Huyu mwanaume simwelewi kabisa

Huyu mwanaume simwelewi kabisa

Kuna vitu naviona.

1. Issue ya kuja kula kwako.

Kwanini kwako? Kwanini usiende kupika kwake? Umeshawahi kwenda kwake?

2. Inawezekana unajiproud sana, tofauti na uhalisia wa kipato chako. Kwa maana hiyo yeye anaona upo vizuri na huna shida.

3. Inawezekana huyo jamaa ni sawa na wale watu ambao mpaka "apigwe kichwani" ndiyo channel ikamate.

Design hii mpaka umwambie anunue vitu, ndiyo ataanza, lakini kwa sasa wala haoni kama anafanya kosa.

4. Majibu yako kwenye huu uzi hayana ule uzito wa shaba, wengi wanashindwa kukujibu inapasavyo.

5. Ifike pahala, mapenzi ya kinafik tuyaweke pembeni, kama una issue inakusumbua, iseme kwa mwenza wako, kwa upole wote.
 
Wew ni kwaajili ya kumpikia tuu

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
733be0580fe2c3a1b0fdd095c87c472f.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
🙂🙂 NO WAY OUT🙂🙂🙂 TELL HIM THE TRUTH AND WAIT THE RESULTS = TELL HIM AS YOU MAKE JOKE""""
 
Jamani naombeni ushauri wenu ndugu zangu nilikua na rafiki wa kiume close friend yaani tulikua marafiki hasa kiasi kwamba haiwezi pita Masaa 2 hatuwasiliani usiku tunaongea mpaka SAA 5 usiku.

Kuna siku alienda kazini akachelewa kutoka akanipigia best ndio nafika alafu gesi imeisha kwakua ni rafiki sikuona ajabu nikamwambia njoo ule huku akaja kula Sijui kilitokea nini tukajikuta tupo katika mahusiano ya kimapenzi kweli mi nilikua nampenda sana before nadhani hata yeye.

Sasa kilichofanya niombe ushauri ni tabia ya jamaa kifupi tumepanga kufikia December tuwe tumesha tambulishana kwa wazazi lengo tuje tuishi pamoja ambacho simuelewi jamaa anaweza piga simu pika nakuja kula kweli najipinda napika anakula anaondoka au anaweza pata mgeni akaniambia piga ninamgeni tunakuja kula nawapikia jamaa hanunui hata mboga wala tu kujiongeza angalau alete hata nyanya tu hapana

Yeye ana kazi nzuri analipwa karibia 1million per month mimi mbangaizaji tu lakini hata huruma hana nashindwa nimuelewe juzi aliniambia njoo uninunulie lunch nikamwambia sina hela basi.

Jana kaja nimekuja kula ikabidi niandae chakula akala akaondoka jamani nashindwa kumuelewa ni mtu wa aina gani mi sio muongeaji sana nashindwa kumuambia nataka niachane nae je naanzaje? maana ukweli nampenda Jamaa ana 36 mimi nina 30.
Naombeni ushauri wenu
mjini shule sio urefu wa maghorofa
 
Hamna mtu hapo, kwa umri wake si mtu wa kuanza kumuelekeza mambo madogo madogo kama hayo, litakapokuja swala la mimba si
ndio atapotea kabisa.
mwanaume akishakuzimia, hujibebesha majukumu bila hata kuambiwa.
Ndicho hicho nachokisema kila siku...

Huwa mwanaume akikupenda anajibebesha zigo hasa na hata hajali!

Wee ukiona hakujali tuu kula kona hakuna mapenzi hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom