Mimi bado napinga Uamuzi wa Magufuli wa kuwasamehe kina Babu Seya hata Kama ni uamuzi halali!
Nategemea Mashirikia ya haki za Watoto wapinge nao!
Watu wameenda mpaka Court of appeal na wamefanya review ya Kesi bado wamekutwa na hatia Halafu wanaachiwa kwa kweli sijaipenda hata Kama Rais Ana haki hiyo!
Maamuzi kama haya yanafanya wanainchi waweze kutafakari umuhimu wa kuwa na sheria na katiba bora zaidi. Hili ni swala moja kati ya mengi ambayo yanahitaji mabadiliko makubwa kwenye sheria za nchi hii. Mkuu anaweza akawa hana kosa kwa sababu sheria imempa nafasi hiyo. Lakini sisi wengine tunajifunza nini?