mwenyekiti Bob Makani, na Katibu Mkuu Dr Amani Kaburu, wakati wewe bado unasoma Machame.

Kama wewe unamjua Mbowe na uwezo wake wa kuongoza niambie elimu yake kasoma wapi nyie si mnasema Chadema chama cha wasomi.
 
Kama kuna mwanasiasa huwezi kuchoka kumsikiliza ni ndugu Mbowe. Ana haiba na sifa za mwanasiasa. Kinachomponza ni chuki zinazopandikizwa na CCM dhidi ya CDM ili kukipunguzia nguvu chama hicho ka propaganda za udini na ukaskazini ambazo hazina ukweli wowote.
Wanaoeneza hofu kwa wananchi eti ni mpiga disko hawajui hata kama angekuwa ni DJ hiyo haiwezi kuondoa ueledi na uwezo wa mtu kiuKupiga disco inaweza kuwa hobi ya mtu lakini.akiwa na sifa na fani zingine tofauti na uwezo hata wa kwenda angani, kuwa daktari, mwalimu, mfanyabiashara nk.
Ndg Mbowe ni mfanyabiashara na ni mtu anayejua kupanga maisha yake vizuri, ni.mpigania haki na mabadiliko katika nchi yetu vipi wewe uliyeshindwa kufungua hata kibanda cha karanga uanze kubwabwaja eti ni mpiga disco. Watanzania katika ulimwengu wa sasas huwezi kufika popote kama huna wanaharakati wenye fedha walionitolea kupigania mabadiliko. Usidanganyike wanasiasa wasiokuwa na uwezo.wa fedha ni rahisi kudanganyika kwa vyeo na fedha za watawala. Watapiga kelele lakini mwisho wa sku watakaaa kimya kwani vitisho na kurubuniwa ni rahisi kwa wanasiada njaa. Sisemi kuwa mtu hawezi kuwa mwanadiada maskini lakini akawa mzuri, nnachosema ni kuwa anaweza kuwepo lakini kupambana dola kongwe kama ccm itakuwa ni ngumu. Mara nyingi matajiri hawataki kujiunga na harakati za kuleta mafiliko waziwazi kwa hiyo mkimpata mtu kama Aikaeli mna bahati ya kipekee. Wanaotaka kuzima uwezo wa Mbowe kwa kumuita mpiga disco misha kuishia hapo bila kutaja kuwa ni msomi, mjasiriamali, mwanaharakati na mwanasiasa mahiri anakosea. Aanacheza propaganda tu.
 
Katika miaka mingi ilopita sijapata kusikia Hotuba nzito na yenye maudhui mazito kama ya Mhe. Freeman Mbowe aloitoa Washington DC mwaka 2012.. Ni hotuba hii inayonipa ushawishi mkubwa kwamba Chadema ile sio hii ya leo. Unaweza kuipata hapa
 
taarifa iliyonifikia hivi punde ni kwamba , leo shughuli zote zimesimama wilayani kyela kwa ujio wa kamanda mbowe , unaambiwa shughuli za uvunaji mpunga zimesimama kabisa , hakika ukombozi umefika .
 
Katika miaka mingi ilopita sijapata kusikia Hotuba nzito na yenye maudhui mazito kama ya Mhe. Freeman Mbowe aloitoa Washington DC mwaka 2012.. Ni hotuba hii inayonipa ushawishi mkubwa kwamba Chadema ile sio hii ya leo. Unaweza kuipata hapa
ngoja tukuwekee hotuba ya kamanda anayoitema hivi sasa kyela , cc - Stand alone .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom