Huyu ndiye Freeman Mbowe wa CHADEMA

kwako mohamed mtoi,

aisee ilikuwa kiboko, kaka tunaomba kwa heshima na taadhima utupatie basi kipande cha maswali na majibu maana tutakuwa tumepata picha kamili once again thanks for the posted clip, it was really educative.
 
Kuna haja sasa kama sio ulazima wa JF kufanya sensa ya kufahamu umri, weredi na fikra za MEMBERS wake, huwezi mtu mzima na akili timamu katika ulimwengu wa leo kustahajabishwa na kumsifia mtu kwamba anajua kuongea, heti ana madini?

Hii nchi tumeshasikia kila tunachotaka kusikia, kilichobaki ni kuona na kushika ambayo hiyo kazi tumewaachia na tutaendelea kuwaachia CCM waifanikishe kama Ilani ya chama inavyotafsiri, wewe kama unatamani kuendelea kusikiliza hao waropokaji kawafate bilicanas ukawasikilizie live huko sio kwenye Youtube videos.
Punguza jazba ndugu,sidhani kwa kauli zako kama hizi kunaondoa ukweli wa Thread hii kwamba wananchi kwa mamilioni wana-support CDM kutokana na weledi wa viongozi wake akiwemo kamanda wa anga mhe. Mbowe. 2015 utaisoma namba,tuijenge nchi yetu
 
Wakuu.

Mtakumbuka kuwa nilisha wahi kuandika hapa jukwaani kuwa kwa sasa hivi hapa Tanzania hakuna mwenyekiti wa chama chochote cha siasa mwenye influence na anae tema madini mdomoni akiongea kumzidi kamanda Freeman Mbowe.

Ukiweka ushabiki pembeni na kusimamia ukweli, Mbowe amekuwa mwenyekiti mwenye mvuto wa kipekee kwenye medani za siasa za Tanzania kwa sasa kuliko mwenyekiti wa chama chochote cha siasa.

Japo najua watanzania wana kiu na njaa ya mabadiliko ambayo naamini wamekata tamaa kuyapata ndani ya ccm naamini uwezo na influence ya Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chadema imechangia sana kuiweka chadema kwenye ramani iliyopo sasa.

Asiye amini kuwa Mbowe anatema madini mdomoni atafute hotuba zake au asikilize kwa makini hii hapa chini

Ukipenda chongo, unaona...?
 
Kamanda wa Anga! Namkubali sana hasa anaposema "tunazungumzia mustakabal wa taifa letu!"
Ukurasa wa 107 wa Kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu kuna aya inasema ....Akichangia mada Sajinihitaji Friimani alisema "Nchi yetu ni mali yetu sote tuliyopewa na Mungu kwa umoja wetu. Hakuna Chama cha siasa chenye hakimiliki ya nchi hii. Hata chama tawala hakina hakimiliki hiyo.
Akitetea hoja ya Utaifa Friimani aliendelea.."Siku za kampeni na uchaguzi huja na kupita lakaini Taifa hubaki.Lazima Taifa libaki moja na lenye mshikamano baada ya uchaguzi....Hakuna nafasi ya chuki. kejeli au utengano wowote wa kiitikadi kwa walioshinda na walioshindwa"
Huyu ndio Freeman Mbowe kama alivyoonyeshwa na Mwandishi wa Kitabu Cha Mwalimu Mkuu wa Watu
 
Anachoongea Mbowe kinamtoka moyoni, ni ukweli usiopingika kwa kila mtanzania. CCM imechoka na sasa tuiweke pembeni. Inatakiwa akili za maiti kuipenda na kuishabikia CCM.
 
Kuna haja sasa kama sio ulazima wa JF kufanya sensa ya kufahamu umri, weredi na fikra za MEMBERS wake, huwezi mtu mzima na akili timamu katika ulimwengu wa leo kustahajabishwa na kumsifia mtu kwamba anajua kuongea, heti ana madini?

Hii nchi tumeshasikia kila tunachotaka kusikia, kilichobaki ni kuona na kushika ambayo hiyo kazi tumewaachia na tutaendelea kuwaachia CCM waifanikishe kama Ilani ya chama inavyotafsiri, wewe kama unatamani kuendelea kusikiliza hao waropokaji kawafate bilicanas ukawasikilizie live huko sio kwenye Youtube videos.

Mkuu
Ulicho kifanya kinaitwa na character assassination! Umeacha kujadili hoja iliyooko mezani una hoji utimamu wa akili yangu?! Hahaha. Hivyo ndivyo anavyo fanya kaka yenu Nape , baadala ya yeye awe ana jibu hoja za Dr Slaa huwa anakimbilia kusema Dr Slaa ana zeeka vibaya huku akiziacha hoja bila majibu.

Nilicho kitegemea kutoka kwako wewe ambaye ni great thinker kuliko mimi unaye nitilia shaka utimamu wangu ni hoja zenye mashiko kuwa labda mbowe kwenye speech zake ana mapungufu 1,2,3... Na labda kwa sasa anaye mzidi kwa kuongelea mustakabali wa taifa lake ni flani au flani na kwa vigezo vya kuweka speech kama nilivyo fanya mimi.

Nakushauri uwe mpole kama huna cha kuchangia.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Ungeweka na CV yake ndio tumjue vizuri, Sitta anamuita DJ. na wengine wanasema anatema madini sijui madini gani.
 
Hivi kusema hakuna kulala mpaka kieleweke, pipooz power...haya ndio madini ya chumvi uvinza.
 
Mnasahau Hotuba ya Lipumba? ile mm ndio naitafuta maana imekusanya mambo mengi mneiweka hapa maana ilianza kwa sala na Hotuba ya Duni Haji akisisitiza wana DINI wote wahamie CUF
 
mbowe jembe. hasa akiongea kwa msisitizo mimi huwa napata machungu natamani niandamane peke yangu mpaka magogoni
 
Hivi kusema hakuna kulala mpaka kieleweke, pipooz power...haya ndio madini ya chumvi uvinza.

Unacho kichangia kinasadifu uwezo wako wa kufikiri. Kwenye hotuba nzima umesikia peoplez power peke yake?! Na hiyo peoplez power imetanguliwa na maneno gani?!

Mkuu ritz wewe acha ushabiki na wenge la asubuhi asuhi! Isikilize tena hiyo hotuba, najua itakuwa unasikiliza labda kwa mara ya pili au tatu, usichoke sikiliza tena hata ukiwa umejificha peke yako utapata neno lingine sio hilo la peoplez power peke yake.

Wanao kutumia waambie wasikutumie vibaya au kama unapenda kutumika vibaya jitwishe utashi kidogo kichwani mwako.

Kazi njema kama utakwenda kazini.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Mbowe ni jembe la ukweli, ana hekima nandiyo maana mara nyingi amekuwa akitengua tungo tata za viongozi wenzake wawapo mjukwaani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom